Friday, July 22, 2011

JUSSA AUVUMBUWA UKIRITIBWA UNAO FANYA KTK MUUNGANO FEKI KUHUSU LESENI ZA UVUVI WA BAHARI KUU

MWAKILISHI wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu ameibua tuhuma nzito juu ya Zanzibar kukoseshwa haki yake katika Muungano ya mapato yatokanayo na leseni za uvuvi wa bahari kuu.Mwakilishi huyo aliibua hoja hiyo jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha 2011/2012 iliyowasilisha na waziri wa wizara hiyo Said Ali Mbarouk.Jussa alimtaka waziri huyo kuliangalia vyema suala la fedha za leseni katika bahari kuu kwani Zanzibar inakoseshwa mapato yake na hawaoni kama serikali ya Muungano ina nia ya kushirikiana na SMZ juu ya mapato ya mgawano wa fedha zinazokusanywa katika uvuvi wa bahari kuu.Alisema sheria  yamakubaliano juu ya mgawano wa mapato ya uvuvi wa bahari kuu yanataka Zanzibar kupewa asilimia 40 na bara asilimia 60 lakini hali iliyopo ni kwamba hiyo asilimia 40 Zanzibar haipewi.
Akifafanua kauli yake alisema katika kikao cha mwezi Juni 15, 2011, Naibu Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo wa Tanzania, Benedict Ole Nangoro, akijibu Mbunge wa viti
maalum Thuwaiba Idrisa Muhammed ambaye alitaka kujua kiasi gani na Zanzibar
imeweza kufaidika na fedha za magao wa lesini za bahari kuu ambapo Naibu huyo
alijibu fedha walizokusanywa na sio mgao wa Zanzibar Alisema Naibu huyo aliliambia Bunge hilo kuwa kwa mwaka 2010/ 2011, meli ambazo zilivua baada ya kupatiwa leseni zilikuwa ni 71 na mapato yaliopatikana yalikuwa dola za kimarekani 2,074,000.Alisema inasikitisha kuona mapato ya Zanzibar katika suala hilo imekuwa haipatiwi huku serikali ikiwa inatoa mchango wake wa kujenga jengo la Makao
Makuu ya uvuvi wa bahari kuu huko Fumba.Mwakilishi huyo anayechachafya Barazani alisema ipo haja ya wizara hiyo kuanza kufanya uchunguzi kwa kutafuta ni kwanini mgao uliotakiwa kupatikana kwa uvuvi
wa bahari kuu mapato hayakufikishwa Zanzibar.Alisema ni lazima serikali iliangalie hilo kwa vile Waziri wa wizara hiyo amekuwa akilalamikia ukosefu wa fedha kwa ajili ya utoaji wa huduma za baadhi ya
ofisi kuwa na mchango mdogo huku kukiwa na fedha ambazo zingeweza kusaidia
kukabiliana na changamoto za wizara hiyo.Alisema tatizo hilo ni muendelezo wa vitendo vya serikali ya Muungano katika mambo ya mgawano wa mapato jambo ambalo hapo awali lilielezwa kuwa limeshapata
ufumbuzi katika vikao vya kero za Muungano.Kwa upande wake Mwakilishi wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo, alisema ipo haja kwa wizara hiyo kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwapatia vifaa vya kisasa wavuvi wa eneo ili kazi yao hiyo iweze kuwafaidisha kimapato.Nae Mwakilishi wa Kojani Hassan Hamad Omar, alisema ipo haja ya serikali kuliangalia suala la baadhi ya wavuvi wanaoenda kuvua Tanzania bara kutozeshwa kodi ya leseni ya shilingi 20,000 wakati wanaotoka bara kuja Zanzibar hawatozwi
fedha hizo.Mwakilishi wa Mkoani Abdalla Mohammed Ali, akitoa mchango wake alisema ipo haja
kwa serikali ikaona inaimarisha sekta ya mifugo kwa kuwapatia wafugaji ng’ombe
wa kisasa kwa mkopo kwani baadhi ya wafugaji hawana uwezo wa kununua mifugo
hiyo.Mwakilishi wa Jimbo la Amaan, Fatma Mbarouk Said, alisema ipo haja kwa serikali
ikawaangalia vijana ambao hivi sasa wanajishughulisha na ajira za Punda na
ng’ombe kwa kuwapatia kazi ikiwa ni hatua itayowawezesha kuacha kuwatumia
wanyama hao vibaya.

No comments:

Post a Comment