Friday, July 22, 2011

MAFUMANIZI NCHINI TANGANYIKA YASHIKA KASI KWELI KWELI HAHAHA


ALIYESHIKA PANGA NI MUME WA MWANAMKE UNAE MUONA KAFUMANIWA NA MWANA MUME MWENGINE NI BALAAAAAAAAA NI BALAAAAAAAAAAAAAAA
                                                         


Ile skendo ya Aibu Bosi wa Bandari, Leslie Milanzi kukutwa gesti na mke wa mtu imeingia sehemu ya pili baada ya mume orijino wa mwanamke huyo kuibuka na kuanika kila kitu ikionekana na yeye amefumania, Ijumaa Wikienda linashuka na ripoti kamili.Mwanaume huyo (jina tunalo) alitinga kwenye ofisi za gazeti hili, Jumamosi ya Desemba 11, mwaka huu na kudai yeye ndiye mume halali wa mwanamke huyo aitwaye Salia, akisisitiza kuwa ndugu wa pande zote wanajua.Alisema kwamba, alikuwa nje ya Tanzania gazeti lilipotoka, lakini alipigiwa simu na mtu wake wa karibu na kumpa taarifa hizo ambazo hata hivyo, aliweka wazi kuwa hakuziamini.
“Mimi nilikuwa nje ya nchi, nikapata simu kutoka kwa mtu akiniambia mke wangu yupo ukurasa wa mbele wa gazeti. Sikuamini lakini pia sikuwa na papara,” alisema kwa sauti ya utulivu mwanaume huyo.Aliendelea kuweka wazi kuwa, alirejea nchini. Desemba 10, mwaka huu na kesho yake, Desemba 11, akaona bora atie timu kwenye ofisi za Ijumaa Wikienda, Bamaga Mwenge ili kupata ufafanuzi wa kilichotokea mpaka mke wake akaanikwa ukurasa wa mbele wa gazeti.Alipotakiwa kutoa maelezo aliyoongea mkewe mara baada ya kurejea nchini na kumuuliza kuhusu sakata hilo, mume huyo alisema:“Yeye amekataa katakata. Tena amesema hiyo siku ya Desemba Mosi, muda mliodai alikuwa gesti, yeye alikuwa kazini na mabosi wake huwa hawaruhusu mtu kutoka kabla ya muda wa kazi.”Akaendelea: “Halafu hata nywele alivyozitengeneza siku hiyo (Desemba Mosi) siyo za kwenye picha iliyotoka gazetini.”
Kingine alichokitolea ufafanuzi mwanaume huyo ni jina ambapo alisema kuwa, mkewe haitwi Salia ingawa hakupenda kuweka wazi jina halisi. Mume huyo alikwenda mbali zaidi akiamuru kuoneshwa ‘evidensi’ (picha nyingine) ambazo zitamridhisha kuwa, kweli mtuhumiwa ni mkewe, akidhani kwamba, huenda amefananishwa na mwanamke mwingine.Baada ya kutakiwa na uongozi wa gazeti kutoa ushahidi kwamba, yeye ndiye mume halali wa mwanamke huyo, alizungushwa nyuma ya Kompyuta na kufunguliwa picha moja baada ya nyingine za tukio hilo. Ilifika mahali, mume huyo alijiridhisha kuwa, mwanamke aliyekuwa akimwona katika picha hizo ni mkewe.“Ni yeye kweli! Ni yeye! Sasa na huyo Shaha (mwanaume aliyedai kufumania awali) ameibukia wapi jamani?” Alihoji katika hali ya mshangao.Mwishowe, mume huyo aliondoka akisema atakwenda kuongea kifamilia na mkewe huku akisita kuweka wazi uamuzi atakaoutoa.Katika toleo la gazeti hili namba 187 la Desemba 6, mwaka huu ukurasa wa mbele iliandikwa habari yenye kichwa kilichosomeka; Aibu Bosi wa Bandari.
Katika habari hiyo, karani mmoja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Leslie Milanzi alidaiwa kufumaniwa katika gesti moja iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam akiwa na mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Salia.
Chanzo cha habari kilisema kuwa, Salia na Milanzi walikutwa ndani ya chumba hicho na mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha ambaye alidai ndiye mume wa mwanamke huyo.Shaha alisema kuwa, aliwafuatilia kwa siku nyingi wawili hao sanjari na kumpa onyo mwanaume huyo kuacha kutembea na mkewe.Siku ya tukio, Milanzi alijitetea kwa kusema kuwa, toka wameanza uhusiano wa kimapenzi, Salia hakuwahi kumwambia ameolewa hivyo kwa upande wake alichukulia kitendo kile cha fumanizi kama uonevu.
Kwa upande wake, siku hiyo hiyo ya tukio, Shaha alipotakiwa kuongea ili kuweka sawa habari hiyo, alikiri Salia ni mkewe huku akisisitiza kuwa, ameshampigia simu mara kadhaa, Milanzi akimwonya kuachana na mkewe lakini hakutaka kusikia.

No comments:

Post a Comment