Friday, July 22, 2011

ASKOFU AMTOWA BINTI MAPEPO....ATWAMBIYA NI BINTI YAKE WA KIROHO


PICHA zinazomuonesha mtu aliyedaiwa kuwa ni Askofu wa Kanisa la Apostle Majani la Namanga Tegeta, Dar es Salaam,Askofu akiwa kitandani na denti wa sekondari aliyetajwa kwa jina moja la Basilisa, zimenaswa.Kwa mujibu wa chanzo makini, picha hizo zenye ladha ya ‘mambo ya kikubwa’, zilianza kuzagaa kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo siku chache baada ya mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza kutolewa mapepo na Askofu huyu.Chanzo hicho kilipepeta umbeya kwamba, mara tu baada ya denti huyo kutolewa mapepo, Askofu  alimchukua na kuishi naye nyumbani kwake maeneo hayo huku kukiwa na madai kuwa, alikuwa amemhamishia mkewe kwenye makazi yake mapya huko Kibamba, Dar.
Baada ya kuzitia ‘foto’ hizo kibindoni,Tulizungumza na Askofu ambapo
mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
FREE-ZNZ- Haloo, nazungumza na Baba Askofu wa Kanisa la Apostle Majani?
Askofu : Naam, mimi ndiye Baba Askofu, nani mwenzangu?
FREE ZNZ: Mimi ni mwandishi wa Blog.

Askofu: Naam. Bwana Yesu asifiwe ndugu mwandishi, una habari gani?
FREE ZNZ: Kuna picha zako ukiwa kitandani na mwanafunzi anayeitwa Basilisa, hili ni tukio gani Baba Askofu?
Askofu: Basilisa ni binti yangu wa kiroho, nilimchukua na tulikuwa tunaishi naye na familia yangu hapa nyumbani. Hizo picha tulikuwa tunahama, baada ya kutoa vitu ndani nikawa nimepumzika kitandani, Basilisa akawa amenilalia, dada mmoja akapiga picha nikaona wakizihamishia kwenye simu zao.
FREE ZNZ: Mbona zina mapozi ya kimahaba?
Askofu: Najua watu wananichafua lakini Mungu atanisafisha, hata mke wangu anamfahamu kabisa Basilisa na kwa kweli ni binti yetu wa kiroho.
Hata hivyo, Askofu  alipangua maswali ya mwandishi na kugomea hapo.

No comments:

Post a Comment