Monday, June 27, 2011

VIJANA WA Z;BAR KTK JUMUIYA YA UAMSHOJumuiya a Uamsho na Mihadhara ya kiislamu zanzibar (UAMSHO) imeandaa kongamano la vijana kuhusiana na masuala ya kutaka kufahamu masuala mbali mbali ikiwemo suala la katiba mpya na kujitayarisha namna ya kutoa maoni wakati wa utengenezaji wa katiba mpya ya tanzania na haya ndio baadhi ya maoni ya vijanwaliokuwepo katika ukumbi wa beit al aamin Malindi Mjini Zanzibar.
Khalfan Ali Faki
Vijana tumekata tamaa, vijana tuna jukumu la kusema au kutetea maslahi ya Zanzibar, tunashukuru UAMSHO kutukusanya pamoja hapa, tunalaani kauli za Mohammed Aboud kutwambia tusubiri suala la mafuta kuondolewa katika orodha ya muungano.
kumbe haiwezekani suala la mafuta kutolewa katika orodha ya muungano mpaka waulizwe watu wa bara, na kama haiwezekani mbona rais wa Zanzibar kukataa kwenda kuapa kule bara kama waziri asie na wizara maalumu? Na kwa taarifa nilizonazo mpaka sasa rais amekatazwa na baraza la wawakilishi asende kuapa.
Tuhakikishe kwanza tunawaandama viongozi wetu wakuu, tunalaani kauli ya makamu wa pili kuwa ukiwa na kidonda hukatwi mguu sisi tunasema kama upo uwezekano wa kukata kidogo basi tupo tayari kukata hata kichwa licha ya mguu.
viongozi wetu wanatusaliti kwa hivyo hatukubali tunataka viongozi ambao wameshafanya kazi kule Tanganyika basi wasipewe nafasi za juu kwa sababu hao ndio wa kwanza kuizamisha Zanzibar kule bara kwa sababu ya kuwa wamelewa kimadaraka.
Iddi Abdallah Ali
Huu muungano sisi hatuutaki maana hauna usawa huu ni muungano wetu ambao unaonesha kama tumevamiwa kwa sababu hakuna usawa Zanzibar ilikuwa na uhuru wake kamili lakini sasa wabunge kule mia tatu huku 50 inawezekanaje, bunge lenyewe limepelekwa kule porini katikati ya Tanganyika?, kule ni porini hakufai kabisa, bunge lirejeshwe huku haraka sana au liwekwe katikakati kati ya Zanzibar na tanganyika analau hapo dae es salaam au tanga lakini kule porini.
wawakilishi na wabunge wawe ni sawa kwa sawa hata kama nyumba kumi mbunge mmoja lakini hivyo hivyo wenyewe tumeridhika, na ikiwa tunataka kuendelea na muungano huu huu basi hatunufaiki kitu basi hakuna haja ya kuungana kabisa.
Nassor mohammed said
Tatizo kubwa ni sisi wenyewe ambao tunabaguana kutokana na upemba na uunguja hasa vijana ikiwa tunatajipanga kuwa wamoja basi tutafanikiwa lakini ikiwa tunaendelea na chuki za kisiasa basi daima tutaendelea hivyo hivyo, wataendelea kutudhalilisha na kutugawa jambo la msingi tuwe wamoja maana hata afrika kusini ilikuwa hivyo hivyo walikuwa vijana kutka nje wakiuliza lakini tatizo wapo watu ambao walikuwa wakipanga kuwauwa na wengine wakipanga kuwaokoa na hiyo inaonesha kwamba hakukuwa na msimamo wa kauli moja kwa vijana.
Ali Kombo Hamad.
Mapema Tanganyika wameanza kutupoteza maana walikuwa na nia mbaya ya kutaka kutuangamiza, suala la umoja na la kuungana ni zuri sana na muungano ni mzuri sana na hata katika uislamu unahimiza muungano kwa maana ya umoja lakini huu muungano wetu umetupotoshwa kwa sababu wenzetu hawakuwa na dhamira ya dhati katika suala la kutaka kuungana.
