Mwenyekiti wa Umoja wakinamama wa Chama Cha Wananchi (CUF) taifa Bi Aziza Nabahani Suleiman akimkabidhi Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Bi Awena Sanani Masoud mashuka na dawa za kusafishia hospitali ili amkabidhi Naibu Waziri wa Afya Dk Sira Ubwa Mamboya katika hafla iliyofanyika hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
HOSPITALI ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini Unguja imepatiwa msaada wa vifaa vya hospitali mbali mbali kutoka kwa Jumuiya ya akina Mama wa Chama Cha Wananchi (CUF) na kutakiwa kuvutumia vizuri.
Akikabidhi msaada huo Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Sanani Masoud aliwataka wafanyabiashara, Wabunge Wawakilishi na wafadhili mbali mbali kuona umuhimu wa kusaidia jamii hasa katika mahospitali ili kutoa nguvu kwa seriklai .
Aidha Bi Awena amezitaka taasisi nyengine kujikita na kujikijitokeza kutoa misaadakamahiyo katika hospitali ambazo zinakabliwa na matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa vifaa muhimu vinavyotakiwa kutumiwa na wagonjwa katika hospitali hizo.
Msaada huo ulitolewa na Jumuiya ya Wanawake wa CUF ni pamoja na mashuka ya vitanda 70, mipira ya kulalia 42 na  madawa ya kusafishia hospitali hiyo maboksi mawili
Alisema suala la kutafuta misaada ni la kila mmoja na taasisi na sio kuiwachia serikali peke yake kwani kufanya hivyo ni kuisaidia serikali katika jitihada zake za kupunguza matatizo katika hospitali hizo ambapo kwa kiasi kikubwa serikali imekuwa ikijitahidi kutaka wananchi wapate huduma bora na ziwafikie walengwa ikiwa pamoja na kuimarisha huduma katika sekta ya afya.
Bi Awena alisema serikali ya umoja wa kitaifa ina miezi michache ni vyema kuweka mazingira mazuri ili kuonekana Zanzibar ni mpya inaanza na mwelekeo  wenye mazingira mazuri ya wananchi wake kusaidia juhudi za serikali kwa kutoa michago yake katika sekta za elimu na afya na sekta nyengine muhimu ambazo zitawasaidia wananchi wake.
“Nina amini kwamba misaada hii mtaitumia vyema na kwa umakini kabisa kwa sababu kile kinahcopatikana kitolewe na kitumiwe vizuri na nina namini kwamba ile fedha iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya mashuka na dawa za kusafishia hospitali basi itatumika kwa shughuli nyengine kwa kuwa hivi sasa mmepata mashuka, mipira na dawa za usafi” alisema Bi Awena ambaye kitaalum ni Mwalimu.
Katika kuhakikisha misaada inaongezeka Bi Awena alisema hata Dk Shein amekwenda Uturuki kwa lengo moja kuitikia mualiko wa kiongozi wa nchi hiyo lakini zaidi ni kuomba misaada katika nchi hiyo kwa ajili ya wananchi waZanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk Sira Ubwa Mamboya aliwashukuru kina mama hao na kuahidi kwamba serikali inaunga mkono juhudi zote zinazochukuliwa na tasisi zinazotoa misaada hiyo kwa kuisaidia sekta ya afya kwani kufanya hivyo ni kusaidia serikali na wananchi wake.
Nae Daktari dhamana wa Hospitali hiyo ya Kivunge Dk Mtumwa Ibrahim amesema hospitali hiyo ni ya wilaya lakini ina uwezo wa kushughulikia mkoa mzima wa kaskazini ingawa kesi zisizo za kawaida huhamishiwa hospitali kuu Mnazi mmoja lakini huduma nyingi za matibabu hutolewa hapo hapo Kivunge.
Alisema hospitali hiyo inatoa huduma za ndani na nje na ina uwezo wa kulaza wagonjwa 53 wakiwemo wa kike na wa kiume pamoja na watoto ambapo licha ya udogo wake lakini imekuwa ikijtahidi kuwahudumia wagonjwa mbali mbali.
Dk Mtumwa alishukuru ujio wa wanawake hao na kuahidi kwamba vifaa viivyotolewa vitawasaidiasanawagonjwa ambapo alisema mshuka watayatumia kwa kutandikia vitanda vya wodi za akina mama huku mipira itawekwa katika vitanda vya watoto ambapo awali walikuwa na upungufu wa mipira ya watoto katika hospitali hiyo.