Thursday, June 2, 2011

HII NDIO PEMBA JIONE MWENYEWE KWA MACHO YAKO BATHI YA PICHA NILIZO WEKA


hichi ndicho kisiwa cha pemba chenye marashi ya karafuuuuuuuu

nimeona bora niweka picha hii kuwazinduwa zaidi dungu zangu wote kuwa
hata kama wanasema pemba ni mbaya ndio kwetu na mkata kwao mtumwa
hata uwishi wapi miaka mingapi wenye nchi unayo ishi watakwita mkimbizi,wakuja,
umetuvamiya n.k. lakini pemba ni kwetu nani atatuita majina ya ajabu..? nyumbani tumekupa mgongo jamaa.

hii ndio karume airport ndio kiwanja cha denge kikuu cha pemba.

abiria wakisubiri kuruhusiwa kupanda denge na kuanza safari yao pemba airport.

                                               airport ya pemba

moja ya hoteli za kitali zilizo funguliwa huko pemba.

hi ni picha ya usiku au juwa linapozama huko pemba hoteli ya kitali

haya ndio majongoo ya pemba makubwa sio mchezo
.


hawa ndio popo mchana wanalala na usiku wanaruka pia miujiza ona wanavyo lala kichwa chini miguu juu

hawa ndio denge wa majabu waliyokuweko huko pemba kisiwani.

bila ya kusahau kunguru wa zanzibar hahaha jamaa musisahau kwenu.

denge wa kila aina wako pemba na wazuri kabisa

hawa ni moja ya denge waliyoja kisiwani pemba na nisisi ndio wakuwatunza ili wadumu.

moja ya ufukwe wa bahari huko pemba.

ona utajiri tuliyo nao pemba.

moja ya wageni waliyo kuja kutembeleya kisiwa cha pemba.

hii ndio airport ya pemba jamaa muliyo kuwa nje fanyeni mpango tujengewe ya kisasa watu kibao watapata
kazi za kufanya na kisiwa chetu kitaweza kupokeya denge kubwa kubwa hapa zinatuwa au sio jamaa.

wakina mama wakivuwa mwaani wao huko pemba

moja ktk fukwe za bahari huko pemba ona mchanga ulivyokuwa mweupeeeeeeee.

hii ni moja ktk hoteli zilizojengwa huko kisiwani pemba.

hii ndio pemba crown hotel ya pemba

jamaa pemba pia munaweza kujenga hayo majumba mazuri munayojenga nchi za watu hapa
ni kwenu haswa jamaa njooni mjenge ili pemba inuke musijenge kwa maduwi zetu nakuwanufaisha wao

hii ndio bara bara ya pemba

ona ufukwe ulivyo tulia jamaa dungu zetu muliyokuwa nchi za nje kama muna pesa mujemujenga
musiwachiye wangeni wajenge na kufaidika na nchi yetu kila moja anajenga kwao

oneni wangeni wanavamiya fukwe na kujenga na kuchuma pesa na sisi tuna
dungu zetu wangapi muko huko nje na mapesa bank yamelala njoni mjenge kwenu
nchi inuke jamaa

mambo yaliyokuwemo ndani ya bahari ya pemba
.
wazungu wameganda pemba

kama hujapata kuona njoo pemba utaona mwenyewe wala hakumizi.

karibu ktk bahari ya pemba ujione mambo

moja ya thamani ya bahari yetu ya pemba ni hii

wakijaribu kuweka tangi la maji.

hizi ndio karafuuu pemba sishakuwatayari kuchumwaa

ona kisiwa kilivyo katwakatwa na maji unaweza kujenga hapa jisupa maketi la nguvu na vioo
ili watu waendele kuona maji yanavyo pishana bila ya kuharibu mathari na ikawa babkubwa

moja ya fukwe za pemba bado kabisa hazijaguswa

oneni jamaa nchi yetu ni nzuri ila tu inataka vijipesa kidogo kujega hapa na pale na kila moja
ataililikuka na kuishi hapa jamaa amkeni

mambo yaliyomo ndani ya bahari ya pemba

haya ndio mambo yaliyokuwepo chini ya bahari unaona wazungu hawaganduki

mambo ya pemba hayo

moja ya vijiji huko pemba.