Mheshimiwa Abubakar hapa amekuja kutwambia kwamba hili ni jukumu letu vijana lakini mimi nasema jukumu hili tusiambiwe sisi vijana tu tunataka kwa kuwa tumekaa kimya hatusemi chochote hata na wao wenye jukumu yaani wawakilishi ambao ndio wenye fursa nzuri ya kutoa maamuzi katika vikao vya baraza wana jukumu hilo.
sisi tutaendelea kusema lakini wenye maamuzi ni wawakilishi ambao wana mamlaka. Hatuwezi kuogopa kuwa na Zanzibar yetu kwa kuogopa eti kwa kuwa serikali ya muungano itakasirika iwapo sisi utatoa maoni yetu au tukisema hatuaki muungano.
Said Juma Mbarouk
Kwa mujibu wa sheria katiba zote zina nguvu sawa hakuna katiba kubwa wala katiba ndogo zote zipo sawa katika nchi yake, kumbe uwezo tunao wa kutoa maamuzi lakini ni sisi wenyewe wazanzibari kumbe hatujaweza kutumia fursa hiyo ya kusema ukweli na kuidai serikali ya muungano juu ya haki ya Zanzibar.
Kumbe viongozi wa Zanzibar hawajajiamini. Licha ya muungano kuwa utakuwepo lakini zanzibar iheshimiwe na haki Zanzibar zielezwe kabisa, muungano wa kuwa chao chao chetu chao hatuutaki, tupo tayari kufa lakini tutaitetea nchi yetu kwa nguvu zote.
Muungano huu sio wa wananchi ni wa kuchanganya udongo tu Abeid Karume na Julius Nyerere, katiba ya Tanganyika ndio iliyooungiza vipengele hivi sio katiba ya muungano. Zanzibar iliingia kama nchi kamili yenye mamlaka kamili makubaliano ya article of union isiwe sababu ya kuwa Zanzibar haipo, tunataka tuelezwe yepi ni yepi.
1967 Nyerere alisema muungano wetu ni wa nchi mbili zenye mamlaka kamili tumeungana kwa kila nchi ina mamlaka yake, kwa nini kila wakati wende wakaombwe wao kama mabwana alaa, Amani alituwekea njia sasa ni rahisi kuzifuata, tunataka kura ya maoni dhidi ya muungano kama tunautaka au hatuutaki lakini hatutaki mdahalo wa muungano.
Kombo Haji Kombo
Suala hili ni kama harusi tunakwenda kutengeneza katiba na hakuna haja ya kumtaja Karume au Nyerere hii tunakwenda kutengeneza harusi ili bi hausi na mumewe waishi namna gani ndani ya nyumba yao, hayo aliopita ndio ameshapita kama makosa waliyenda wazee wetu ndio wameshatenda ili sisi tusitende makosa kama wao basi tunajukumu la kurekesbisha hapa tulipo sasa.
Tujipange na hoja za msingi na sio jazba wala kusema maneno hao kwa hayo kila siku kwamba hatutaki muungano wakati hutoi sababu wenzetu wana hoja zao na sisi tujitahidini kutafuta hoja za msingi ambazo zitachukuliwa wakati wa kukusanywa maoni ya katiba mpya. Tunataka Tanganyika na serikali yao na baraza lao na sisi zanzibar tuwe na serikali yetu na baraza letu na kiserikali kidogo kiwepo cha muungano, haya ndio mambo ya kujadili.
Imefika wakati kama hatuna maslahi katika muungano hatuna haja ya kuwa na muungano huu, tusiendelee kurudi nyuma tusonge mbele kwa nini wabunge waliopo kule bungeni kutoka zanzibar kama hawakubaliani na hoja wakatoka nje? Hata kama jambo litapita lakini dunia itafahamu kwamba katika hili wazanzibari wamekataa kunga mkono hii dunia sio ya kuogopa kitu kila kitu kiwekwe wazi. Tunaingia katika katiba tutafute mambo ambayo yanatulinda na kupata haki zetu.
Juma Khatib Ali
Tunaambia kwama article of union ina mambo yake ya msingi 11 lakini pia hayafai hebu tuyaangalie vyema mambo haya kama kuna mambo mengine ndio tuyaweke lakini sio tunaendelea nao hayo ambayo walikubaliana nao watu wawili tu.
