Sunday, May 29, 2011

WANGONJWA WAFAA MNAZIMOJA HOSPITAL KWA KUWA HAKUNA((ICU))VIONGOZI WA SMZ.GNU AU SUKARI WAJINUNULIYA MAGARI YA KIFAHARI KWANZA.


HII NDIO MASHINE YA ICU AMBAYO IMEHARIBIKA KWA MWAKA MZIMA SASA KTK
HOSPITAL YA MNAZIMOJA NA HAIJANUNULIWA MPYA NA WAZIRI WA AFYA HAONEKANIKI NA WAGOJWA MAHATUTI WAKILETWA HOSPITALI WANAKUFA MAANA HAKUNA HII MASHINE YA KUWASAIDIYA HONGERA SHEIN HONGERA SEIF KWA SUKARI MUNAYO WALISHA WANANCHI.

ONENI HOSPITALI ZA WENZENU WANAVYOJALI RAI WAO NYINYI MUNAJINUNULIYA MAGARI KWANZA.

ONENI USAFI NA NITHAMU SIO ZNZ HATA WAZIRI WA AFYA HAJULIKANI ALIPO.

KITANDA HICHO ILI MGONJWA APATE NAFUU ARUNDI NYUMBANI SIO KULALA KWENYE FLOOR KAMA MNAZIMOJA

HII NI KWA WATOTO WACHANGA.

CHUMBA CHA MGONJWA MOJA SIO KUMI NA KUAMBUKIZANA
MARATHI.

SHEIN NA SEIF ONENI WACHENI KUWATESA WAZENJI AU
NYINYI NDIO MADIKTETA WA MWISHO MUMEKUJA KUWA
MALIZA WAZENJI PESA ZA MAGARI ZEPO ZA KUFANYA HOSPITAL
HAKUNA MAMBO HAYA VIPI AU NDIO SUKARI..?GNU

MGONJWA MAHATUTI NCHI ZA WENZETU ONENI WANAVYO WAJALI
RAI WAO SIO NYINYI KAZI KUIMBA TU.




-Mashine zote za ICU ni mbovu
-Hazijawahi kufanyiwa matengenezo
-Viyoyozi pia vimekufa, hewa ni madirishani
-Matengenezo kusubiri bajeti ya serikali
Mashine tano za huduma kwa wagonjwa mahututi, ziitwazo Monitor Machine zimeharibika katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazimoja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, imebainika.
Kwa kawaida mashine hizo aina ya HP/Hewlett Packard, huwasaidia madaktari kujua mwenendo ya mgonjwa aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Uchunguzi wa MSAMARIA MWEMA MWENYE KUJALI WAZANZIBAR, Amebaini kwamba mashine hizo zilianza kuharibika moja baada ya nyingine kuanzia mwaka jana na hadi Januari mwaka huu zote ziliharibika.
Uchunguzi huo unaonyesha kuwa mashine hizo ziliwekwa miaka 10 iliyopita, lakini zimekuwa hazifanyiwi matengenezo kutokana na ukosefu wa mafundi wa kuzikagua na kuzitengeneza kwa kuzingatia teknolojia yake.
Kuharibika kwa mashine hizo kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichoomba kuhifadhiwa jina, tayari umesababisha watu kupoteza maisha kwa kukosa uangalizi wa afya yao unaohitaji matumizi ya mashine hizo.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa viyoyozi aina ya Sanyo vilivyopo chumba cha ICU vimeharibika na kusababisha madirisha ya chumba hicho kuachwa wazi kuruhusu hewa kupita.
Chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali hiyo kina uwezo wa kupokea wagonjwa sita.
Katibu Msaidizi wa hospitali hiyo, Omar Juma, alithibitisha chumba hicho kukabiliwa na hali mbaya kwa kukosa vifaa hivyo. “ICU na yenyewe ipo ICU inahitaji matengenezo makubwa au kununuliwa vifaa vipya.”
Omar alisema uongozi wa hospitali hiyo tayari umepeleka makadirio ya bajeti ya karibu Sh. milioni 80 kugharamia utengenezaji wa vifaa hivyoila mpaka sasa hizo pesa hazijafika na matengenezo yake hayajafanywa na wagonjwa mahatuti huletwa mara kwa mara na hakuna vyombo hivyo matokeo yake watu hufa na wengine kuteseka kwa siku nyingi bila ya kutibiwa maana hakuna vyombo hivyo.
Alisema matengenezo ya vifaa hivyo ni muhimu ili kuiwezesha hospitali kurejesha haraka huduma kwa wagonjwa.
Mmoja wa madakari bingwa katika hospitari hiyo, alisema mashine hizo huwawezesha madaktari kufahamu kiwango cha hewa safi (oxygen) katika mapafu ya mgonjwa mahtuti.
Alisema kuharibika kwa mashine hizo kumesababisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa kutofanyika kwa usahihi unaohitajika kitaaluma.
Daktari huyo ambaye pia aliomba jina lake kuhifadhiwa, alisema wagonjwa wenye matatizo ya kupumua husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mitungi ya oxygen kwa kuunganisha mpira ili kumwongezea mgonjwa uwezo wa kupumua.
Alisema mashine hizo zilizoharibika pia hutumika kupima kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu ya mgonjwa.
Alipohojiwa juu ya tatizo hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya, alisema lipo na tayari hatua za kutafuta ufumbuzi zimeanza kuchukuliwa.
Alisema hatua hizo ni pamoja na kupeleka bajeti serikalini ili kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa ICU mpya katika hospitali hiyo.
“Wakati tukiwa katika mpango wa kutengeneza mashine zilizoharibika pia tuna mpango wa kujenga kitengo kipya cha wagonjwa mahtuti na tunatarajia kupata fedha za mradi huo mwaka huu,” alisema.
Hospitali hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vifaa hivyo muhimu katika huduma za afya, huku kukiwa na malalamiko juu ya serikali kuwanunulia magari ya kifahari watendaji wake wakuu wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Juhudi za kumpata Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, hazikuweza kufanikiwa.

atapatikana vipi na yeye pesa ashazinunuliya gari jipya na anatanuwa sasa kweli ataonekana huyo maluuni mkubwa.na wewe sira ubwa mamboya unasema zimeanza kuchukuliwa na hakuna moja munalolifanya ndio kazi yenu kusema tu kama kasuku mambo ya hospitali ni muhimu sana hayana haja ya kungojeya bajeti ila nikuwa nyinyi mawaziri na wabunge na wake zenu na watoto wenu mukiumwa hamupelekwi ndio maana munangojeya mpaka bajeti sisi masikini tunapelekwa mnazimoja na kufaa maana hakuna hizo mashine sio. na ikiwa hamuwezi kuzifanyia marekebisho hizo kweli muta weza kununuwa mpya au kujenga ICU mpya munapaka mavi nani hapa shein wewe si ni doctor shein mbona hujuwi kama mnazimoja hakuna ICU na ukuta wako wa ikulu umeshikana na ukuta wa mnazimoja na hata hujali sio kama ni kiongozi bora jivalishe hata mararu kisha uingiye hapo mnazimoja usiku uikanguwe uwone rai wako wanavyo teseka ila huna upendo huo wewe kwa rai wako ndio maana umebana tu ikulu unakula kuku wako basi wazenji wache wafee sawa hata hujali m/mungu atakwenda wachoma nyinyi kweli kweli siku ya kiyama maana munajita viongozi wala hata hamujuwi uwongozi ni nini.

1 comment:

  1. @Editor
    Well done man. You are doing good work for Zanzibar & Zanzibaris.
    Keep it up and God Bless you.

    ReplyDelete