Wednesday, April 27, 2011

NCHI ZILIZO VUNJA MUUNGANO BAADA YAKUJUWA HAUNA MASLAHI NA NCHI ZAO


Dhana ya muungano barani Afrika Nchi kadhaa duniani ziliwahi kuungana na hii leo imebakia kama ni historia, na hususan katika bara letu, zipo nchi kadha wa kadhaa zilizo ungwanishwa kutokana na nguvu za kikoloni na baadae ziliivunja miungano hio baada ya kukosa misingi madhubuti ya huo muungano mfano wanchi kama hizo ni north Rhodesia{Zambia} na south Rhodesia{Zimbabwe} leo nchi hizi ni nchi mbili zenye mamlaka yake kila mmoja nchi hizi ziliungwanishwa kwa nguvu ya mkoloni.pia kuna nchi zilizo ungana kwa hiari baada ya kujipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni katika mada yangu hii ya leo napenda zaidi kuzungumzia nchi hizi juu ya matatizo yao musakabali wao na ustawi wao. Ghana na Guinea ziliwahi kuungana mara tuu zilipo jipatia uhuru wao kwani mnamo tarehe 23 November 1958 zilianzisha muungano baina yao na kuwa ni chi za mwanzo zenye idadi kubwa ya waafrika weusi kuungana na mnamo mwaka wa 1961 Mali nao kwa hiari yao walijiunga na muungano huo, muungano ambao ulikuwa ni alama tuu ya muungano kuliko utendaji na ufanisi wa huo muungano ulio kusudiwa. Egypty na Syria nazo pia ziliungana pia haukudu muungano huo na ulivunjika muda sio mrefu, pia kuna muungano ulio dumu katika kipindi kifupi zaidi nao ni muungano wa Senegal na Gambia,lakini pia kuna muungano ulio kuwa uko kwenye hatau za awali kabisa kutiwa saini makubaliano hayo ya muungano na upande mmoja kugundua dhamira mbuvu ya upande mwingine na ikaamua kuuvunja haraka zaidi nao ni muungano wa Egypty na Libya, baada ya Libya kubaini mbinu chafu za Egypty dhidi ya mshiriki mwenza. Imaa katika tatizo la muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuna muuonekano tofauti kabisa juu ya miungano yote hio kwani ni wazi dhamira ilio kusudiwa hai kuwa ya kweli yenye misingi madhubuti ya kuleta umoja kama kinadharia unavyo onyesha ila kilichopo hapo ni mtawala na mtawaliwa. Kwani dhana hii ndio ilio kuwa na nguvu zaidi ambapo mataifa jirani kama Zambia ambayo mwanzoni ilihitaji kujiunga na muungano huu ilikuja kubaini ya kwamba hapakuwepo na uwazi wa muungano huo zaidi ya kujitumbukiza kwenye ukoloni mpya wa kutawaliwa na Tanganyika ilisitisha mara moja mpango huo na hata hivi leo hawana hamu tena na aina ya muungano uliopo baina ya Tanganyika na Zanzibar , pia ikumbukwe Julius K Nyerere alishidwa kuziunganisha au kulifanikisha wazo la mkolono la kulifanya shirikisho la East Afrika Kenya ,Uganda na Tanganyika hapa pana masuali mengi ya kujiuliza nikitu gani kilicho pelekea kushindikana kuazisha federation la Afrika mashariki ? kama lipo jambo kubwa la kumkumbuka Nyerere hii leo ni kule kuliasisi jina la Tanzania kutoka kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar mungano wenye utata mkubwa tokea siku yake ya awali mpaka hii leo kwenye uhai wake wote, kwani nasema hivi kuna vigezo vingi tuu Tanganyika na Zanzibar tunaambiwa ziliungana rasmi ingawa kumbukumbu hazionyeshi hivyokwa kujua zaidi angalia hati za muungano zilizo tiwa saini utaweza kubaini ukweli huu.kwa ufupi baada ya miezi sita ya muungano ulijulikana MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Pia ulikuja julikana au kubatizwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania mnamo October 29 1964 na kuliko pelekea makao makuu ya huo muungano kuwa Dar es salaam nchi Tanganyika. Na itoshe kuonyesha kwamba Nyerere alishindwa kuwa shawishi na kuwahamasisha viongozi wa Kenya na Uganda kuunda shirikisho la East African Federation mnano 1963. Sasa wakati umefika kwa Zanzibar kutanabahi ya kwamba shauku ya muungano huo haukuwa wenye muelekeo wa Pan-African ila ulikuwa ni mungano usio kidhi haja kabisa ya kuwa nao.