tusisahau tuliko toka mtu kwao.

hii ndio ofisi ya prime-minister huko pemba

ona mambo ya pemba hayo bahari inavyovutia

jamaa karafu pemba zishakuwa tayari kuchumwa karafu pemba zishakuwatayari kuchumwa.

moja ktk huteli za kitali

moja ktk hoteli za kitali

moja ya visiwa vidogovidogo vilivyo nje ya pemba.

moja ya visiwa vidogovidogo vilivyo nje ya pemba

ona ufukwe unavyo tualika jamaa

oneni fukwe hizo ni zetu wote jamaa

pemba jioni wakati wa kuzama jua angalia m/mungu alivyo ipamba pemba ila sisi hatuoni

kuzama kwa juwa wakati wa jioni pemba

jione na ukumbuke pemba ndio nyumbani na sio kama ni kubaya ila ni sisi tushikana na kuijenga pemba yetu

kuzamaa kwa juwa ndio kama hivi mzee

moja ktk skuli za sekondari huko pemba.

moja ya hoteli za kitali pemba

moja ya visiwa vidogovidogo hapa pemba vilivyo geuzwa kuwa hoteli za kitali

moja ya wazungu waliyo ipenda pemba mpaka kufa sisi wenye pemba tunaichukiya
aibu ngani jamaa..?

kumbukumbu za pemba zinawachwa zikianguka hakuwa wakuzitunza

vijana wakijuvulia samaki wao fresh kabisa kutoka baharini

moja ktk hoteli za kitali pemba sisi wenye kisiwa hatujuwi uzuri wake wengine wanasafiri masafa kujakufaidi na hii ni hoteli ya mtu binafsi na ona ilivyo nzuri huishi kuitazama.

na hii hapa ndio hoteli ya watali inayo milikiwa na serekali yetu ya zanzibar aibu ngani hii jamaa hoteli ya serekali imeka kama shimo la kuchimbiya makaa ya mawe wanashindwa na watu binafsi ibuu iliyoje.

moja ya fukwe za bahari hapa pemba

moja ya chumba cha hoteli hapa pemba

ona fukwe zilivyo jaa hapa pemba na bado hazija haribiwa jamaa njoni tuzishike ili wageni wasizivamiye

moja ktk hoteli za kitali pemba

mkoani pemba hapa

hii ndio lighthouse hapa pemba

jioni hapa pemba

haya ndio mambo ya mahanjumati hapa pemba

watali wakitia roundi na viboti hapa pemba

moja ktk hoteli za kienyeji hapa pemba

majumba ya kumbukumbu ya pemba yananguka tu hakuna wakuyatunza

bandari ya mkoani pemba

bandari ya mkoani pemba

mkoani pemba ktk pirikapirika za hapa na pale

mkoani pemba

jioni watu wakijishibuwa kwa mpira mkoani pemba

hii ndio soko la samaki hapa mkoani pemba

bandari ya mkoani pemba

abairiya wakisubiri meli ifunge gati ktk bandari ya mkoani pemba

hii ndio bandari kuu ya mkoani pemba
 
ona hapa wananunuwa vitu majishi waliyojazwa pemba hao kutoka bara

hawa ndio majeshi waliyo jazwa hapa pemba ati na wao wako marikiti wananunuwa umeona wapi ktk ulimwengu huu tuliyo nao majeshi kwenda katika soko la rai kununu vitu hata kama wanakwenda ni wawili na gari lao sio hawa malori yote yanamwangwa sokoni wanazurura tuu jamaa wazenji amkeni.

