Monday, May 9, 2011

JE WAZENJI TUTAKUBALI DUNGU ZETU WAISHIYE JELAA..?

Katika tukio hili la majuzi la mabanda kuchomwa moto.Kutakuwa na wazanzibari wachache watashikiliwa na polisi na kupandishwa mahakamani.
Ushauri wangu kwa wazanzibar wote nasi tusiwaache mkono tuchangishane kihali na mali kuwapatia msaada wa kisheria.Ninachokusudia hapa tumlipe mwanasheria mmoja asimamie kesi hio mwanzo hadi mwisho.
Nasema hivi nikitarajia suala hili liwe na uzito wake.Maana kuna mambo mengi ambayo nayatizama nahisi yanahitaji majibu.Kuanzia uhalali wa hao watanganyika kupata ardhi huko Shamba, hadi ushahidi gani waliokuwa nao Jeshi la Polisi kuwafungulia kesi.Mbinu gani zimetumika hadi kumshtaki mtu na kesi hii.Tukumbuke wao wanaungwa mkono na jeshi la polisi (tanganyika).
Hatusemi kama tunaunga mkono kitendo walichokifanya, lakini tunafahamu kilio chao au kwa maneno mengine ya kiengereza “we do understand their frustration!”.kwa hiyo wazanzibar wote ulimwenguni tushikamane kwa guvu zote na kwa hali na mali tuhakikishe tunaikombowa zanzibar yetu na tuhakikishe dungu zetu hawaishi jela.

No comments:

Post a Comment