Fadhil Khamis Fadhil
Muungano huu hautufai tokea tulipoungana hatuoni faida za muungano kwa nini hatunufaiki sisi kwa nini viongozi walisema muungano huu miaka 10 sasa kwa nini tunaendelea nao mpaka leo?
Mshenga
Tumeusaliti utaifa wetu vipi tutalitia meno taifa la Zanzibar ndio jambo la msingi lakini hili taifa halina uraia na hakuna taifa lisilo na uraia duniani.
Ipo haja ya Tanganyika na wazanzibari kurejeshewa mataifa yao, mimi siwafiki serikali tatu kwa sababu kuhusu serikali ngapi ni katiba za vyama na sisi hatuna vyama Zanzibar tuna serikali isiyokuwa na chama maana tuna serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa na CCM na CUF.
Jambo la kujiuliza kwa sasa kama kamati ya kukusanya maoni kuhusu katiba imeshakuja tutaongea nini? Katiba ioneshwe iwe na katiba tatu ili itoe utaifa kusaini mikataba ya kimataifa, urais, kujiunga na mikataba ya kimataifa na kuwe na ushirikiano katiba hii isiweze kudhoofisha utaifa wao wazanzibari na watanganyika, wazanzibari wanatakiwa kuonekana nje na kujiunga na mataifa mfano FIFA lakini sasa hawawezi.
Said Salim Said
Historia inaonesha kuwa muungano haukuwa na background mzuri, wazanzibari tumefikia hapa hatuna kitu hatuna uraia, hakuna passport hatuna chochote kwa hivyo katika hii katiba mpya tuiangalie inakuja vipi na kuwepo, na matumizi ya baraza la wawakilishi yatumike vizuri tumeona katika serikali ya umoja wa kitaifa imefanikiwa kwa sababu ya baraza la wawakilishi limefanya kazi vizuri kwa hivyo na hayo masuala mengine ya katiba na mengineyo kuwepo na suala la kuwatumia wawakilishi wetu maana hata serikali ya umoja wenzetu bara walikuwa hawataki lakini kwa kuwa wazanzibari tulikuwa tunataka tumeweza.
Khamis Khatib Khamis
Hatuna uhuru hapa Zanzibar muungano utaendelea kutufanyia haya mpaka milele ikiwa tutaendelea hivi hivi sisi tunayo haki ya kujiamulia mambo yetu tuwe na sauti ya kudai haki zetu lakini tatizo tunaogopa.
Kama tatizo ni katiba ya muungano kwanza ni lazima kujua nini maana ya muungano na kujua faida zake ni miaka 47 ya muungano sasa hakuna faida yoyote iliopatikana katika muungano na iwapo tokea watu kuungana ni lazima kuwepo na malengo yenye kuleta maslahi kuna mambo matatu ambayo yanayo sababisha kufikia katika hali hii tulio nao ambayo ni ubinafsi wa viongozi woga kusema kweli na hofu walio nayo viongozi wetu.
Ali Seif Salim
Wakati umefika sasa Zanzibar kusema tunataka katiba ya aina gani na ili kujua katiba gani inayotakiwa iwepo ni kusoma historia za viongozi kutoa matatizo yalioma ndani ya katiba hii ya muungano na kama haitakiwi katiba ya muungano kabisa nikukaa pamoja na kutoa sauti zetu na sababu ya kukataa katiba hiyo.
Azzan Khalid Hamdan (Naibu Amir wa UAMSHO)
Waziri Mizengo Pinda kasema viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi lakini sisi tutaendelea kuwaelimisha watu wetu kama anataka kuwakataza basi ni huko Tanganyika lakini sisi tutaendelea kwa sababu tulitoa ahadi pale bwawani kwamba tutandelea kuelimishana katika hilo huu ni wajibu wetu tumeshaufanya na tumesema kama huu wajibu wetu basi tunautimiza na kama kutumia maneno na kama kutumia nguvu tutatumia mpaka tupate nchi yetu.
Pinda amesema viongozi wa dini wasipotoshe watu huo ni ujinga wake tu lakini yeye hawezi kutuzuwia kwa lolote tutakalotaka sisi.