hawa ndio watoto wetu watarithi nini na majeshi hawa waliyojazwa hapa pemba

kina mama na kina dada wakisoma maulidi ya mtume s.a.w. hapa pemba

hawa ndio dada zetu hapa pemba

bado tunaendeleza utamaduni wa kuchonga ngarawa kwa vifaa vya mkono wete pemba

jimeli likioza taratibu hapa pemba

markiti ya wete pemba

wadau wa wete wakivichapa vilivyo pikwa na kina mama na dada zetu

hapa ndio wete mjini

usafiri bado ni shinda hapa pemba dungu zetu leteni magari ya kisasa nyinyi mutanufaika ni sisi pia tutakuwa na uhakika wa kusafiri bila ya shinda jamaa amkeni

hii ndio cinema ya wete pemba jamaa njoni mujenge ya kisasa jamaa.

wete pemba ndio hapa home sweet home jamaa

markiti ya zamani wete

ukisikia wazee wetu walivyokuwa wakisema kazi ni kazi hata kuzaa nazi ni kazi ndio kama hivi anajitafutiya riziki yake na wanawe na mke basi anajishukuriya mungu siku imepita.

hapa ndio chake chake pemba watu wakingia msikitini

hawa ndio dada zetu hapa chake chake pemba wakiwa ktk harusi

ikitaka nazi njoo chake chake ktk soko la nazi utanunuwa mpaka utaziwacha hapa hapa.

hapa ndio chake chake pemba kama kawa hakuna noma

ukija chake utapata embe na kila utakapokwenda pemba hii kuna embe

chake chake pemba hapa

hizi ndio korosho zipo kibao hapa pemba

chake chake pemba

kama unavyoiona ndio karume airport jamaa kweli boeing air,emirates air,gulf air,klm air,air france,british air,lufthansa air kweli zitatuwa hapa kwenye hichi kijiairport jamaa tujengeni kubwa ili zote zituwe hapa vijana wapemba sote tutapata kazi ya kufanya hakuna atakae kuwa hana kazi.

kiwanja cha watoto kufurahi kimekufa jamaa si aibu hii

hapa ndio chake chake pemba ktk pirika za hapa na pale mjini sokoni

hapa pia ni chake chake pemba ktk pirika za hapa na pale
moja ktk kijana mwenye kujitahidi kijenga caffae yake na wakati huwo huwo anafanya
biashara yake.

fukwe za bahari hapa pemba


ona pemba ilivyo tulia ktk fukwe zake ona mchanga ulivyo mweupe safi kabisa

ona mathari nzuri ya bahari ya kisiwa hichi cha pemba

usiku hapa pemba na umasikini wetu lakini tunajivunia pemba yetu

shekh akitowa mawili matatu kwa vijana hapa pemba

hapa ndio pemba yetu na gari zake za abiri ktk pirika za hapa na pale

pemba yetu hiyo inayo nukiya marashi ya karafuu

watoto wakicheza ufukweni hapa pemba

ona green ilivyo shamiri utafikiri uko jamaica kumbe ni pemba yetu

23 comments:

  1. dah picha nzuri sana,ni kivutio sana kwa watalii ila inasikitisha kuona ndugu zetu wa kipemba wamejenga sana huko tanganyika,wamewekeza huko tanganyika,na kukutupa hapa kwao pemba,lakini wakae wakifahamu home sweet home.

    Pemba ni sehemu nzuri ya kuekeza katika kibiashara hasa utalii na kilimo,ningelikuwa na uwezo basi ningeliwekza,lakini nia ipo inshallah nikiwa na uwezo nitajenga hotel na kufungua biashara ili ndugu zetu wapate ajira,nasi tunufaike wote kwa ujumla

    ReplyDelete
  2. Thanks man for the wonderful piece of info. Its sweet, vargin and stressless land of opportunity. Let authority open more to attract investments.

