Friday, April 29, 2011

VIONGOZI WA ZANZIBAR WAJILIYA MILIONI 7OO KUMHAKIKISHIA MFAMLE KIKWETE SHEREHE ZA MUUNGANO ZINAKUWA ZANZIBAR NA WATU MICHEWENI WANAKUFA NA NJAA HUKO PEMBA

HUYU NDIYE MFALME KIKWETE  AKIWASILI KTK NCHI YA ZANZIBAR
ANAYOITAWALA

haya ndio mambo yanayotokeya huko nchini kwake
mfalme huyu ambaye anawatawala nchi ya zanziba

msikilize mfalme kikwete anavyosema
kisha mzanzibar jiulize kayafanya hayo aliyo
yasema nchini zanzibar ambako anaganganiya kuitawala
kwa njia ya MUUNGANO???

sikiliza hii nyimbo ndio utajuwa ni vipi na vipi
kikwete wewe ndio mkuu wa majeshi,rais wa
tanganyika,pia unaitawala zanzibar vyeo vingapi hivyo
je kofia moja haikutoshi ya tanganyika ukiva nyingi mwisho
utaziangusha.
WANGALIYE WANCHI WA NCHI YAKO TANGANYIKA KWENYE HII MUSIC VIDEO
KIKWETE

hii ni kwa wala WABUNGE  wote na WAWAKILISHI wote
wa
ZANZIBAR
munauza nchi na kila kilicho kuwemo ili nyinyi muwe na maisha mazuri na familiya zenu
na huku munajuwa kuwa wazanzibar wanakufa na njaa na nyinyi mumeufyataa kama
mkia wa mbwaa koko
ila kumbukeni iko siku hizo pumzi munazo ringiya mwenyewe atakuja kuzichukuwa
ALLAH
na hapo ndio utakapo juwa kati ya maziwa na tuwi kuwa sio sawa ni vitu tofauti
maana ukirudi kwa ALLAH hakuna tena UWAKILISHI wako wala
UBUNGE wako wala CHAMA CHAKO wala MAPESA YAKO uliyokuwa
UKIYAIBA KUTOKA SEREKALINI NA KUJINENEPESHA WEWE NA FAMILIYA YAKO
UTAINGIZWA KABURINI NA SANDA TU HIZO SAA NA SUTI NA VIATU VYOTE
UTAVIWACHAA HAPA HAPA DUNIANI NA UKIFIKA HUKO ALLAH ATAKULIZA WEWE
SI ULIKUWA KIONGOZI JE ULIWASHUGHULIKIYA RAI WAKO?

JE ULIHAKIKISHA WANA KULA NA KULALA PAZURI KAMA UNAVYO KULA WEWE
NA UNAVYO LALA WEWE?
JE ZILE MALI ULIZICHUMA VIPI NA NINANI ALIKUWA NA HAKI YA KUTUMIYA MALI ZILE?
NA MENGINE MENGI TU ALLAH ATAKULIZA WEWE KIONGOZI WA KISLAMU NA UNAWADIDIMIZA WAISLAMU WEZAKO KWELI HII NI HAKI MUTAKWENDA MUAMBIA
NINI ALLAH SIKU UKINGIZWA KABURINI??
NA SIKU YA KIYAAMA JE UTAMUELEZA NINI
ALLAH ???

