Monday, June 20, 2011

MIL.780 WALIZO PEWA KIKOSI CHA MAJI KMKM HAKUNA KARATASI YAKUONYESHA ZIMETUMIKA VIPI NA WALA ZIKO WAPI PESA HIZO




Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) kimeshindwa kuonyesha nyaraka za mamilioni ya fedha walizopewa na Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar katika mwaka wa fedha 2008/2009.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2008/9 kikosi hicho kilipewa Sh milioni 780.1, lakini haijaelezwa jinsi fedha hizo zilivyotumika.
Ripoti hiyo inaonyesha kiwango hicho cha fedha kiliingizwa na wizara hiyo, lakini viongozi wa KMKM wameshindwa kuonyesha nyaraka za fedha hizo kama walivyotakiwa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
“Wakaguzi wamebaini kwamba kikosi cha KMKM kimepokea nyaraka za kuingiziwa fedha kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi, lakini nyaraka hizo hazikupatikana wakati wa ukaguzi wake,” imeeleza ripoti hiyo.
Fedha hizo ziliingizwa kwa awamu mbili Agosti 4, na 29 mwaka 2008 kupitia waraka namba MFEA/B10/0715 wenye kiwango cha fedha milioni 390,081,007 na waraka kwenye kumbukumbu namba MFEA/B10/08/47 chenye kiwango cha fedha 390,081,007 ambazo zilitolewa na wizara hiyo.
Kikosi hicho cha KMKM pia kimeshindwa kutoa uthibitisho wa matumizi wa Sh milioni 52.5 fedha ambazo zinadaiwa zimetumika kwa ajili ya kazi za maendeleo ya kikosi hicho.
Ripoti hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa serikali yenye kurasa 305 imesema, wakaguzi wa hesabu wameshindwa kuthibitishiwa matumizi ya fedha hizo kitendo ambacho ni kinyume cha matumizi ya fedha ya mwaka 2005.
Aidha KMKM imeshindwa kuunda kamati ya ukaguzi wa hesabu katika kikosi hicho, kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za fedha Zanzibar kifungu namba 28 cha mwaka 2005.
Vile vile imebainika kuwa mali za kudumu za kikosi hicho zimekuwa zikiorodheshwa bila kuwekwa thamani, kama inavyotakiwa na sheria ya fedha kifungu cha 24 (2) cha mwaka 2005. Alisema hadi kufikia Juni 29, 2009, kikosi hicho kilipewa Sh bilioni 5.3 kwa ajili ya kazi ya kawaida, sawa na asilimia 99 kati ya fedha zilizokuwa zimeidhinishwa kwa mwaka huu wa fedha.
“Ukaguzi umebaini kikosi cha KMKM hakiweki daftari la kuhifadhia mali za kudumu, hali hiyo huweza kusababisha upotevu wa mali hizo.”
Ripoti hiyo imekitaka kikosi cha KMKM kuwasilisha vielelezo na maelezo juu ya matumizi pamoja na nyaraka zinazoonyesha kupokea fedha na matumizi yake.
