Sunday, June 12, 2011

JE VISIMA SABA VYA GESI NA MAFUTA VILIVYOGUNDULIKA NCHINI TANGANYIKA VITAKUWA VYA MUUNGANO PIA AU VYAWATANGANYIKA TU..?



Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, amesema kasi ya utafutaji wa mafuta na gesi nchini imeongezeka.
Aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo ya ukaguzi wa mazingira kwa wakaguzi madini na nishati, iliyofanyika mjini hapa jana.
Alisema hadi sasa kuna leseni 22 kwa ajili ya utafutaji wa mafuta na gesi nchini.
Jairo alieleza kuwa, jumla ya visima saba vimegunduliwa kuwa na gesi asili, ambapo visima vya Songo Songo na Mnazi Bay vimekuwa vikitoa gesi inayotumika kwa matumizi mbalimbali.
Alifafanua kuwa, visima vingine ambavyo vimeonyesha uwezekano wa kupatikana gesi ya kutosha ni kisima cha Mkuranga, ambacho uhakiki unafanywa kuanisha kiasi cha gesi kilichopo.
Alisema utafutaji na uchimbaji mwingine unaendelea kwenye kina kirefu katika Bahari ya Hindi maeneo ya kisiwa cha Mafia

KAMA HATUKUAMKA GESI TUTAISIKIA TU
TUTAISHIA MAGARA YA NGOMBE MPAKA KUFA.
haya sasa oneni walivyo kuwa ni wabaya hawa watanganyika nawanuku((visima vya Songo Songo na Mnazi Bay vimekuwa vikitoa gesi inayotumika kwa matumizi mbalimbali.kupatikana gesi ya kutosha ni kisima cha Mkuranga,)) sasa wao wanavisima vyao vya mafuta na gesi na wanavichimba kwa kasi kabisa ila vilivyo pemba hawataki vichimbwe mpaka serekali ya zanzibar ikubali kuwa mafuta na gesi ikiwa itapatikana pemba basi iwe ni yamuungano jamaa wazenji bado tu tumelala hatuja amkaa...?

No comments:

Post a Comment