    ReplyDelete
  3. Office ya waziri kiongozi pemba inatia aibu kama gofu,noma kweli,nakuomba mwenye hii website ambaye muekeja wa habari tupatie picha za tanganika ofice zao za serikali zote,ikisha tuekee picha na majengo ya serikali ya zanzibar,pia tunataka hopital za tanganika na zanzbar.

    Hii itawavumbua wazalendo wapi tulipo.

    ReplyDelete
  4. nimewahi kuweka picha hapa labda huja angaliya miezi iliyo pita nimeweka na inasomeka kama hivi-ANGALIYA PICHA KISHA JIULIZE JE NCHI HIZI MBILI KWELI ZINA HAKI SAWA?? ila pia nitajaribu kuweka picha za ofisi kama ulivyo sema sawa kabisa ili kuwamsha wazenji wote na kuona ni jinsi gani tanganyika imeinyonya zanzibar mpaka sasa wanapanga kuichukuwa iwe yao haswa na sisi watufukuze hii ndio plani yao sasa.

    ReplyDelete
  5. Thank you brother for this pics...i never was in Pemba but I enjoyed these pics. They are wonderful. I hope you tweet them so more people come to know about Zanzibar....

    from a Patriotic Zanzibari

    ReplyDelete
  6. Eti mkoloni mweusi wakati picha zote ni za watu weusi. Haya jidanganyeni, sisi waPemba tuliofunguka vichwa tupo bara, tumejitajirisha na tumependa ustaarabu wao. Mambo ni maendeleo siku hizi, mnaosubiri wanasiasa wawakombea basi mtasubiri sana. Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  7. Anonymous kama wewe ni mbara sistajabu ukisema hivi.ila kama ni mzanzibar nawakati kama huu ulimwengu mzima unajikombowa ili kila mtu akae nchini kwao na wewe unasema kama hivi basi unanishangaza sana tena sana ikiwa wewe ni mzaliwa wa zanzibar na unauchungu na visiwa vya unguja na pemba basi siwakusema maneno kama haya nakunuku((sisi waPemba tuliofunguka vichwa tupo bara, tumejitajirisha na tumependa ustaarabu wao))nakuliza swali je wewe huku penda ustarabu wa kwenu pemba.?ndio ukaja ndio ukaenda bara kutafuta ustarabu mwengine.?unathamini utajiri kuliko nchi uliyo zaliwa..?
    m/mungu inshaa allah akufunguwe tena hicho kichwa chako naona kama hakijafunguka kabisaaaaaaa.

    ReplyDelete
  8. Nakupa heko ya nguvu wewe mwenye website hii angalau sisi waPemba tutakuwa angalau na pa kusema yetu japo wengine yataudhi.

    Asante sisi tuko pamoja na wewe.

    ReplyDelete
  9. asanteni sana nyote munaotembeleya hapa na pia hii sio website yangu hii ni website yetu sote watu wa unguja na pemba sote na niko hapa kwa kufichuwa uwoza na uchafu uliyofinikwa kwa miaka mingi na unaendeleya kufinikwa na pia hapa kwa kuonyesha ukweli na sote kushirkiana kwa pamoja ili tujikombowe na kuvijenga visiwa vyetu vya pemba na unguja na maoni yenu hapa ndio yatakayo zidi kufumbuwa wengine macho na akili yatakayo wauthi basi hao ni mahasidi wa zanzibar nzima yani pemba na unguja na sisi hatutampa nafasi hasidi yoyote sasa kutufitinisha tena asante nyote m/mungu ibariki zanzibar.

    ReplyDelete
  10. Maisha ni po pote bwana ndiyo maana wengine wamekwenda Ulaya, wengine Oman, Marekani na kote duniani sembuse bara!

    Kila Mpemba mmoja aliyeko bara kabeda ndugu zake kadhaa wa kumsaidia katika shughuli zake za kazi, kama ni kuuza duka, ujenzi au cho chote kile cha kujipatia rizki. Cha ziada japo kidogo hurudi nyumbani kusaidia jamaa. Unadhani dogo hilo?

