Sunday, June 26, 2011

W;Z;BAR TULITHAN SMZ NI VIONGOZI KUMBE VIFUU TUUNDU

Mh Nahodha asingwa apate kuimaliza vizuri Z'bar ambiwa(Good boy).Kama kweli Wzanzibar tumezamiria kweli kweli kuwa huru ktk taifa letu la
watu wa Zanzibar, Basi kuvunja Muungano ni kitu cha sekunde tu. kwanza
Katika makubaliano ya Muungano hakuna kitu kulazimishana, na  Muungano
nimakubaliano ya pande mbili husika, ikiwa upande mmoja watu wake
watahisi hawataki tena Muungano basi hakuna chama wala kiongozi yoyote
anaweza kupinga mamuzi au matakwa ya wananchi wenyewe,
Na kwenda kinyume na mamuzi ya wananchi basi inamana ni U-dictator na
nikujichukulia jukumu na zima mbele ya M/Muungu. hivi sasa kiuhakika
Muungano hauna tena nafasi ya mapenzi na Wazanzibar na wanaoba kila leo
uvunjike na ubakie ujirani tu mwema kama vile Kenya na Unganda.
Hii nikutokana na vitimbi vya Muungano na udanyanyifu ulozidi  wa
Tanganyika ndio iliosababisha Wzanzibar kuukana hazarani na kuushukia,
hakuna shaka kuwa kero za Muungano zimekuwa nyingi na kutatulika nitabu
kwa vile tayari zamira halisi ya Muungano kwa upande wa Zanzibar
imeshaondoka.
Kwanza Wzanzibar waleo sio wale wakuburuzwa tu na kuvungwa vungwa,
zamira ya Muungano ni udugu,upendo ushirikiano na ummoja? jee hayo yapo
ktk mfumo huu tulio nao wa Muungano? Muungano ulikuwa ni kati ya watu
wawili yani Tanganyika na Zanzibar? leo tumeletewa mtu mpya from no
where? ana-act kama Tanganyika na Tanganyika ambayo ndio mshirika wa
Muungano tunambiwa imekufa ktk Tumbo la Tanzania ndio inachukuwa nafasi
yake.
Huu ni utapeli tena mbaya na nihatari kwa Zanzibar kumezwa ktk mdomo wa
Tanzania, halafu wenzetu kujifanya eti wana akili nyingi ni kumchukuwa
Rais  watu wa Zanzibar kumfanya Waziri asio na wizara malum?  Sasa kwa
mtazamo wa viongozi wetu wa SMZ jee sifa ya Muungano au kiungo cha
Muungano kikowapi hapo kinacho waunganisha Wzanzibar kusema bado wamo
ktk Muungano ikiwa Rais alopigiwa kura na Watu wa Zanzibar leo ni Waziri
asio na wizara?.
Hii ni viongozi wetu kutupunza na kuipeleka kubaya nchi yatu kutokana na
matamanio yao binafsi, lakini wasi sahau kila kiongozi atahukumiwa kwa
athari alizo watia Wazanzibar, hivi sasa kutokana na unafiki wa viongozi
wetu kuona kuwa Tanganyika wana vutwa na Wazanzibar wana wavuta ndio
unawaona hasa ule unafiki wao wa double face unajitokeza.
Utaona viongozi wa SMZ husema Muungano una tunyonyo, Tanganyika ina
tuzulumu, sijuwi Zanzibar ni nchi mafuta sia Muungano nyoko nyoko nyingi
lakini wao ndio wanafiki wakubwa na kikwazo kwa Wzanzibar kujinasua ktk
minyororo ya Mkoloni mweusi Tanganyika.
Kama kweli Muungano una inyonyo Zanzibar kukuwa kiuchumi na kimaendeleo
basi njia ni rahisi tu, nikusema katika Baraza la uwakilishi kuwa mchezo
basi,tuangalie Tanzania haito fufuka kwa jina lake Tanganyika na tuone
wataendelea kututawala kinguvu au itakuwa ndio mwisha wa Kero na
Matatizo ya Muungano.
Lakini viongozi wetu ndio wanaotubebesha mzigo na wao kubebe jukumu
mbele ya Allah, maana utaskia kiongozi husema matatizo na kero za
Muungano kila siku zinazidi kuiminya Zanzibar lakini ukweli halisi
mwisho ya hayo husema tuulinde Muungano na tuuenzi abooo.
Vipi tulinde kitu kilichokuwa hakiko? kama tumeungana na Tanganyika,
Tanganyika imeshakufa na haitajwi tena, sasa na sisi Zanzibar tuiuwe tuwe
na Nchi mmoja? jee kero za Muungano zitapungua au zitazidi tukisha uwa
Utaifa wa Zanzibar?.
wake up SMZ siasa munayo nyinyi Tanganyika wao wako ktk kukuza uchumi
wao nyinyi hutumiliwa siasa kuwa ndio kitanzi chakuisarenda Zanzibar na
rasilimali zake, iteni kura ya maoni kuwauliza Wzanzibar hatama ya nchi
yao sio muchukuwe majukumu makubwa musio weza kujibu mbele ya haki.
Kama mumeshindwa viongozi au munawaonelea vibaya Tanganyika basi wao
hawawaonaeni vibaya wala huruma lao moja na nikuimeza Zanzibar ishara na
athari nyingi ziko wazi kuwa wenzetu hawakutaka Muungano kwa heri,
wasingali iuwa Tanganyika na Wakavaa koti la Ubaba Tanzania nikuliwaa
akili SMZ na kutubebesha mzigo mzito Zanzibar.
Kama mumesha owa au kujenga bara basi hizo zote sio sababu za
kujibebesha jukumu la Wzanzibar ktk hatma ya nchi yao, mutakuwa na lipi
mbele ya Allah la kumueleza? hamujuwi kuviuza visiwa ni sawa na
kuchukuwa mali ya mayatima na kuwapa wasio husika kurithi..?
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote

No comments:

Post a Comment