Kuna taarifa nyingi tuu juu ya njia ilio tumika juu ya muungano huu pia ikihusishwa madola makubwa ikiwemo uingereza na marekani kuwemo katika mpango huo,kwangu mimi hayo yote kama yalikuwepo ama haya kuwepo nina simamia dhana ile ile ya uhuru wa kila binaadamu kutowa mawazo yake juu yahayo na jengine lolote lile, kwa upande wa America wao wenyewe walio kuwa wanatumikia serikali ya wakati huo ya rais Lyndon B Johnson kwa wakati huo hawajapatapo kudai kuhusika na kuusuka huo muungano, kama alivyo wahi kunukuliwa Frank Carlucci wakati huo alikuwa ni US Consul in Zanzibar na baadae kuwa mkuu wa shirika la kijasusi la marekani la CIA na kufikia cheo cha waziri wa ulinzi wa America , aliwahi kueleza katika mahojiano maalum 1986 naomba nimnukuu hapaa
Frank C. Carlucci
November 23, 1987 – January 20, 1989
16th Secretary of Defence
Reagan Administration
http://www.smokershistory.com/Carlucci.htm
“Nyerere had to do something about the Zanzibar problem. I don’t know for a fact whether he came up with the idea himself, or whether we gave him the prescription. Whether our urging him to do something about Zanzibar had an effect on him….
I do know that the situation in Zanzibar was one of continuing deterioration. In the absence of action from Tanganyika, the place would have been completely controlled by the communists.”
Ikiwa kama kuna ukweli ndani yake inaonekana kweli Zanzibar tulikuwa tuna matatizo au bado tumo ndani ya mtatizo ambayo kila kukicha yanatupelekea tuwe dhaifu zaidi tulivyokuwa hapo awali mimi kwa mawazo yangu muungano uliopo ndio kiini kikubwa cha kuifanya Zanzibar kila uchwao tuwe hokhe hakhee.
Kwanini nchi za Africa zilizowahi kuungana zilivunja muunano?
Sina maana au niseme nimesoma mara kadhaa badhii ya nchi hizo kuwa zimeungana na sasa zinahitaji kupeeana talaka hili neno kwangu lina nikereketa kama alivyo wahi kusema mzee wangu kiongozi wangu Mhe Juma Duni Haji sipendi kulisikia wala kulisema neno hilo kwani kwangu ni zaidi ya tusii.kwani kimaumbile penye ndoa siku zote huwepo mwanamme na mwanamke, au muolewa na muolewaji.
Ni vyema tukaungalia muungano wa Egypty na Syria kwani muungano huo uliwahi kuanzisha jamuhuri ya kiarabu
KAMA ILIVYO TANGANYIKA NA ZANZIBAR KUANZISHA JAMUHURI YA TANZANIA Sina ufahamu wa kina kutokana na ufinyu wangu wataaluma juu ya mashariki ya kati moja ya sehemu kubwa yenye utamaduni ulio fanana au mmoja na kwanini zisiwe ni nchi mmoja, kwani utambulisho wa utaifa una umuhimu wowote ule ? Kwakweli kabisa niseme nisuali lenye kuhitaji ufafanuzi mpana na wa kina ila naweza kusema una umuhimu wa pekee katika ulimwengu huu . katika muungano wa Egypty na Syria nchi mbili hivi kila moja ilikuwa na malengo yake yalotofauti na mwingine ambayo kwayo ilikuwa sababu kubwa ya kuuvunja muungano wao, Egypty wakati huo rais wake alikuwa Abd Nasr yeye alikuwa na wazo la kubadilisha mfumo wa uchumi kutoka sekta inayo milikiwa na jamii na kuifanya ni sekta yote imilikiwe na serikali,wakati wananchi wa Syria walio wengi ni wafanya biashara hivyo hawa kulikubali wazo hilo kwani waliliona linadhamira ya kuwa angamiza wananchi wa Syria. Kusema jamii, mila. udugu mambo hayo kwa pamoja iwe ni kichocheo cha muungano kwa kweli ni kinyume kabisa na dhamira ya muungano wowote ule. Kwahiyo muungano wa watu silazima uwe watu wale wawe na tabia hulka na utamaduni ulio fanana, lakini la muhimu zaidi ni uchumi unao fanana au kulinganishwa,tamaa ya jambo Fulani miongoni mwao,nguvu, pamoja na udhibiti wa mambo Fulani na wala sio lugha wala dini.
