Kundi hilo linaloongozwa na Rashid Salum Addiy, lilianzaa harakati za kudai mkataba wa muungano wenye saini mbili za Nyerere na Karume mwaka 2005 katika mahkama kuu ya zanzibar na mwanasheria mkuu wa Zanzibar bila mafanikio.
Dai katika Mahakama kuu lilitupwa kwa kile Mahakama ilipoona kuwa walalamikaji kushindwa kujenga hoja yao katika misingi ya kisheria. Mwanasheria mkuu naye alijibu kuwa ofisi yake haikuwa na nakala ya makubaliano.
Akizungumza na gazeti hili, Rashid alisema kuwa kundi lake limekusudia kuendelea na madai yao ambapo mwishoni wa mwaka jana walipeleka notisi katika Mahakama ya Kimataifa (ICJ) kutaka kushitaki Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuridhia kwa kuanzishwa Muungano uliopo kinyume na misingi ya kisheria na kuendelea kuwepo Muungano ambao si halali katika mahakama ya uhalifu ya umoja wa mataifa Hague.
Rashid alisema tayari ameshaasilisha hati ya kuishitaki serikali, kupitia wakili kampuni ya J.C.CHIDZIPHA&CO.ADVOCATES yenye ofizi zake huko Mombasa Kenya iliyowasilishwa octoba 19 mwaka jana imesema pamoja na mambo mengine ….
Lengo la kuishitaki serikali ni kupata hati ya Muungano ambapo kundi hilo limesema tayari limeshajibiwa barua yao hiyo na Mahakama hiyo ya Kimataifa na sasa wanaendelea kukusanya vielelezo vinavyohitajika na mahakama hiyo ikiwemo kukusanya saini ya wananchi wasiopungua mia mbili wa Unguja na Pemba jambo ambalo amesema ana hakika kufanikiwa.
Awali kundi hilo la watu kumi liliwasilisha barua kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar mwaka 2005 kutaka kupatiwa nakala ya hati ya mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika Zanzibar lakini barua yao haikujibiwa hadi pale kundi hilo lilipowasilisha madai katika mahakama kuu ya Zanzibar kudai hati hiyo ya siri na kuanza kusikiliza 20 Mei 2005.
“Tulipowasilisha barua yetu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar atupatie hati ya siri ya mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walikaa kimpya hawakutujibu mpaka sisi tulipoamua kuwapeleka mahakamani ndipo wakatujibu kwamba serikali haina hati hiyo” alisema Addy.
“Ofisi yangu haikuweka kumbukumbu ya nakala ya hati ya mkataba wa asili (original) wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo tarehe 26 Aprili, 1964.” Alinukuliwa barua ya Juni 22, 2005 iliyowekwa saini na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati huo, Iddi Pandu Hassan.
Nakala ya majibu ya barua hizo alipelekewa Spika wa Baraza la Wawakilishi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambao nao walijumuishwa katika kesi hiyo kesi ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Wakili Lamwai kwa upande wa chama cha mapinduzi ambapo aliwaita kuwa ni wahaini na wanataka kuipindua serikali kupitia madai ya kudai hati ya Muungano na kuwepo na mapungufu mengi katika ufunguaji wa kesi hiyo.