Friday, June 24, 2011

MAJONZI,MASIKITIKO,FETHEHA,KAMA SMZ HAIKUVUNJA MUUNGANO WATATUNAKAMISHA W,Z;BAR


hali ngumu ya maisha na mzigo mzito wa Muungano.
Hivi sasa mzigoo waliotubebesha Serekali ya SMZ umekuwa mzito na siku
hadi siku unazidi kutuinamia, mimi nawabebesha lawama kubwa %75 viongozi waloko Serekalini wakiongozwa na Rais shein wanastahili kubeba lawama na
jukumu kwa vile wao ndio viongozi wetu na hawako tayari kutushirikisha
Wzanzibar ktk hatma ya Zanzibar inakoelekea kumezwa na kupoteza thamani yake.
Mimi ni mmoja ambao naungana na wezangu kuwa Muungano huu tunaokwenda
nao ufe na tubakie nchi mbeli jirani zenye utamaduni tafauti,kama kenya na sisi au uganda na sisi ni majirani tu na tunaishi nao kwa salama na tanganyika iwe hivyo nasema
hivi sio kwa kuwa sipendi Muungano no, hali ya Muungano tulionao ni
mbaya ki-dini,kimila na kiuchumi wa Zanzibar.
Tukija ktk Dini, hali ya Zanzibar inatisha kwa sasa,tumeletewa utamaduni
na mila zisizo za ki-Zanzibar ambazo % 100 ya Wzanzibar ni waislamu na
wenye mila zinazo fuata uislamu.
Leo hii ukenda ktk Fukwe za Zanzibar utashindwa kujuwa kuwa uko Zanzibar
au Itali Rome, ukija Mji mkongwe ndio usiseme hakusemeki utazani uko
Manzese au mwananyamala au sehemu zenye uchafu wa kuuzaa ..?
Hili loto ni jukumu la viongozi wetu wa SMZ 75% wao ndio wakuwalaumu
kutokana na kuwa na nyuso mbili na ubabe wao mkubwa wakutukadamiza na
kuzidisha ghathabu kwa Wzanzibar kutatua hatma ya nchi yao.
Kila penye fursa ya Wzanzibar kushikamana na kujikombowa ktika minyororo
ya ukoloni wa Tanganyika ndio viongozi wetu huzidi kujipendekeza na
kuwa watifu kwa Tanganyika na kushindwa kuisimamia Zanzibar kiuzalendo,
hubakia kulinda na kudumisha itikadi za chama huku Zanzibar na
Wazanzibar wakizidi kuangamia kwa umaskini na kupoteza muelekeo wa
ki-Zanzibar  katika dini.
Kama kweli viongozi tulio wakabidhi nchi wanataka kuvunja Muungano na
Zanzibar kuwa huru na kujiamulia mambo yake wenyewe basi mimi nasema
Baraza la Uwakilishi wanaweza , na nikitu cha dakika tano tu, ikiwa
Wawakilishi watasema kuwa Muungano basi. basi hakuna wakuwalazimisha
kwanguvu.nyerere aliye ungana na mzee karume alisema kama wazanzibar hawata taka tena muungano. sito wapinga mabomo sasa kwa nini baraza la wawakilishi wanaogopa kuvunja muungano. huu usiokuwa na maslahi ya wananchi au maslahi yao basi ndio sisi wananchi tuendele kuangamiya na maisha kwa kuwa mawaziri na wabunge wananufaika?
Muungano sio kulazimishana nirizaa za pande mbili mmoja akisema basi
inamana basi,lakini still viongozi wetu ni wanafiki na Muungano upo
Zanzibar sio tena kwa ridhaa bali kwa kufosiwa na viongozi wetu wa SMZ
kujipendekeza Tanganyika na kuhisi riski zao zinatoka Bara.
Wanao sema kuwa tusiwalaumu viongozi wetu wa SMZ na wao niwanafi vile
vile,ikiwa wao ngoma imekuwa mzito kwao au wanaoneleana haya na
Tanganyika kwa nini suala la hatma ya Zanzibar lisirudishwe kwa
Wzanzibar wenyewe wakamuwa kama muungano au laa kwa jili ya hatma ya nchi yao?.
Lakini viongozi ni wanafi na wamekumbatia sana chama kwa maslahi yao
binafi,na wanajuwa wakiyalete kwa wananchi kuamuwa muungano au laa wanajuwa ni laa ndio maana hawataki kuleta kwa wazanzibar kuamuwa. kuna vituko vingi na viroja viongozi wetu wanavyo tufanyia,kwanza masuala makubwa ya mamuzi ya Wzanzibar huyakwepa kuwapelekeaWzanzibar wenyewe na Baadae hubabaisha na kuingiza ubaguzi.Jengine ni inapo onekana dalili kwa njia hii au nyingine ya Zanzibar
kuhujumiwa au kutharauliwa hutokezea fisadi kwa kulinda maslahi yake binafsi
 hujipendekeza Tanganyika kwa shabaha ya kuiathir Zanzibar.
Mifano iko mingi tu yakuwalaumu viongozi kutokana na uthaifu wao na ndio
wakachezewa na W-Tanganyika na wakatuangamiza ss na Zanzibar kwa ujumla.
hivi sasa kuna jungu linapikwa kuhusu Mswada wa Katiba? Zanzibar
inasimama kama Zanzibar Tanganyika inasimama kwa jina gani? TANZANIA KWA NINI...?JEE MZEE KARUME ALIPO UNGANA ALIUNGANA NA TANGANYIKA AU TANZANIA...? jee hii ni haki Tanganyika kuvaa Koti la Tanzania? ni lini au siku gani kusikia Wawakilishi wetu au SMZ kusema Tanganyika irudi?.
Kikubwa huambiwa Tudumishe na tulinde MUUNGANO ABAO TUNAJUWA NI FEKI HUU wa TANZANIA na ZANZIBAR.
jee Wzanzibar nipumba au wajinga kiasi gani kubadilishiwa kibao?tutafika
wakati tutachekwa ktk ushirika wetu wa Muungano kuandikiwa Reciet kwa
mshirika lakuwa sie.
M/mungu ibariki zanzibar  na uwaangamize wenye thamira mbaya na Zanzibar.


No comments:

Post a Comment