VIONGOZI WAJILIYA MILIONI 700 TU KUFURAHISHA MFALME WA TANGANYIKA
Suti mzuri ni sanda ktk safari ya heri na kama nikatika wenye kula hasara wele wako.
Baada ya Tanganyika kuona ‘maneno maneno’ yamekuwa mengi kutoka Zanzibar, waliamua kuifanya sherehe kubwa ya miaka 47 hapa Zanzibar. Naam, Wazanzibari hususan CCM wameitikia wito huo kwa makini sana.
Tanganyika wameshatujua sana Wazanzibari kuwa ni wanafik, waongo, na hatuna msimamo wa jambo lolote, hata lile la dini yetu ya uislamu. Hilo liko wazi kabisa.
Wameamua kutoa pesa taslimu kama 700 milioni, au zaidi kugharimia shughuli hiyo. Ina maa kuwa, akina Balozi Seif Ali Iddi na ofisi yake na waratibu wengine wametia ndani chochote sihaba! (yumkin).
- Kuna habari nimepenyezewa zaidi ni kuwa sherehe hizi zimegharimu shilingi 1.2bn/= zikiwemo gharama za kubeba gari za mfalme Kikwete kuletwa hapa Zanzibar (Kikwete haezi kupanda land rover au angalau Prado kama wanavyopanda wengine). Jumla hasa ya gharama za sherehe hizi ni hizo hapo juu. Pesa ambazo zingaliweza kujenga skuli moja kule kwao JK Chalinze au popote pale katika eneo lake, ambalo wanaishi maisha dhalil kabisa.
Baada ya SMZ kupokea cheque yenye donge nono kama hilo, wamekaa kimya. na wamebaki kuusifu na kuuenzi Muungano. Sisi sote thamani yetu ni hiyo 1.2bn/=. Tumeona bora pesa kuliko utu.
Akina Bi.Samia nao wametetea sana msimamo wao kupitia TVZ kuwa “muungano hauna doa, na ni halali”.
- Akina Mahadhi Juma Maalim ameonyeshwa amekamata kibendera chake anakipepea kw araha kabisa, yaani ndio amefika huku kule kwao Muungano, na jimboni kwake, hata gari haifiki siku kama hizi za mvua kubwa. Anashindwa hata kupeleka kifusi, na kutabaruk kwao. Amepewa kura, basi…sasa anakula nchi.
Kwa dharu ya mwisho ya sherehe kwa Wazanzibari, JK ameamua hata asitoe hotuba angalau ya kutwambia ‘nyie Wazanzibari mkivunja Muungano mtakiona cha mtema kuni”….tuavunja maghorofa yenu yote pale Kariaakoo. CCM wameishuika nyimbo hii siku hizi wakiongozwa na Seif Ali Iddi — eti Wapemba wamejaa kariakoo, wamejenga maghorofa….hii sio siasa ila husda tu.
Sisi wengine tulisema mwanzo kuwa Balozi Seif Ali Iddi, hatufai (huyu ni Mgogo kutoka Dodoma), Shein ni kutoka Kimbiji (Rufiji) — wote hawa wakuja tu hapa. Watatuzamisha itakavyokuwa.
Ninavyoona mimi, dawa ya muungano ni mbili:
1. CCM warejeshe kadi zote Dodoma (kitu ambacho hawawezi mpaka mwisho wa dunia kukifanya).
2. Baraza la Wawakilishi wafanye mswada wa kuukana Muungano kisheria ndani ya baraza la wawakilishi (kitu ambacho kwa unafiki wa wawakilishi wetu, na hususan hypocrisy ya Abubabkar Khamis Bakari, Waziri wa Sheria — hawawezi kukifanya hata kama wataambiwa hawafi tena). Zanzibar inakufa, na tunaiiuwa wenyewe.
Muungano unatudhulumu sana sana Wazanzibari, hasa kiuchumi. seuze siasa ambayo tumepoteza utaifa wetu wote. Tumenyonyolewa mbawa zote, hatuwezi tena kuruka.
HAWA NDIO TAIFA LA KESHO ZANZIBAR WANGALIYENI WAZANZIBAR AMKENI.
Mfalme Kikwete, mwisho wa jeuri yake, amekwenda na vikundi vya ngoma kutoka kwao, Bagamoyo na Dodoma, pale Ikulu Zanzibar – na kwenda kuwapongenza, na kutimka tena huko – yaani ile ya amani stadium haikutosha. Dharau ya mwisho mwisho kabisa, jeuri hasa. Lakini tutafanya nini na tumewezwa? Tusisahau kuwa tunayo maradhi ya kupenda watu kutoka Tanganyika kuanzia wapishi wetu hadi watia rangi, na watia mifereji. Then, wanatutapeli. tunalia…mwisho eti tunamuachia Mungu (sijawahi kusikia tauhidi ya namna hii).

No comments:

Post a Comment