Mselem Ali (Amir wa UAMSHO)
Tunapoongea kudhalilishwa kwetu ndio maana tunadai haki yetu, tupo nyuma kiuchumi tulikuwa tukiheshimika ulimwengu mzima sasa tunataka kurejesha heshima ya nchi yetu na kurejesha heshima ya watu wake.
Nchi inapokuwa watu wake sio wazuri huitwa nchi hiyo sio nzuri. Mtume alianza kufanya mabadiliko kwa watu waliokithiri kwa rushwa, washirikina, ufisadi, Na Mtume alikuwa alifanikiwa kwa sababu alikuwa na vitu hivi vinne vision, mission, responsibility na assessment.
Mtume alikuwa ni kiongozi mwenye kujua kazi zake uteule wake kutoka kwa Mwenyeenzi Mungu alikuwa na limit katika masuala ya maamuzi aliambiwa awashauri watu wake katika maamuzi kwa hivyo alikuwa akishauriana na watu wake kwa kuwa alitakiwa ashauriane nao na hakuwa akijiamulia mwenyewe.
Sisi Zanzibar tuna wataalamu wa kila fani lakini bahati mbaya sisi ndio tunaongoza kwa ubovu na ujinga tuna kila nyenzo lakini tumekuwa hatuna chochote kwa sababu tumekosa kufuata mwenendo tunaotakiwa kuufuata.
Mtume aliambiwa kwenye maamuzi ya nchi asitumie ubabe. Mtume alipingwa sana na aliishi katika mazingira mabovu sana alikuwa na dipration kubwa tu lakini alikuwa na watu wenye fani wa kila kitu kwa hivyo alisaidiwa na Abubakar akawa anamtumia vizuri maana alikuwa mchumi, Abubakar Bin Affan alikuwa mtu mwenye elimu Mtume alimtumia sana katika kumshauri, Ali bin Abutalib alitumiwa kuwaongoza vijana hasa katika suala la maamuzi.
Kijana ukimtumia vizuri anatumika vyema, hapa kwetu vijana wanatumiwa vibaya na ndio maana hapa tunashuhudia wamealikwa vijana wengi tu wako wapi lakini kukifanyika katika maovu mbio wanakuja wenyewe bila ya kuitwa, hapa akiwemo mambo ya ngoma na mambo ya ukosefu wa adabu ndio utaona wanafika kwa wingi na wapo tayari hata kutoa fedha katika kulipia mambo ya kipuuzi kama ya kuchukua wanawake au kwenda katika muziki.
Sayyidna Omar bin khataab alitaka kumuua Mtume Muhammad (s.a.w) lakini ‘daaru narwa’ nyumba ya kutolewa maamuzi, Omar alikuwa anakwenda kudai haki, Omar alipokwenda na kukuta mambo vyenginevyo na akahakikisha mambo ni ya faida akaufahamu uislamu akaingia katika uislamu na alimuuliza Mtume wewe jee sio Mtume kweli? na haya maneno haya unayoongea sio ya Mwenyeezni Mungu? Mtume akasema mimi ni Mtume wa Mungu lakini kuhusu kwa nini wanafanya daawa kwa kujificha katika masuala muhimu Mtume akasema sisi ni wachache na ni dhaifu ndio maana tunajificha.
Hapo ndio Sayyidna Omar akachukua jukumu la kuhakikisha usalama na ulinzi kwa kuwa yeye alikuwa mtaalamu wa ulinzi na kuanzia hapo akamwambia Mtume atahakisha analishughulikia suala hilo kwa umakini na ndio kuanzia hapo dini ikaanza kutangazwa hadharani.
Ni kweli kwamba ukikosa elimu na uchumi ni tatizo. Omar akachukua dhamana kuanzia hapo alijipanga kwa sababu ya kuwa na elimu na hivyo akachukua dhamana hiyo nimetaka kutoa mfano huo ili na sisi tuone jinsi tulivyo katika maisha yetu kama tunaishi katika khofu tunahitaji ulinzi, tunahitaji kushirikiana pamoja vijana kwa vijana, watu wa dini na wenzao wa dini viongozi kwa viongozi lakini ilimradi watu waungane kwa pamoja katika kutetea heshima ya nchi yao

UMOJA NI GUVU UTENGANO NI THAIFU VIJANA WA Z;BAR TUUNGANE

No comments:

Post a Comment