Wednesday, June 22, 2011

KARAFUU NI ZAWANANCHI SMZ WAACHIENI WAUZA WANAKOTAKA


HAWA NDIO WENYE HAKI YA KULA PESA ZA KARAFU
SIO ZSTC

WATU HATA HAWAZITHAMINI TENA KARAFU KWA WIZE WA ZSTC KUWA THULUMU WANYONGE WACHENI WAUZE WANAKOTAKA NYINYI ZSTC MAJAMBAZI WAKUBWA,WALAFI WAKUBWA,WATAPIA MLO WAKUBWA,MUMEKULA HARAMU TOKA 1964 MPAKA LEO BADO TU MUNATAKA KULA HARAMU..?

Libinafsishwe tuu,hakuna hivi wala vile hata nami sioni SMZ inasubiria nini.Ni nani asiejua vigogo waliopo nyuma ya ZSTC ? Kwa kuwataja wachache habari zilotufikia ni familia ya Karume ndio wenye share kubwa ndani ya mradi wa kuuza karafuu kupitia ZSTC.walizitaifisha kwa watu wa z;bar 1964 kisha wakawapa watu wanaowataka wao ili wao wale wakishiba basi sasa wakati umefika na wao pia wataifishiwe na rai wajipatie chao na wao waishi vizuri kama walizo iba hazijawatosha wala hazitawatosha tena.
Mkulima apoteze nguvu zake halafu wachache wafaidike na mapato.Nawashauri wananchi wakajipanga vizuri kutetea haki hii ya kutafuta soko la mavuno yao ya karafuu. Kama kwa hivi sasa kilo moja ya Karafuu inauzwa dola 178, lakini pishi nzima ambayo ni kilo moja na nusu ya karafuu hapa znz haifiki hata dola 25 sasa nani anaye vimba tumbo kama sio wao kisha ona wananchi wenye mikarafu nyumba wanazo ishi na wanaonunuwa karafu nyumba wanazo ishi wizi na unyonyaji tu basi hakuna lolote. Mambo ya ujamaa na kujitegemea ikawa SMZ inamiliki biashara imepitwa na wakati.

MWAKILISHI wa Wete, Assa Othman Hamad (CUF), ameelezea kushangazwa na uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kuendelea kung’ang’ania kumiliki zao la karafuu.
Hamad amesema,wakati wa Serikali kumiliki biashara pamoja na sekta ya kilimo kwa sasa umepitwa na wakati katika mfumo wa soko huria.
Mwakilishi huyo ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011-2012.
Karafuu inalimwa kwa wingi katika kisiwa cha Pemba ambako katika miaka ya 1972 Zanzibar ilikuwa ikiongoza duniani kwa uzalishaji wa zao hilo.
Amesema, kilimo cha karafuu kimeporomoka sana kutokana na wakulima kuvunjika moyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo bei ndogo wanayoipata baada ya kuuza karafuu kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC).
Mwakilishi huyo alisema hali hiyo imesababisha wakulima wa karafuu kushirikiana na wafanyabiashara kusafirisha zao hilo kwa njia ya magendo kwenda nchi jirani.
Zao la karafuu bado linaendelea kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZSTC ambao ndiyo wauzaji pekee wa karafuu ya Zanzibar nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mfenesini, Ali Abdalla Ali (CCM), alitaka kilimo cha karafuu kiimarishwe na wakulima wapatiwe utaalamu wa kilimo hicho.
Alisema hadi sasa kilimo hicho kimezorota visiwani hapa kwa sababu wakulima hawapatiwi utaalamu wa kilimo huku Serikali ikishindwa kuweka kipaumbele katika programu zake za kuimarisha kilimo.
“Mimi ni mkulima pia nalima karafuu lakini mwaka jana nilipanda mikarafuu 20, iliyoishi ni miwili tu na wakati huo huo nilipanda miti ya michungwa na yote imeota,” alisema.
Alisema, kwa kawaida mikarafuu inahitaji mazingira mazuri ya matunzo ikiwemo kupata mvua nyingi hivyo wataalamu wa kilimo wanatakiwa kuwapatia wakulima elimu ya kilimo hicho.
Alitaka kuimarishwa kwa vituo vya kuotesha miche ya mikarafuu ili wakulima wapate muda wa kununua miche hiyo kwa wingi huku wakipewa mafunzo ya kuotesha miche hiyo.
Hivi karibuni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni alipokuwa Pemba alisema Serikali itaimarisha karafuu ikiwemo kuweka bei nzuri itakayovutia wakulima hao.
Dk. Sheni alisema, karafuu bado bei yake katika soko la dunia ni nzuri hivyo Serikali itaweka mazingira mazuri kwa wakulima katika kilimo hicho.

ione ilivyo vimba

ona mikono yao iko wapi juu ya matumbo jinsi yalivyokuwa makubwa kama vyura wenye mimba za miazi19 na kuna rai wanakufa na njaa na wengine wana haha kupata ulo moja tu kwa siku pia una wahahisha na hawa ndio viongozi wa nchi wanyonyaji wakubwa.

ona ilivyo vimba hata kupumuwa haiwezi.

hata maji ya mferejini hawayataki tena wanakunywa ya chupa na chakula kizuri na huko nje kuna rai wengine hata mkate wa bofulo hawana uwezo wa kununuwa wanakula muhogo mpaka hawapati choo maana muhogo hata nazi hauna wala kipande cha samaki
na huko nje kuna rai hawana maji wana yatafuta hayo maji  na wakiyapata ni machafu ndani ya znz hii hii.

hao hapo juu ni viongozi waone walivyo na wanasema nchi ni masikini kisha ona hapa chipi picha za rai wa znz je kweli hawa viongozi ni wema hawa au ni matumbo yao tu
ona rai wa znz walivyo choka hata viatu wengina hawana  kisha angalia hao viongozi
ndio utajuwa hatuna viongozi tuna majambazi na watapia mlo na wanyonyaji.

No comments:

Post a Comment