Friday, May 6, 2011

NCCR-MAGEUZI,TADEA,CCWC-AFP.VYATETEA HAKI ZA WANYONGE NA KUMTAKA SHEIN KULIVUNJA BARAZA LA WAWAKILISHI KWA MADAI KWAMBA((SUK))GNU IMESHINDWA KUFUATA MISINGI YA UTAWALA WA SHERIA WANAUZA TU KILA KITU CHA SEREKALI NA CUF IMEBANA KIMYA JE MUSHAKATIWA NA NYINYI CHENU....?

                                                              
JE ULIWA AHIDI UTAUZA MAJUMBA....?
ELIMU YA ZANZIBAR KAIYUWAA  HUYU AJIUZULU

HAWA NDIO WENZAKO MUNAOGAWANA SIO..?

SEIF VIPI USHATUWACHA MKONO NINI....?


HILI NDIO JUMBA LENU MUNALOKUTANA NA KUFANYA UKIRITIBWA
HAMUNA MOJA LA MAANA MUNALOLIFANYA LA MAANA JUMBA ZURI
KUBWA WANACHI MKATA WA ASUBUHI KUNYWIYA CHAI HAWANA
KISHA NYINYI MUNAKUTANA HAPA MUKIGAWANA WEWE KAUZE
JUMBA MIMI NAUZA VISIWA VIDONGO VIDONGO YULE AU VIWANJA
KUNA NA KIYAMA PIA MITHAMBI MUNAYOBEBA MUTAKWENDA KUMU
ZIA NANI SIKU YA KIYAMAAAA........? WALIKUWAPO VIONGOZI KAMA
NYINYI SASA WAKO WAPI MBELE YA HAKI ALLAH ANAWAPA TUUU


Vyama vitatu vya upinzani Zanzibar, vimemshauri Rais Dk. Ali Mohammed Shein,
  kulivunja Baraza la Wawakilishi kwa madai kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) imeshindwa kufuata misingi ya utawala wa sheria.
Viongozi wa vyama hivyo wametoa ushauri huo baada ya Rais Dk. Shein, kutetea kuwa serikali haikufanya makosa kuuza majengo yaliyomo katika Hifadhi ya Mji Mkongwe bila kuitangaza zabuni kwa vile majengo hayo ni mali ya serikali.
Vyama vya upinzani vilivyotoa kauli hiyo ni NCCR-Mageuzi, Tadea na Chama cha Wakulima cha AFP.
Viongozi wa vyama hivyo walitoa kauli hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mjini hapa jana.
Katibu Mkuu wa Tadea, Juma Ali Khatib, alisema hakuna sababu ya kuwa na baraza la kutunga sheria wakati serikali imeshindwa kufuata misingi ya utawala wa sheria ikiwemo kuuza mali zake bila ya kutangaza zabuni wakati mali hiyo ni ya umma.
Alisema majengo ya Mambo Msiige, yamekodishwa kwa miaka 99 kwa thamani ya dola milioni 1.5 bila ya kutangazwa zabuni kitendo ambacho ni kinyume na Sheria Namba 9 ya mwaka 2005 ya Manunuzi ya Mali za Serikali. Alisema kauli iliyotolewa na Rais Dk. Shein, imelenga kuwalinda viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa majengo hayo ya serikali.
“Rais amekula kiapo atalinda Katiba na Sheria na mawaziri wake, haikuwa mwafaka kusema serikali ina haki ya kuuza mali bila ya kutangaza zabuni wakati ni uvunjaji wa sheria,” alisema.
Juma alisema tayari wameshamwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi ya kutoa notisi ya kuishtaki serikali tangu Aprili 13, mwaka huu, lakini hadi sasa hawajajibiwa.
Hata hivyo, alisema wanatarajia kufanya maandamano makubwa Mei 17, mwaka huu, kupinga kitendo cha serikali kutetea uamuzi wake wa kukodisha majengo hayo kinyume na sheria.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP), Soud Said Soud, alisema hakuna sababu ya kuwa na baraza la wawakilishi wakati Serikali imeshindwa kuheshimu sheria zinazopitishwa na chombo hicho.
“Tunamshauri Rais avunje Baraza la Wawakilishi badala ya kuendelea kupoteza fedha wakati serikali imeshindwa kuheshimu sheria zinazotungwa na baraza hilo,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukakamlisha ziara yake ya Uturuki mjini Zanzibar juzi, Rais Dk. Shein alisema serikali haikufanya makosa kuuza majengo yaliyomo katika hifadhi ya Mji Mkongwe na hakukuwa na ulazima wa kutangaza zabuni kwa vile majengo hayo ni mali yake (serikali).
“Serikali haifanyi makosa, serikali ina maamuzi yake hasa kwa mali zake. Hakuna anayeweza kuihoji ikiimaua kuliuza jengo itauza . Wengine wanasema hatujatangaza tenda, kwani lazima kutangaza tenda, mbona hayo mengine tuliyoyauza hatukutangaza tenda,” alihoji Rais Dk. Shein.
Mradi huo wa Hoteli ya Kitalii ya Nyota tano umeibuwa mjadala mkali kutoka kwa wanasheria na wanasiasa wakipinga utaratibu uliotumika wa ukodishwaji wa majengo hayo yanayofanyika kinyume na sheria.

No comments:

Post a Comment