Thursday, June 9, 2011

NIMEKUJA KUIWAKILISHA SEREKALI YA TANGANYIKA HAPA U.N.

Makamu wa Rais wa Tanganyika, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini New York.
Makamu wa Rais wa  Tanganyika, Dkt. Mohammed Gharib Bilal yupo mjini New York, Marekani ambapo anahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi ulioandaliwa na UNAIDS.
NCHINI  TANGANYIKA
Anuani ya Simu: “MAKAMU” Ofisi ya Makamu wa Rais wa tanganyika,
Simu Na.: 2116919 S.L.P. 5380,
Fax Na: 2116990 Dar es Salaam,
Tovuti: http://www.vpo.go.tang/- Tanganyika.
TAARIFA KWA UMMA
MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL KUIWAKILISHA TANGANYIKA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI
Makamu wa Rais wa Tanganyika, Dkt. Mohammed Gharib Bilal yupo mjini New York, Marekani ambapo anahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi ulioandaliwa na UNAIDS. Makamu wa Rais anaiwakilisha Tanganyika katika mkutano huu unaojumuisha pia asasi za kiraia, uwakilishi wa vijana, wabunge, wadau katika mapambano dhidi ya Ukimwi nchini.
Makamu wa Rais kwa mujibu wa ratiba iliyopo atakuwa anatoa hotuba ya Tanganyika Juni 08, 2011 na hotuba yake inafafanua kuhusu nafasi ya Tanganyika katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi huku akisisitiza juu ya wananchi wa Tanganyika pamoja na serikali yao wanavyojitahidi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya yanazidi kupungua kuliko kuongezeka. Makamu wa Rais ambaye ameingia hapa jana anaambatana na Mama Zakhia Bilal ambaye naye ataungana na wake wa viongozi wa nchi mbalimbali katika mijadala ya nafasi yao katika kukabiliana na janga la Ukimwi, pia yupo Waziri wa Afya wa GNU wa serekali ya zanzibar Duni Haji Duni, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa GNU wa serekali ya zanzibar Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatma Fereji na viongozi wengine wa Wizara ya Afya waliokuwa wakitarajiwa kufika jijini hapa jana.
Katika siku hiyo hiyo ya Juni 08, 2011 Makamu wa Rais wa serekali ya tanganyika Dkt. Bilal anatarajiwa kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo mazungumzo yao yanatarajiwa kuzungumzia nafasi ya Umoja wa Mataifa katika mapambanao dhidi ya Ukimwi. Makamu wa Rais wa tanganyika pia atakuwa na mikutano kadhaa iliyoandaliwa na nchi za Marekani na Uingereza ambao ni wadau wakubwa katika kuisaidia Tanganyika katika mikakati yake ya kupambana na Ukimwi. Katika mkutano wake wa kwanza na wawakilishi wa Tanganyika kabla ya mkutano huo, Makamu wa Rais wa tanganyika ametoa rai kwa wawakilishi wa Tanganyika, kuhakikisha wanafatilia mkutano huu kwa umakini na kuandika ripoti zao kwa lugha ya Kiswahili ili punde mkutano huu unapoisha ripoti hizo ziweze kuwafikia wananchi wa Tanganyika kupitia njia zote za mawasiliano. Tena amesisitiza juu ya umuhimu wa wawakilishi wa Tanganyika kuhakikisha kuwa wanautumia mkutano huu vema na kuwakilisha mawazo ya Watanganyika kwa ajili ya kuisaidia Tanganyika yote.
Kwa mujibu wa Ratiba ya Makamu wa Rais wa tanganyika, atakutana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro siku ya mwisho ya mkutano, huku pia akitarajia kuwa na mahojiano na vyombo kadhaa vya kimataifa ili kufafanua nafasi ya Tanganyika katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Imetolewa na FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI.
Bilal
makamo wa raisi wa tanganyika akisalimiyana na raisi mpya wa comoro huko
comoro aliko huthuria sherehe za kuampishwa raisi mpya wa comoro.raisi wa comoro mpya kamuliza Mmhhaaiio huko ktk serekali yako ya tanganyika hakuna vijana? maana wewe mzee tena.

makamo wa raisi wa tanganyika akisalimiyana na raisi aliye maliza muda wake nchini
comoro je wewe utamaliza lini mdaa wako maana wewe  pia mzee raisi wa comoro anamuliza bilal..?

makamo wa raisi wa tanganyika akisalimiyana na raisi wa Madagascar, Andrew Rajouline ila raisi wa madagascar anaona duuuuuuuh babu bado tu utajiuzulu lini..?

makamo wa raisi wa tanganyika alipo wasili kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan, aliyeapishwa  Mei 29 jijini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo jijini Brazzaville, jana Ijumaa, Juni 3, 2011 kuhudhuria Mkutano wa 3 wa Nchi za Tropiki zilizo katika ukanda wenye misitu mikubwa na mvua nyingi. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka katika nchi zaidi ya 30 zilizo katika ukanda huo, mataifa yaliyoalikwa sambamba na mashirika ya Kimataifa yanayoshughulika na masuala ya mazingira. Picha na ofisi ya Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa tanganyika Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanganyika  katika mkutano  uliofanyika katika jiji la Brazzaville, Jamhuri ya Watu wa Kongo ambapo Tanganyika ilishiriki kama nchi mwalikwa

No comments:

Post a Comment