Jambo lipi la muhimu zaidi juu ya mfumo wa muungano.
Mimi kwa mtazamo wangu uwiano wa maamuzi ndio njia, msingi au nguzo ya muungano.
Nidhahiri mahusiano hayo pamoja mahusiano ya kimataifa yanapo kusekana , huleta msegano na kusababisha msingi mkubwa wa malalamiko toka upande mmoja katika muungano huo, kunako pelekea kukosekana uwiano wa maamuzi, katika uchumi,siasa na ustawi wa jamii husika.
Kuvunjika kwa miungano
Kuvunjika kwa ulio kuwa muungano wa soviet ni wazi kulibadili mfumo wa uchumi na muenendo wa kisiasa duniani, ambapo kupelekea kutokuwepo tena mvutano ulio kuwa umeanzishwa na matokeo ya vita ya pili ya dunia kama ilivyo kuwa ikijulikana vita baridi vilivyopo baina madola mawili makubwa.
Kuvunjika kwa dola hizi kulidhaniwa kutadhiasiri baadhi ya nchi ndogo zilizo kuwa ndani ya soviet lakini ukweli hali imekuwa ni tofauti na matarajio hayo kwani nchi nyingi za ilio kuwa soviet leo hii zina ustawi mkubwa wa kimaendeleo ikiwa na wananchi wake pia.
Kuvunjika kwa muungano wa jamuhuri ya kiarab {Egypt na Syria alliance} muungano huu ulivunjika baada ya upande mmoja kujiona unadidimia kiustawi na kimaendeleo haraka walichukua hatua ya kuomba kurejeshewa kiti chao kwenye umoja wa mataifa ili iwe ni kinga madhubuti katika mkataba wa uanzishwaji wa umoja wa mataifa “UN charter” unavyo elekeza juu ya khaki ya kila taifa mwana chama wa umoja huo.
Kuvunjika muungano wa Senegal na Gambia sote tuna elewa Senegal ni taifa kubwa zaidi ukilinganisha na Gambia ingawa nchi mbili hizi zina maingiliano ya lugha, utamaduni na wananchi wake wengi ni wa moja ila kama nilivyo kwisha kueleza mambo hayo sio kigezo cha kuziunganisha nchi husika, na lau kuwa hichi ni kigezo mashariki ya kati yote ingekuwa moja na Gambia nayo ingekuwa moja na Senegal hii ni kuonesha kuwa mambo hayo sikigezo cha kuziunganisha nchi husika.
Nini tatizo hasa?