Ripoti hiyo pia imeeleza kuna malipo ya Sh milioni 3.1 amelipwa mkuu wa KMKM kupitia hundi namba 249838 ya Novemba 11, 2008 bila kuwepo stakabadhi ambazo walitakiwa kuambatanisha na hati ya malipo kwa mujibu wa kifungu cha 95 (4) cha sheria ya mwaka 2005.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti Mkuu wa serikali, Fatma Mohammed Said alisema kwamba baada ya ripoti hiyo kutolewa hatua inayofuata ni kuona vitendo hivyo vinadhibitiwa kwa vile ni kinyume na sheria na misingi ya utawala bora.
Alisema katika ripoti iliyotolewa hivi karibuni, imebainika Sh milioni 413.6 zilifanyiwa malipo katika wizara mbalimbali bila kuwepo mikataba kupitia wizara mbalimbali ya SMZ.
Sh milioni 51.8 zimetumika bila kuambatanishwa vielelezo vya uthitisho wa malipo katika hati za malipo, kitendo ambacho ni kinyune na sheria
ONENI MELI ZA KMKM ZA WENZETU SIO KMKM WETU PESA KUIMBA NA
KUJAZA MATUMBO YAO TU HATA INCHI IKIVAMIWA HAIWEZI KUJISAIDIA.
HAWA NDIO KMKM SIO ZNZ WAULIZE KUONEYA WAVUVI TU BASI
WANAJUWA UMUHIMU WA KULINDA NCHI YAO
UNAONA KMKM HIYO HAWA WETU HAPA ZNZ WENGI WAO MACHOGO
HATA KUONGELEYA HAWAJUWI KISHA KMKM MAWE LABDA
HII NDIO KMKM HAWA TULIYO NAO SISI NI GANGA NJAA UWONDOKE
KMKM HAO SIO MCHEZO HAO WETU WAKISIKIA UKUTI TU
WASHAKIMBIA ZAMANI
KMKM HAO KILA KITU KIPO PESA ZINAONEKANA ZILIPOTUMIWA WETU ZNZ HAZIJULIKANA PESA ZIMEKWENDA WAPI NA WALA HAWAULIZWI WALA HAWAPELEKWI MAHAKAMANI KISHA TUNATAKA KUJENGA NCHI MAWE NAFIKIRI KUJENGA NCHI MCHEZO..?
HII NDIO KMKM YATU YA HAPA ZNZ NI GANGA NJAA UONDOKE TU
ONENI KMKM HAO SIO HAPA ZNZ KAZI KUZUGANA TU MIYAYOSHO MINGI PESA ZA KMKM HAZIJULIKANA ZIKO WAPI PESA ZA JESHI DAAAH
AMAKWELI ZNZ SIO NCHI NI JAA LA TAKA KILA MOJA ANAKUJA AKITUPA ZAKE AKIONDOKA NA SISI TUMO KUWACHAGUWA TUKIWACHANGUWA KILA UCHANGUZI MPYA SURA ZILE ZILE AIBU HATA KUSEMA ZNZ ZNZ INASIKITISHA WALAHII
ONA MAMBO HAYO VIJANA WANGAPI WAMEPATA AJIRA UNAFIKIRI KAMA ZNZ INGELIKUWA NA HII KUSINGELIKUWA NA KIJANA HATA MOJA ANAYEVUTA BANGI WALA UNGA MAANA WOTE WANA KAZI YA KUFANYA HAKUNA TAIMU YA VIBARAZANI NA MASKANI ILA KILA KITU KIMECHUKULIWA NA MACHOGO VIJANA WA ZNZ WANAZURURA TU NA KULALA BASI HAO WAKUBWA WA KMKM ZNZ WAELEZE PESA WAMEZIPELEKA WAPI KAMA HAWANA WASHATAKIWE NA WAFUNGWE JELA NDIO FUNDISHO KWA WANGINE ILA HAKUNA HAYO ZNZ KWASABABU TUNATAWALIWA NA WATANGANYIKA VIONGOZI HAPA ZNZ SIO VINGOZI NI VIBARAKA WA WATANGANYIKA MAANA KAMA NI VIONGOZI WANGELIWAMBIA MAFUTA NI YETU NA HAYAMO KATIKA MUUNGANO,TUNAPANDISHA BENDERA YATU NA TUNAKWENDA KUDAI KITU CHETU U.N.KAMA MWANACHAMA WA U.N. KAMILI NA TUNA SARAFU ZETU NA KILA KITU KISHA TUNA MUUNGANO WA KIURAFIKI TU LAKINI HAWAWEZI MAANA WOTE MAJOGA ILE MBAYA NA KILA MOJA KARITHIKA NA FUPA ALILOPEWA ANYONYE NDIO MAANA ZNZ INAZAMA NA ITAENDELEYA KUZAMA.

No comments:

Post a Comment