Saturday, June 25, 2011

KARATA TATU ZA NYERERE ZAIDI YA MAPINDUZI YA Z;BAR 64


Sultani wakiarabu aliwapokea Tanganyika?, Waasisi wa mapinduzi aliwarudisha Z'bar kwenda kunyongwa?.

Mapinduzi ya 64 ktk plan za Nyerere sio kumgomboa Mzanzibar au Zanzibar
kuwa huru, hakuna shaka ktk mapinduzi ya 1964 walouwauwa sio Warabu na
Wahindi tu pekee , Wzanzibar wengi weusi waliuliawa mamia kwa mamia na
uvamizi wa Wageni wenye asili ya Bara na Unganda(John Okelo).

Zamira halisi ya Nyerere nikuitawala Zanzibar na Kuuwa uislamu Zanzibar,
kuitawala Zanzibar hakuna shaka hilo kafanikiwa kutokana na kupandikiza
mbegu za Tanganyika kwa kuwapa nafasi nyeti za Nchi na kuwauwa
Wzanzibar wasomi, lakini lakuuwa uislamu hilo kashindwa.
Sasa tuangalie mchango wa Juliasi na athari za mapinduzi ktk mapinduzi ya
64? Nyerere alikuwa na mawazo mbali na mawazo walokuwa nayo wanaojita
Wasisi wa mapinduzi ya 1964(Wazawa wa Ki-Zanzibar). Akina Othmani
Shariff,Mdungi Usi,Ubwa Jaha na Wenzake Wazawa wa Ki-Zanzibar.
Nyerere kwa lugha ya kigeni tunasema aliwaona (Foolish) wana mapinduzi wa
Zanzibar kwa lengo lakuitawala  Zanzibar kimbinu na kiujanja ujanja ili
zamira yake iwe alijifanya (Master mind),
Ni zipi athari za Nyerere baada ya mapinduzi ni kuwauwa Wzanzibar
wasomi,wana mapinduzi wazaliwa halisi wa Zanzibar na Wazanzibar na
kuweka watawala wenye asili za Kigeni(Tanganyika) kushika nafasi nyeti
za nchi ambayo mizimu yake na mabaki yake mpaka leo ndio inayo isumbua
Zanzibar.
Kuna mambo mingi ya lijitokeza ili kumshuku Juliasi kuwa hakuwa na nia
njema ya mapinduzi ya 64 kwa Wzanzibar, bali lengo kubwa nikuitawala
Zanzibar kuwa ktk himaya yake, haya yalijitokeza vipi? Baada ya
kuwa-(Brainwash) na kuwatumilia wasomi wa Zanzibar Othmani Shariff na
wenzake na baadae kuwageuka na kuwakata roho, hii ndio ilikuwa malipo
yao na kumfanya kafiri kuwa kiongozi na rafiki mpenzi wakukupangia mambo
yako.
Sasa tuangalie sababu ya kuwauwa hawa ilitokana na nini? kwanza ni
woga wa Nyerere kuwa pindipo akiwapa nafasi kubwa kubwa hawa atashindwa
kutimiza zamira yake ya kuitawala Zanzibar kwa vile hawa walikuwa ni
Wzanzibar hasa Bibi na Babu a. halafu sababu nyingine wengi wao walikuwa
niwasomi wakubwa Zanzibar kwa hio wangewaza kufanya mingi kwa Zanzibar
na lamwisho ni waislamu ambao Nyerere kwa kushirikiana na wa bara la ulaya
walikuwa wakipinga kuenea kwa uislam afrika masharaki.
Ndio ukaona hata mchakato wa mapinduzi yenyewe yalipangwa kimbinu
yafanyike  J,mosi kuamkia J,pili na Muengereza alikuwa ndio Mlinzi
(Protector) wa Zanzibar , lakini yalipo tokea mapinduzi hakuweza kufanya
chochote zaidi ya kumsafirisha Mfalme wa Zanzibar kumtowa ktk himaya
yake na kumpeleka Bara ili kwa Safari ya Uengereza.
hii ilikuwa ni mbinu imeshapangwa na Muengereza alishiriki kikamilifu na
alipo ombwa kutowa ulinzi alikataa na kusema yeye siku ya Jumamosi na
Jumapili hafanyi kazi ni siku ya ibada, sasa kama yeye hafanyi kazi
mbona aliweza kumsafirisha mfalme na kumpeleka nchi jirani Tanganyika?
a.) b.) Kama Nyerere alikuwa na nia safi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 64
mbona yeye ndio aloshiriki kikamilifu kuwasafirisha Warabu,wahindi na
Wazanzibar wenye kuondoka Zanzibar kwenda Tanganyika kuomba hifathi?.
