Waziri anasema wazanzibari hawana sifa na vigezo vya kuingia jeshini kutokana na kutokuwa na vyeti hilo ni kweli lakini au kuna sababu nyengine zaidi ya hiyo?kufuatia hilo ndio vijana kutoka Tanzania Bara wanakuja Zanzibar kuja kuwania nafasi hizo na matokeo yake huingia jeshini kupitia fursa hiyo si wazanzibari hawana vyeti basi wao wanakuja navyo na wanaomba wakiwa hapa hapa
Tatizo vijana wetu hawana sifa SMZ
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa maelezo juu ya vijana kutoka visiwani kukosa ajira katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa inatokana na kukosekana sifa za kujiunga na jeshi hilo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema jana kuwa vijana wengi kutoka visiwani wanashindwa kupata ajira katika jeshi hilo kwa kukosa sifa na viwango vyao vya elimu kuwa vidogo.
Mwadini alikuwa anajibu swali la nyongeza la Mahmoud Muhammed Mussa (Kikwajuni) juu ya vijana wa Zanzibar waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutoajiriwa na JWTZ.
Mussa alisema jeshi hilo mwaka jana liliajiri zaidi ya vijana 200, lakini kati ya hao hapakuwepo wa kutoka Zanzibar.
Akifafanua Waziri Mwadini alisema, ingawa vijana waliomaliza elimu ya sekondari wanapewa nafasi kubwa na JWTZ katika ajira ya jeshi hilo, vijana wengi kutoka Zanzibar wanakosa fursa hiyo kwa kukosa sifa, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vyeti.
“Vijana wetu wengi hawana vyeti, na kama wanavyo ni vya kufoji na pia wanafeli interview,…ajira jeshini siku hizi inazingatia suala la elimu,” alisema.
Mwadini alisema vijana kutoka Zanzibar wanapoitwa kwenda kufanya usaili jeshini wanashindwa kusema hata sentensi moja kwa Kiingereza.
Akijibu swali lingine la nyongeza la Makame Mshimba Mbarouk kwamba kutowaajiri vijana kutaongeza ujambazi, Mwadini alisema vijana wajengewe msingi wa kufanyakazi za kujiajiri.
Alisema chini ya sheria ya mwaka 2003, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatoa fursa kwa vijana kupata emafunzo kupitia Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) nia ikiwa ni kuwawezesha kujiajiri.
Alisema chini ya utaratibu huo mafunzo hayo yanatilia mkazo elimu ya taalima za nyanja mbali mbali, zikiwemo za kilimo, uvuvi na ufundi.
Hatutawachukulia hatua zozote
SERIKALI haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaorejea katika akili ya baada ya kutibiwa ugonjwa waliopata kwa kutumia madawa ya kulevya.
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Zanzibar , Omar Yusuf Mzee alisema jana kuwa ni kinyume cha sheria kumfikisha mahakamani aliyepona ugonjwa, hata kama aliupata kwa njia ya uhalifu.
“Si jambo jema kumwadhibu mgonjwa anapopata hujambo, baada ya kutibiwa kwa gharama za serikali,” alisema Mzee.
Alisema kugharamia matibabu ya wagonjwa mbali mbali, wakiwemo wanaosumbuliwa na maradhi ya akili ni miongoni mwa majukumu ya serikali kwa wananchi.
Waziri Mzee alikuwa anajibu swali la nyongeza la Fatma Mbarouk Said (Amani) aliyesema wapo wagonjwa wa akili wanaopata ugonjwa huo kwa kutumia madawa ya kulevya na kutaka kujua hatua zinazochukuliwa dhidi yao baada ya kutibiwa kwa gharama ya serikali na kurejea katika akili ya kawaida.
Akijibu swali la msingi la Jaku Hashim Ayub (Muyuni) juu ya kutotekelezwa kwa mradi wa afya ya akili licha ya serikali kutenga sh. milioni 95 mwaka jana na fedha hizo kutopelekwa wizara ya afya.
Mzee alisema baraza liliidhinisha jumla y ash. Milioni 107 lakini hazikutolewa kwa sababu hazikupatikana kwa sababu fedha hizo zilipaswa kutokana na ufadhi wa wahisani.
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi, wamependekeza iundwe tume ya kuchunguza kuwepo kwa mikataba yenye utata katika Manispaa ya Zanzibar .
Wajumbe hao walitoa pendekezo hilo jana wakati wanajadili ripoti ya kamati ya baraza hilo ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa, juu ya utekelezaji wa kazi za kawaida na za maendeleo.
Ripoti hiyo ilisomwa katika kikao cha baraza hilo kinacoendelea mjini hapa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanajuma Faki Mdachi.
Akijadili ripoti hiyo Makame Mshimba Mbarouk (Kitope) alisema, “kuna wimbi kubwa la mikataba ya ubabaishaji, kiasi kwamba manispaa inaweza kushtakiwa.”
Alisema April 23, mwaka 2006 Manispaa ya Zanzibar iliingia mkataba wenye thamani ya Sh. milioni 700 na Kampuni ya simu za mkononi Zantel, lakini imeshindwa kuuheshimu mkataba huo.
