Wednesday, July 20, 2011

DR SHEIN ASEMA....................NDANI YA LONDON U.K.


Imeelezwa kwamba kuwapo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni jambo lilotakiwa na kupangwa makusudi. Na Serikali hiyo ndio iliyoonekana kuweza kumaliza uhasama na malumbano ya kisiasa ndani ya Visiwa hivyo.Baraza la Wawakilishi lilifanya mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar na kutunga sharia ya kuwapo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa kwa lengo la kumaliza uhasama, kupatikana kwa amani ya kudumu na kujenga hali ya maridhiano.Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchi Uingereza (ZAWA) mwishoni mwa wiki iliyopita mjini London.“Kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa, halikuwa jambo la kukurupuka na kulazimisha, hapana; ni jambo lililopangwa na kutakiwa na ndio sababu iliyotufanya tuamuwe kuwapo kwa Serikali hii”. Dk Shein alisema na kuongeza kwamba yeye na makamo wake wote wawili wameshikana kabisa kwa kufanyakazi wote wakiwa timu moja.
Kwa mujibu wa Dk Shein, viongozi hao watatu wanafanyakazi kwa pamoja “team work”, masaa 24 wakiwa maofisini na hata kutembeleana majumbani na kuwa na uhusiano wa kirafiki ingawa ulikuwapo tangu zamani. Dk Shein aliwaambia viongozi hao.Kiongozi huyo mwenye shahada ya PhD katika fani ya “Clinical Biochemistry and Metabolic Medicine”, aliwaambia viongozi hao wa ZAWA kuwa kuandaliwa na kupangwa mapema kwa Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kwa kuingizwa ndani ya Katiba na sharia za nchi kumenusuru kukumbana na matatizo ya uongozi yaliyojitokeza kwa Serikali za Kenya na Zimbabwe.Rais huyo wa Serikali ya Zanzibar iliyochini ya umoja wa kitaifa, alizidi kueleza kuwa baada ya chama chake kupata ushindi na kuapishwa Novemba 3, 2010 kilichofuata alimteuwa Maalim Seif baada ya kupokea jina hilo kutoka chama chake cha CUF.Dk Shein ambaye ameondoka nchini hapa leo kurejea nyumba alisisitiza kwamba uundwaji wa Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kuanzia ngazi ya mawazi, manaibu mawaziri na ngazi nyengine zilizofuata viongozi wote wameteuliwa kwa mashauriano na makamo wake wote wawili.Rais huyo wa SMZ-SUK, alisema kwamba viongozi wa Serikali hiyo na hasa mawaziri na manaibu mawaziri wanafanyakazi bila kujibainisha wanatoka vyama gani. “Tumepania mpaka 2014 tuwe tumeirejesha Zanzibar ile tunayoikumbuka na tunayoipenda”, alisema.Novemba 5, 2009 Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume walikutana kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika Ikulu ya Zanzibar na kuwa na mazungumzo yaliyozaa maridhiano. Chanzo cha mazungumzo ya viongozi hao ndio yaliyochochea kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar

No comments:

Post a Comment