    Tukirudi sote tukajikunja na umaskini jee ndiyo maendeleo yatapatikana? La muhimu ni kusaidia kupeleka hayo maendeleo nyumbani ili angalau kung'are.

    ReplyDelete
  11. labda umenielewa vibaya mimi nia yangu sio watu warudi waje wajikunyate na umasikini bali warudi na kuijenga pemba ili ingare maana ndio kwetu.na mcheza kwao hutunzwa.

    ReplyDelete
  12. Mwenyeenzi Mungu azibariki Unguja na Pemba na watu wake wote wa kila kabila na rangi. Pemba ni nchi nzuri kupita kiasi, ina mandhari ambazo mtu yeyote hawezi kuona bila ya kusifu, lakini ina taka watu wake waindeleze nchi yao, kwani ipo nyuma kwa maendeleo bila ya kiasi (haya ni maoni yangu baada ya kwenda kutembea Pemba mwaka jana).

    ReplyDelete
  13. Fungua milango ya uchumi, na siasa ya chuki haitasaidiya na muwapokee mainvestors kwa imani na biashara na pemba itanyanyuka kama nchi za far east. Hakuna sababu yoyote kwanini pemba isiendelee mbele kuingiya kwenye dunia ya leo kama sehemu zzozte nyengine.

    ReplyDelete
  14. Eee Mpemba mwezangu. Ha wataka uwambiwe vipi mpaka uamini kuwa Pemba ni nzuri. Kunjisambika huko hwebu rudi au hwebu leta mapesa ukawekeza kwenye maendeleo watakani? Kake au dade yangu au ndudgu yangu, njoo uwekeze hapa Pembaaa, hata kama kunaamuwa ukifa uzikwe huko, bado hapa mpenuuu na mjengaji ni miye na weye, si wakujaaa.Ziole vizuri hizo picha na utafakariiii.

    ReplyDelete
  15. UZURI WOTE WA PEMBA HAFAIDI ANAEKAA AU ALIEZALIWA HAPO, ANAEFAIDI NI YULE MGENI ANATOKA NJE , NI UFAKIRI MKUBWA WENYE KUHZUNISHA ULIOWAPATA WATU WA VISIWA HIVI, NI VISIWA VILIOKUA NA KILA KITU LAKINI HAVIKUJITAWALA.HATUJUI KHATMA NA MWISHO LAKINI DUNIA YOTE ISHAENDELEA BADO SIE TU. ALLAH AWAFUNGULIE KILA LA KHERI WANAOISHI KWENYE VISIWA HIVI.

    ReplyDelete
  16. Very nice island lakini hasara haijapata serikali kuijenga, uchumi uko lakini untaka investment

    ReplyDelete
  17. Wengine wao Wapemba wanaogopa kujenga kwao wakichelea kurogwa! au kuonewa kijicho!

    ReplyDelete
  18. Keep up the campaign.May be one day those who chose to live out of the island will come back.

    ReplyDelete
  19. Mola aihifadhi (Amen)

    ReplyDelete
  20. Pemba Oyeeeeeeee...waliombali wanajitafuna kwa uzuri wake ila haijapata serikali tu....Allah atawafungua macho yao na kuona mbali penye kheri na waraiya wao...wa shukran.

    ReplyDelete
  21. ABA WEWE WAIJUA HADITH YA MSHIKAKI KWA DINARI NA NG'OMBE KWA DINARI.

    ReplyDelete
  22. The big problem of most Africa country is their Governments,how somebody can invest without protection from Government to his life and his proprety.Ruanda only is the safest place.

    ReplyDelete
  23. Asante picha nzuri sana ,basi ingekuwa ndege zinakuja Pemba direct bora nchi ingeendelea.

    ReplyDelete