Mimi kwa muono wangu tuna matatizo mawili makubwa nayo ni kama ifuatavyo:-
• Sisi wenyewe wazanzibari ndio tatizo nambari moja
Na matatizo yetu yamegawika katika sehemu zifuatazo
1. Wanzanzibari tulio wengi ni wanafiki
2. Wanzanzibari bado hatujawa kitu kimoja
3. Wanzanzibar wengi ni wabinafsi
4. Wanzanzibar bado hatuamini kama tunaweza {HATUJIAMI}
5. Wanzanzibar ukarimu na umughali tulio nao pia nitatizo kwetu.
6. Wanzanzibar walio nunuliwa ambao wapo ndani ya jamii yetu {MamlukI}nalo pia ni tatizo.
7. MWISHO VIONGOZI WA ZANZIBAR NAO TATIZO
• Nguvu toka nje ya Zanzibar
1. Kuwaweka watu wao ili watimize lengo na dhamira yao
2. Kuwa gombanisha na kuwagonganisha vichwa wanzanzibari ili wapate kuendelea kuwatawala.
3. Kuibomoa silka na utamatuduni wa wanzanzibari
Kwa vyovyote iwavyo muungano uliopo upo kwa sababu wanzanzibar wenye bado tuna matatizo hayo niliyo yaeleza hapo juu, leo hii wanzanzibar tukiukataa muungano kwa kauli moja tena kwa vitendo hapatakuwepo na malalamiko ya muungano.
Nini kifanyike kuuvunja muungano hewa
Mapendekezo yangu binafsi sote tunapaswa tuwe kitu kimoja tuuache unafiki tuachane na itikadi ya vyama vyetu sote kwa pamoja tupiganie nchi yetu tusiwe tuna sema tuu hayo hayatatufikisha asilani Abadan, itikadi pekee inayo paswa tuitumie ni dini yetu iwe ndio dira yetu , kwa kama tunadai kushirikiana na Tanganyika na Zanzibar ndio tija hilo halipo kwani ALLAH SUBHANA AMESEMA NDANI YA QURAAN TUKUFU “Hakika ya washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao isipokuwa wale walioamini na kutenda mema na hao ni wachache”TMQ34:24
Suali tunadhani hapa Tanganyika atawacha kutudhulumu sisi wanzanzibari? asilani Mwenye Enzi Mungu ni mjuzi wa kila kitu na kama tuna taka kweli tusidhulumiane tuachane na huu ushirika na Tanganyika.
Sote kwa kauli moja tunapaswa tudai haki yetu ya kikatiba ya kuitishwa kura yamaoni juu ya muungano hivyo tunapaswa tuhamasishane tuwe na kauli moja mbiu moja hatuu taki muungano lakini halitoweza kufanikiwa hilo bila ya kuacha unafiki na kuwa sote letu moja.
Imefika wakati sasa tuwakatae wanafiki na mamluki tulio pandikiziwa miongoni mwetu iwe viongozi wetu au ndugu zetu kwani yeyote Yule ane ijali nafsi yake huyo sio ndugu yako bali ni adui yako wewe na jamii yako nzima kwani yuko tayari kuuza utu wake na wako kulinda maslahi yake sote tumuepuke huyo.tusi waamini tena viongozi wetu kwani wote wameshakula kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano, ni dhahiri unapo kukula kiapo hicho umeapa kuendelea kuididimiza na kuikandamiza Zanzibar katika Nyanja zote zile ziwe za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
Jee Zanzibar inaweza kuendelea bila ya muungano na Tanganyika?
Zanzibar ama nchi nyingine yoyote ile duniani inaweza kuendelea kama kutakuwepo na nguzo kuu nne
• Katiba ya nchi husika nayo ni shurti iwe na mambo manne nayo ni
1. Jamii ya wafanyaji wa sheria.{ Legislature}
2. Watendaji wa hizo sheria zilizo wekwa { executive}
3. Wasimamizi wa hizo sheria zilizo wekwa { Judiciary}
4. Jamii au watu wenyewe.
• Pawepo na mwenendo endelevu wa maendeleo itakayo gawanya na kuongoza mambo muhimu ya kitaifa na kimataifa katika kuweka, kufanya sera katika ujumla wake “national and international policy-making circle”
• Utengemano wa kisiasa na uchumi.
• Uongozi imara na thabiti.
Jee sisi wanzanzibari hatuwezi kuwa na vitu hivyo? Na jee kama tunavyo vinawajibika au kuwatumikia jamii au wazanzibari?
Ni wazi kabisa kilicho kuwepo ni ubabaishaji tuu, hivyo tunapaswa kwanza kwa umoja wetu tuyasimamie hayo na bila ya shaka yoyote ile Zanzibar inaweza kuendelea na jamii yetu sote tukayaona hayo maendeleo tuyatarajiayo katika nafsi zetu.
Naomba kuwakilisha

No comments:

Post a Comment