Chini ya mkataba huo, Zantel ilipewa nafasi ya kuweka mabango, yaani Billboards za kuuza biashara yake katika manispaa hiyo, lakini kila yanapowekwa mabango hayo yanashushwa badala yake yanaonekana ya kampuni nyingine, pia ya simu za mkononi.
Zantel ina mkataba uliofikiwa kisheria, lakini kila inapoweka mabango yake, viongozi wanaagiza yatolewe, alisema Mbarouk na kuongeza “iundwe tume hapa kuna mchezo mchafu.”
Mbarouk alisema kuwepo kwa ubabaishaji katika mkataba huo ni dalili ya rushwa miongoni mwa watendaji wa Manispaa ya Zanzibar na wengine serikalini.
Alisema anapendekeza iundwe tume kwa sababu kuonekana kwa mabango ya kuuza biashara ya kampuni nyingine tofauti Zantel ni dalili kwamba kampuni hiyo imeruhusiwa kuweka mabango hayo kinyemela.
Hoja ya Mbarouk juu ya kuundwa tume ya baraza pia ilungwa mkono na wajumbe watatu wa baraza hilo , Abdalla Juma Abdall (Chonga), Salmin Awadh Salmin (Magomeni) Hija Hassan Hija (Ziwani).
Hija kwa upande wake alisema taarifa kwamba wajumbe wa kamati walidharauliwa wakati wanachukunguza utendaji wa Manispaa ya Zanzibar .
Juu ya tatizo la umeme katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Awadh alisema ukosefu wa jenereta limezungumzwa kwa kurudia rudia lakini mpaka sasa halijapatiwa ufumbuzi.
Alisema unapokosekana umeme wa kawaida, shughuli za baraza zinasitishwa na kusababisha serikali kupata hasara kwa kuongeza muda wa vikao.
“Ni jambo la aibu jengo hili kukosa jenereta,” alisema na kwamba mbali na ukosefu wa jenereta, jengo hilo pia muundo wa jengo jipya la baraza na vifaa vinasababisha sauti kutosikika vizuri.
“Sauti hazisikiki vizuri ndani ya ukumbi wa baraza na kusababisha wazungumzaji kuomba kurudia rudia kila wanachozungumza,….tunatumia muda mwingi na nguvu kuwasikiliza wazungumzaji,” alisema Awadh.
Pamoja na maeneo mengine, ripoti iliyowakilishwa na kamati katika kikao cha baraza hilo juu ya utekelezaji wa kazi za kawaida na za maendeleo, zinazosimamiwa na ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa, imegusa Ofisi ya Rais, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Wakati huo huo, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, alisema jana kikao cha baraza hilo kitaendelea kama kawaida leo kufidia muda uliopotea kwa kuahirisha shughuli za baraza mara kwa mara umeme unapokosekana ukumbini



SASA HAWA WATU WA BARA WAO NDIO WANAJUWA KIENGEREZA? NA KAMA WZANZIBAR HAWANA VYETI WW SINI WAZIRI KWANINI USIFANYE MPANGO WAKAWA NA VTETI. JE UNAJUWA KAMA JESHI KUBWA ULIMWENGUNI NI WAMAREKANI JE WANAJESHI WAKE UNAWAJUWA NI AKINA NANI??KAMA HUWAJUWI MM LEO WEWE WAZIRI NITAKUAMBIYA NI WALATINO WANAOTOKA SOUTH AMERIKA. WANAKUJA KUWA MAJESHI WA WAMEREKANI ILI WAO NA FAMILIYA ZAO WAWE RAI WA MAREKANI.WENGINE NI VIJANA KUTOKA GHETTO WAMAREKANI WAUSI AMBAO HAWAKWENDA HATA SKULI. PIA WANAFUNZI WENGI WANAO FELI MASKULI NDIO WANAKUWA MAJESHI MAREKANI NA NDIO JESHI LINALOTISHIA ULIMWENGU MZIMA. SASA WAZIRI VIPI LEO UNASEMA WAZANZIBAR HAWAWEZI KUWA MAJESHI WALA POLISI KWA KUWA HAWANA VYETI NA HAWAJUWI KIENGEREZA??JE HAO WANAJESHI WA MAREKANI AMBAO NI TISHIO NA NATO KABLA HAWJAWA MAJESHI JE WALIAMBIWA WAJIFUNDISHE KIRUSI,KICHINA NA KISWAHILI NDIO WAWE WANAJESHI WA KULIHAMI TAIFA LAO. AU NCHI YAO??WACHENI KUWADANGANYA WAZANZIBAR NYINYI NI VIONGOZI NA MUME WAWEKA WABARA WAWALINDE NYINYI ILI MUDUMU MILELE MAANA MUNAJUWA KUWA KAMA VIJANA WA ZANZIBAR WANGELIKUWA MAJESHI NA POLISI NA NYINYI MUNAWATESA MAMA ZAO,BABA ZAO,DADA ZAO,KAKA ZAO NA FAMILIYA ZAO KIMAISHA NA KUWANYANYASA KWA KUWAFANYA MASIKINI WANGELI WAPINDUWA ZAMANI NDIO MAANA MUKAWAWEKA HAO WABARA ILI MUZIDI KUWA ANGAMIZA WAZANZIBAR  NA NYINYI MUNAKULA ULUWA WENU NA KUVIMBA MATUMBO MAKUBWA YA KULA HARAMU.