Thursday, July 14, 2011

MAFUTA YA Z;BAR YANAWATOWA ROHO WATANGANYIKA KILA KUKICHA

Hivi sasa Viongozi wa Tanganyika wanafanya kila hila lakini mafuta ya Zanzibar yabakie kuwa ni mali ya Muungano huku gus ya songo songo na mineral nyingine za Tanganyika zibakie kuwa za Tanganyika kutokana na kisingizio cha mafuta ya Zanzibar yamo kwenye Muungano hata kama yalingizwa kimakosa.
Hii ni yale maswala ya mivutano ktk kutatua kero za Muungano kwa kuingiza mambo kutoka 11 mpaka 22 bila ya kukaa pande mbili za Muungano kujadili mambo yaliomo ktk (Article of Unio) nimangapi.
Kwa nini wenzetu wanakuwa wazito kuondosha mambo yenye utata ktk Kero za Muungano ili kuimirisha Muungano wenyewe? jawabu la hili nikuwa wenzetu hawakuwa na nia safi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ispokuwa ni kujifanya wajanja wa kunyakuwa rasilimali za Zanzibar na kuitawala Zanzibar kwa kutumia upepo wa sera za chama tawala na itikadi za chama.Tunawaomba viongozi wetu wa SMZ hususan CCM/SMZ  waache tafauti za chama na wajali maslahi ya ndugu zao na watoto wao wazanzibar ili kulinusuru taifa la watu wa Zanzibar lisiagamia ktk jinamizi la Sera na itikadi za chama ambazo ndio zenye kulinda Muungano Zanzibar hivi sasa. Zanzibar hivi sasa inahitaji Wazanzibar wenyewe wazalendo na wenye mshikamano wa kuokowa Zanzibar yetu tuipendayo na kizazi chetu cha badae kukijengea mazingira mazuri na kuwachia urithi endelezi kwa vijukuu vyao vya badae.Hii wanayo tufanyia wenzetu sio haki na sio udugu wa Muungano hii nikuuwa Muungano kutokana na Zanzibar nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo kubebeshwa mzigo mkubwa na kila siku bada ya kupungua kero za Muungano basi zinazidi kukuwa tunatoka katika Bad na kwenda katika Warst.Mimi sioni sababu kwa jinchi kubwa la Tanganyika lenye uchumi mkubwa na ardhi kubwa yenye watu millioni 44 kungagania uchumi mdogo wa Zanzibar kama vile Bandari na ukushanyaji wa mapato ya Zanzibar, hii ni choyo tu na roho mbaya ambayo wenzetu wanayo.
Kama kweli walikuwa na nia safi ya kuendeleza Muungano udumu na kuimarika ilikuwa wenzetu waisaidie Zanzibar kimaendeleo na kiuchumi sio wafanye ujanja ujanja wa kuibana koo Zanzibar isikuwe kiuchumi na kimaendeleo hichi ni choyo na husda, kama sio hivyo basi wasingali uwa Bandari ya Zanzibar ambayo ndio uti wa mgongo wa Wzanzibar.Tunawaoba Wawakilishi wetu na Baraza lake ambalo ndio Bunge la Zanzibar na sauti ya Wanyonge Zanzibar wache tafauti zao na panapokuja swala la haki za Zanzibar kuwa kitu kimoja na kulinda rasilimali za zanzibar.Hivi sasa Tanganyika wanafaidika kwa menaral Zao na Zanzibar hawafaidiki chochote na mineral hizo sasa vipi leo tukubali ku-sacryfy rasilimali zetu na power ya nchi yetu kwa jinamizi la Tanganyika yenye kuvaa Koti la Tanzania?.Vipi tuendelee kukumbatia bomu lililokwishwa tolewa fuse, hivi sasa Tanganyika inaomba misada mingi tu kwa jina la Tanzania, zanzibar ikifanya hivyo huombiwa wanaingilia mambo ya Muungano swala la mambo ya kigeni ni la Muungano? mbona wao huomba misada kwa jina la Tanzania lakini ikifika nchini hutumika kwa jina la Tanganyika? sio misada yote Zanzibar hupewa %4.5, kuna misada mingi tu huombwa kwa jina la Tanzania lakini Zanzibar haiambukii kitu.Sasa kusema Samuel sita kuwa Serekali 3 sio solution au kurudi kwa Tanganyika kutaleta ushindani hii mimi nasema sio kweli na ni unafiki na roho mbaya tu yakuzani bado viongozi wa SMZ niwatu wa kuburuzwa na kuwaburuza Wzanzibar,tunasema Generatio hio haipo tena hivi sasa, tutazisimamia haki zetu zote kikamilifu.Jee hafahamu sita kuwa Zanzibar imeungana na Tanganyika? vipi leo aseme Tanganyika ikija itakera, hii nikuonyecha kuwa Muungano ni jindamizi la ujanja wa kuitawala Zanzibar ki-imla kwa hio wajibu wa Viongozi wetu na Wazanzibar kwa jumla nikusimama kidete na kutetea ardhi yetu kwa vizazi vyetu vya baadae.Mimi nasema kama viongozi wa Tanganyika watakaataa mfumo wa Serekali tatu basi kuendelea na Muungano SMZ nikujizonga na itafika hadi tutashindwa kujizongowa.
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote popote pale walipo.

No comments:

Post a Comment