Na wakifika Tanganyika hakuna mtu kuguswa lakini vijana wake waloko
Zanzibar waliamuriwa kuwauwa Warabu na Wahindi na watu wausi kuonyesha kama kigezo tu
cha harakati za mapinduzi kuonyesha kuwa alopinduliwa ni Muarabu lakini
uhakika walopinduliwa ni wzanzibar na wengi walipoteza roho ktk
mazingira tafauti ya utatanishi ni Wazanzibar halisi.
Mfalme na gengi lake hakuguswa alisafirishwa kwa lengo lakupatikana nchi
ili Nyerere aweze kuitawala na bara la ulaya wapate kuvunja nguvu za
waislamu, kama kweli Nyerere alikuwa na zamira njema kuhusu mapinduzi
asinge pokea Warabu Tanganyika wakatii kama wa mapinduzi au anavyo waita mwenyewe na wana  mapinduzi ASP (Masultani wa Kiarabu).
Lakini chakushangaza nikuwa aliwapokea Tanganyika na kuwapa hifadhi bila
kuguswa haliyakuwa huku Zanzibar alitia kasumba za kusema ni watu
wabaya na niwatu wa hatari Sultani, lakini hao watu wabaya aliwapokea
na kuwapa hifathi na wale Wasisi wana mapinduzi kinaga naga akina Othmani
Shariff , Mdudi Ussi na wenzake Baada ya mapinduzi kudai hasusa ya vyeo
na kukataliwa na Nyerere kuweka Ndugu zake aliaza kampeni nyegine za
kumwabia mzee Karume awatie magerezani na baadae awakate roho.
Hoo ndio Wzanzibar halisi waasisi wana mapinduzi lakini kinyume chake
ndio walokuwa wahanga wa mapinduzi na waliofanyiwa magerezani hayasemeki
kabla ya vifoo vyao, wako waloweza kuchomoka na kukimbilia Tanganyika
ili kuweza kupata hifadhi, lakini kutokana na Nyerere kuwa Ndumi
lakuwili aliwarudisha Zanzibar na kumkabithi mzee Karume amalize kazi yake ya kuwakata roho zao.
Sasa hii ndio zamira kubwa ya Juliasi na kundi lake la kijasusi ambalo
mizimu yake na mabaki yake yanaisumbua Zanzibar mpaka leo, hakuna shaka
kuwa mapinduzi ya Zanzibar hayaja wafaidisha baado wana wa Zanzibar
kufurahia uhuru wao mpaka hii leo bado nimisiba na majonzi wanayokwenda
nayo na Muungano ndio kitanzi kikubwa kinacho iumiza Zanzibar, Nyerere
kafa lakini mikakati na mbinu zake bado ndugu zake wanaedeleza, kuwa
uchumi wa Zanzibar ili kuwahamisha Wzanzibar matajiri wafanya biashara
wakubwa kuwavutia upande wake a.).
B.) Kuwatumilia Wzanzibar akina Samia,Nahodha, ili kuwapa viji
vyeo ili kuisalimisha Zanzibar kwa Tanganyika,. hizi ndio mbinu za
Nyerere na ndugu zake wakishirikiana na bara la ulaya, Nyerere ni choyo cha
kuvitamani visiwa na bara ulaya walimtumila ktk kuwaa uislam.
Hili la kuwa uislam sio Zanzibar tu, bara ulaya walimtumilia nchi nyingi tu
za kislamu kupenyeza sumu zake, mfano kama Naigeria kule Biasra,Ethiopia
na kwengineko, hata kule Naigeria ktk jimpo la Biasra walipo taka
kujitenga Nyerere alipigania kifua kuwa lazima wajitenge kwa vile wengi
wao ni wakatoliki na aliulizwa kuhusu Zanzibar wakitaka nawao kujitenga
vipi? akajibu hakuna matatizo kwa vile ni nchi mbili zimeungana mmoja
ikitaka kujitenga ok.
Lakini uhakika sio hivyo tunambiwa tulinde na tudumishe Muungano kwa
nguvu zetu zote,hata kuwa ni toto lisilo pendeka na katili mkubwa,
lakini tunambiwa tusiuchokonyowe na wasio taka Muungano wakatafute ardhi
yao waishi, kifupi asilimia ya 90 ya Wzanzibar wazawa hivi sasa
hawautaki hata kuona Muungano kwa hio tunaambiwa tukatafute ardhi
nyingine ili tupishe wageni ambao ni watanganyika na vibaraka wetu hapa waendeleze zulma.
Mungu ibariki Zanzibar na Wzanzibar wote

1 comment: