Monday, April 25, 2011

MUUNGANO HUU MWISHO CHUMBE


Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed akiongea katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa shule ya Haile Sellasie ndio aliyechana mswaada huo na kufuatiwa na watu wengine kuchana nyaraka hizo kwa madai kwamba hauna maslahi ya wazanzibari na kwamba suala hilo halijazingatia hadhi ya Zanzibar hivyo hauna faida kwa wananchi.
MKUTANO wa kutoa maoni kuhusu mswaada wa uundwaji wa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umevunjika hapa rasimu za mswaada huo kuchanwachanwa katika mkutano huo.
Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed akiongea katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa shule ya Haile Sellasie ndio aliyechana mswaada huo na kufuatiwa na watu wengine kuchana nyaraka hizo kwa madai kwamba hauna maslahi ya wazanzibari na kwamba suala hilo halijazingatia hadhi ya Zanzibar hivyo hauna faida kwa wananchi.
Mkutano huo ulipangwa kumalizika saa nane mchana lakini ilipofika saa saba Sheikh Farid alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo huku badhi ya wananchi wakiwataka wananchi wengine kundoka katika mkutano huo kwa kuwa hakuna faida a kujadili kitu ambacho haina faida kwao.
Awali akiochangia mjadala huo Sheikh Farid alisema alijaribu kufutalia mchakati mzima wa rasimu hiyo ya katiba lakini inaonesha kwamba kuna taratibu nyingi hazikufuatwa na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuujadili kwa kuwa hauna maana.
“Hapa tumesikia kelele nyingi sana kwa hivyo ilikuwa inatosha tutawanyike kabisa, tunakwenda katika kujadili marekebisho ya katiba ya Tanzania lakini swali jee katiba ya Tanganyika mnao? Jee hapa huo muungano uko wapi? Kipi cha kutangulizwa? Kwanza kafanyeni katiba ya Tanganyika kwanza” alisema huku akishangiriwa na wananchi.
Sheikh Farid alisema ngea katika akiwataka wananchi kutawanyika kujadili katiba kwa wadau mbali mbali umevunjika kufuatia sheikh Farid Hadi Ahmed kuchana rasimu ya katiba iliyowasilishwa kwa wadau mbali hapo katika ukumbi wa Shule ya Haile Sellasie ambapo awali mkutano huo ulipangwa kumalizika saa 8:00 kamili mchana lakini ulilazimika kukatishwa baada ya kuchanwa na watu wote kutawanyika katika ukumbi huo majira ya saa 7 mchana.
“Mswaada kwao sisi hatuna shida ya kutungiwa mswaada basi tunasema hatutaki kuvundwa vundwa….huu mswaada mnautaka ….mnasubiri nini chengine mkitaka muone kivitendo kwamba hatuutaki basi ndio hivi” alisema Sheikh Farid huku akichana chana mswaada huo.
Akichangia kwa ufupi mswaada huo Farid amesema lazima maamuzi ya wananchi yachukuliwe na suala la kuheshimu mawazo yao ni suala la lazima hivyo hakuna sababu ya kuwalazimisha kitu wasichokitaka.
“Natoa wasia wangu kwa serikali ya mapinduzi na serikali ya umoja wa kitaifa tunataka kura ya maoni tuulizwe muungano tunautaka au hatuutaki” alisema huku akipigiwa makofi kwamba muungano huo hatuutaki” alisema.
Akichangia katika mjadala huo baadhi ya wananachi walisema wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakidharauliwa sana hivyo hakuna sababu ya kuendelea kudharauliwa.
Walisema walisema zama za udikteta umekwisha na kama serikali inaogopa basi wananchi wapo tayari na hawataki kuingiliwa
Mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria ya bunge la jamhuri ya muungano Jadi Simai Jadi wa jimbo la Mkwajuni Zanzibar alitamka katika mkutano huo kwamba hakuwezi kuenelea tena na mkutano huo kutokana na hali ya usalama kutisha ndipo wananchi wakaanza kushuka nazi na kuondoka taratibu bila ya fujo lakini walikuwa wakiimba kwa nyimbo ya kuukataa muungano.
“’Wadau mliohudhuria mkutano huu wa kujadili rasimu ya katiba hapa ndio mwisho wa mkutano huu…hali ya usalama inatia mashaka”’alisema Jadi.
Kufuatia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria alitangaza kwamba hapo ndiyo mwisho wa kikao hicho.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi waliohudhria mkutano huo nao walichukuwa uamuzi wa kuchana mswada huo na hivyo hali ya usalama kuwa tete katika kipindi hicho.
Katika mjadala huo walikuwepo viongozi waandamizi akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Samuel Sitta pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais Muungano Samia Suluhu Hassan.
Akiongea katika mjadala huo Mzee Nassor Moyo ambaye alikuwa waziri wa sheria wakati muungano uliopoundwa alisema yeye amekuwa shahidi wa makubaliano hayo kati ya Zanzibar na Tanganyika.
“Nilikuwa waziri wa sheria wakati huo mambo haya ni 11 lakini hivi sasa yameongezeka naambiwa yamefikia mpaka 30 haya yote yaliongezwa na wenzetu bara ….na kwa yale yalioengezwa na watu wa unguja Jumbe alifukuzwa kazi sasa spirit ile ile ya Jumbe ipo maana sisi wengine tuhai hatujafa na pia wapo wanaunga mkono na yeye mwenyewe jumbe hajafa yuhai””alisema Mzee moyo huku akionesha nakala ya makubaliano hayo ya muungano.
Alisema mambo waliokuwa wameafikiana Nyerere na Mzee Karume wakati huo yameweza kuheshimiwa na viongozi wengine kulingana na wakati lakini kwa sasa vijana hawawezi kupangiwa mambo kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo sas vijana wanahitaji kurekebisha na kuwepo muundo wanaoutaka wao jambo ambalo alisema lazima serikali iwasikilize wananchi.
“Tusiwazuwie vijana hawa kufanya muungano wanaoutaka wao wenyewe, mimi na karume na jumbe tumeufikisha hapa …na haiwezekani kama tumeshaufikisha hapa halafu tuendelee hivi hivi bila ya wao vijana kuwaachia wenyewe wanavyotaka kuuendeleza lazima tukubali kuwapa fursa waseme wenyewe wanataka muungano wa iana gani …tusiwazuwia wenyewe …sisi yetu tumeshwikwisha” alisema Mzee Moyo.
Mzee moyo alisikitishwa na tabia ya kuambiwa kwamba suala la muungano zilijadiliwe jambo ambalo amesema iwapo halitazungumzwa kutakuwa hakuna jembo jengine la kulijadilia zaidi ya muungano kwa kuwa ndio kubwa kwa Zanzibar.
“Mnatwambia tusizungumze suala la muungano mnataka tuzungumze nini hapa wakati hilo ndio jambo la msingi….mnataka tuzungumze nini …hili ndio jambo tutakalolizuingumza” alisema huku akisisitiza kwamba kosa walilolifanya wakati huo hivi sasa lisirudiwe tena kwa kuwa vijana wa sasa wamesoma na sio wajinga kama wao ambapo haifai kupuuzwa vijana hao.
Akizungumza katika mjadala huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari alisema utaratibu uliotumiwa sio na serikali haikushirikishwa katika uandaaji wa rasimu hiyo na serikali ya muungano haifajafan ya uungwana hata kidogo.
Alisema licha ya kuwa hawajashirikishwa lakini serikali ya Zanzibar kupitia mwanasheria mkuu wake aliandika barua kupeleka serikali ya muungano lakini hakujibiwa angaua kwamba barua yao imepokelewa lakini pia walipeleka mapendekezo yao 14 lakini jambo la kusikitisha ni mambo mawili tu ndio yalioingizwa katika rasimu hiyo na badala yake kuongezwa mambo mengine manane kinyume na makubaliano.

No comments:

Post a Comment