Thursday, June 30, 2011

Z;BAR IMEFUNGUWA MILANGO KWA WAZBAR WALIOPO NJE YA NCHI KUJA NCHINI Z;BAR


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefunguwa milango wazi kwa Wazanzibar waliopo nje ya nchi kuja nchini na kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa nchi na kuleta maendeleo zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2011-2012 hapo katika baraza la wawakilishi.
Dk Mwinyihaji alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambuwa mchango mkubwa wa wananchi hao katika kusaidia na kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo imeanzisha idara ya kuratibu maendeleo ya wazanzibari walipo nje inayojulikana kwa jina la Diaspora.
Alisema Idara ya Ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa shughuli za Wazanzibari waliopo nchi za nje (DIASPORA) tayari imeandaliwa mipango ya kuwashirikisha wataalamu mbali mbali katika mikutano ya kikanda ikiwemo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mjadala wa soko la sarafu.
Aidha Idara hiyo pia imeanza utaratibu wa kukutana na wazanzibari walionje ya nchi ikiwemo Uingereza na kuwataka kuwa tayari kushirikiana na serikali ya Zanzibar kwa kutoa michango yao baada ya kuandaliwa kwa mpango na sera inayowashirikisha na serikali yao.
Dk Mwinyihaji alisema mazingira ya kisiasa yaliopo sasa ni mazuri,ambapo Zanzibar ipo chini ya mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa iliyowashiriikisha wanan chi wote kufanya kazi.
Aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba serikali tayari imeanza kufanya mawasiliano na wazanzibari waliopo nje kuja na kushirikiana na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nchi.
Alisema mafanikio hayo yameanza kuzaa matunda ambapo wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kushirikiana na umoja wa wazanzibari waliopo Uingereza kufanya mkutano mkubwa ambao ulikuwa na lengo la kuwakutanisha na kutambuwa Mchango wa Watanzania walio nje ya nchi.
“Mkutano ule ulikuwa na manufaa makubwa ambapo ulihudhuriwa na waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe…..watendaji wetu kutoka SMZ walihudhuria na mambo mengi yalizungumzwa kwa faida ya Zanzibar ikiwemo kuitangaza Zanzibar”alisema Mwinyihaji.
Alisema tangu kufanyika kwa mkutano huo yamekuwepo mafanikio makubwa kwa baadhi ya wananchi wazanzibari waliopo nje kuonesha nia ya kuja nchini na wengine kusaidia shunguli mbali mbali za ujenzi wa taifa.
Mwinyihaji aliliambiya baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashirikishwa kikamilifu katika mikutano mbali mbali ya kimataifa na kanda ikiwemo taasisi za kimataifa.
Kwa mfano Mwinyihaji alisema kwamba Zanzibar itanufaika kwa kiasi kikubwa kufuatia kuanzishwa kwa eneo huru la biashara la utatu COMESA pamoja na Jumuiya ya Afrika ya mashariki pamoja na SADC.
Alisema eneo la soko hilo ni muhimu sana likiwa na nchi wanachama zipatazo 26 likiwa na idadi ya watu Milioni 600 na wastani wa pato la taifa linalofikiya dola za kimarekani Trilioni moja.
Mwinyihaji alisema kuanzishwa kwa soko huru la utatu utakuza biashara na kuongeza uwekezaji katika viwanda na kukuza miundo mbinu katika nchi wanachama wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“Mheshimiwa hili eneo la biashara la utatu ni muhimu sana tukilitumia vizuri basi yapo manufaa makubwa ya kuimarika kiuchumi na biashara” alisema waziri huyo.
Aidha aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashiriki kikamilifu katika vikao vyote vya jumuiya ya Afrika ya mashariki,ambapo watendaji wake wamekuwa wakishiriki katika mikutano ya matayarisho la baraza la mawaziri na wakuu wa nchi.
Mwinyihaji aliliomba baraza la wawakilishi kuidhinisha jumla ya sh.33,127,.2 Milioni ambapo kati ya hizo jumla ya sh.29,386.2 kwa ajili ya kazi za kawaida na jumla ya sh.1,930.0 kwa kazi za maendeleo katika mwaka 2011-2012.

TANGANYIKA NDIO WENYE JESHI Z;BAR NA SILAHA-WAZ;BAR HATUNA KITU YAKITOKEYA YAKOTOKEYA HAYAWAPATI NYINYI NI VIONGOZI HUTUPATA SISI NA DUNGU ZETU WALIO KIMBIA MUSITULETE UBABAIFU

 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini namnuku alivyo sema(zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.)unasema kweli au unataniya watu wewe..?juzi juzi hapa kulikuwa na mabala ya mswaada na mpaka tukauchana na kutiya moto na mpaka leo bado tunamivutano.kisha unasema kama hivi unamanisha nini..? sio kama sitaki dungu zetu warudi kwao laa hasha ila vipi utawarudisha hapa na watu ndio kwanza tunapigania uhuru maana z;bar haiko huru bado tunatawaliwa na mkoloni mweusi nawashasema 2014 katiba mpya inakuja tukitaka tusitake ndio katiba na znz nzima hatutaki muungano.kama wewe na seif munataka wazenji warudi vunjeni muungano kisha nyamazeni kimya muona kama denge hazikutuwa kila leo ila mchezo huu hatutaki watu wakati wa ali hassan mwinyi alipokuwa raisi wa muda znz alisema hivyo hivyo znz ni jemaa atakae aje kisha akakimbiliya dar wakatuekeya salmin amour akatunywisha maji kikuku watu wakakimbia wengine wakaishi mombasa shimoni kenya hapo sasa munataka tena sio mchezo wenu huu mara hii sithani dungu zetu waliyokuwepo nje watakuwa wajinga kiasi hichi mpaka muungano uvunjwe hapo utaona.

No comments:

Post a Comment