Thursday, July 21, 2011

MANSOUR YUSSUF HIMID JASIRI WA ZANZIBAR ANAYE TETEA HAKI NA UHURU WA Z;BARWAKATI huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapokabiliwa na mtihani mgumu wa kurejesha imani kwa wananchi kupitia kaulimbiu yake ya “kujivua gamba,” siamini kama kina nafasi ya kumjadili Mansour Yussuf Himid.na hata kikimjadili kwa hapa zenji basi wakipinga tutajuwa kuwa hao ndio wanafiki ila kama ni bara CCM haiwahusu wao maana huyu ni waziri wa z;bar sio morogoro wala mbeya wala moshi.
Mansour ni waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoendeshwa kwa ushirika kati ya chama hichi cha  CCM  na Chama cha Wananchi (CUF) Ni mwanasiasa kijana huyu ambaye amekuwa akiimarisha rekodi yake ya utendaji wa moyo wa kizalendo juu ya Zanzibar , nchi mama yetu ya Z;bar.
Tangu alipokuwa chini ya Amani Abeid Karume (2000-2010), Mansour alionyesha kupenda sana nchi yake. Aliitetea kila palipohitajika nchi hii ya zanzibar.Alijitahidi kujieleza kwa hisia kila alipohojiwa kwa jambo hili au lile lililokuwa mamlakani mwake tangu akiwa Waziri wa Nchi, Maji, Nishati, Ardhi na Mazingira chini ya Burhan Haji Saadat 2000-2005.Alipopandishwa hadhi kuwa waziri kamili baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, Mansour siyo tu aliongeza kasi ya utendaji kazi kizalendo,Itakumbukwa hiki kilikuwa ni kipindi cha Karume kutafuta hatima yake na ya kutafuta maridhiano na Maalim Seif Shariff Hamad.
Hiki kilikuwa kitendawili kikubwa isivyo kawaida kwa Wazanzibari. Hakuna aliyegundua haraka mipango ile. Hata pale ilipotangazwa rasmi kuwa Karume alikutana na Maalim Seif Novemba 5, 2009 Ikulu kuu ya Zanzibar , watu bado walijiuliza nini hasa kinachopangwa.Mansour alijua kila kitu. Najua alijua kila kitu. Niliwahi kusimuliwa kauli zake wakati akisimamia maagizo ya rais kuhusu mipango ya maridhiano. Alikuwa jasiri hasa na namsifu kwa hili la kuhifadhi siri ile mpaka ilipolazimu kuanikwa.Hatua zile zilienda sambamba na mipango ya kuhakikisha sekta ya mafuta na gesi asilimia inachomolewa kutoka mambo ya kusimamiwa kimuungano mansour huyu huyu mjasiri aliyepigania hayo.Ni Mansour aliyeongoza kampeni ndani ya serikali na Baraza la Wawakilishi. Yeye ndiye alikuwa waziri mhusika wa wizara inayohusu nishati.
Alikuwa kinara wa kuliambia Baraza kuwa serikali inataka kuweka mazingira ya kisiasa na kisheria kuwezesha kusimamia yenyewe utafiti na uvunaji wa raslimali hiyo ili Zanzibar inufaike moja kwa moja na raslimali hiyo iliyothibitishwa kuwepo katika ardhi ya Zanzibar .Aliibeba dhamira hiyo hadi barazani. Alitoa hoja za serikali na akaahidi kuhakikisha utekelezaji wa yaliyoazimiwa na Baraza.Ni Mansour aliyeahidi wananchi wa Zanzibar kupitia baraza lao kwamba kwa kuwa serikali imeshaamua na baraza limeidhinisha kwa kutoa azimio, hakuna kurudi nyuma.Wakati akisimamia hili, alikuwa akitoa kauli nzito kwa Serikali ya Muungano bali pia akiashiria kutohofia chochote kwa chama – CCM ya huko bara ama hapa ndio tunavyotaka viongozi jasiri kama hawa ktk cha cha CCM na CUF pia ili z;bar inuke kiuchumi na kurudi ktk hathi yake na kuwa nchi kamili.basi. Akapita vizuri na kukamilisha yale yaliyowezekana kabla ya uchaguzi. Akashinda tena uwakilishi Kiembesamaki; akabahatika kurudi waziri.Mansour sasa ni waziri anayehusika na Kilimo na Maliasili ambako pamoja na kuwa suala la nishati haliko moja kwa moja kwenye utawala wake, anajivunia kuweza kulizungumzia kwa kuwa nayo ni maliasili ya nchi.Si hivyo tu; katika nafasi yake ya uwakilishi jimboni, ana haki ya kutoa maoni yake (yakichukuliwa ni maoni ya wanajimbo), kunapokuwa na mjadala unaolenga maliasili za nchi.Kwa hivyo basi, kwa muda wote huo Mansour akiwa serikalini – hapo kabla alikuwa katika sekta binafsi – amekuwa muwazi kusema kile anachokiamini.Na katika kutumia haki yake hiyo ya kikatiba na kama kiongozi, anatoa kauli zenye sauti bila ya kujali kama kuna watu watakasirika. Kumbuka nilitangulia kusema huyu ni jasiri – haogopi mtu yoyote.Ni Mansour aliyechagiza muswada wa marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ufutwe maana Zanzibar haijashirikishwa katika kuandaliwa kwa muswada sasa hawa makada wapumbavu wahajuwi lolote wanataka kutia midomo sisi tunakujuweni nyinyi ndio watoto wa wale walio uwa 1964 sasa munataka yale yatoke tena mara hii ili mufanye tena mara hii nyote mutaishia jela.Kwanza alisema kitendo cha kamati kuwaita wananchi kutoa maoni kuhusu muswada, ni sawa na kuwadanganya maana vipi watowe maoni na sio katiba yao..? vipi watowe maoni wakati tanganyika haipo..? je wakitowa maoni yao kuwa muungano uvunje mutavunja..?, halafu akaapa kuwa “Wazanzibari tutapinga muswada iwe katika Baraza la Mapinduzi, hadharani au katika kikao cha faragha.”na hii ndio dimokrasia sio asemalo kiongozi hawala huo ni udikteta.Ni kauli zile nzito zikiwemo za mawaziri wenzake kadhaa, zilizolazimisha uongozi wa serikali Bara kutia kwapani muswada na hatimaye kuuondoa katika mjadala bungeni.Mansour ameibuka tena. Akichangia hoja ya makadirio ya matumizi ya wizara ya Ardhi, Maji, Makazi na Nishati,amasema kweli kuwa huu sio mfumo mzuri wa serikali mbili na kupendelea wa serikali tatu – sera ya CUF na sidhani ni kitu kibaya maana sasa tuna serekali ya umoja wa kimataifa sasa kunaubaya gani akifuata sera ya CUF na sasa z;bar hakuna tena CUF wala CCM kuna wazenji basi.Katika kauli iliyochangamsha baraza na kujikuta akishangiliwa na wajumbe wa CUF, Mansour alisema:“Hapa mpango wa serikali moja hatutaki kuusikia maana anajuwa ikiwa serekali moja inamaana z;bar imekwisha hakuna tena z;bar ni hiyo ndio plani ya watanganyikaaa kwa kutumiya vibara wenye njaa baraza la wawakilishi na hao makada wazenji tuwe makini kabisa. Mfumo huu butu wa serikali mbili, sasa basi, (busara) twende kwa jambo ambalo kila mmoja wetu analizungumza la serikali tatu na mengineyo.”Sasa anaonekana msaliti wa sera za chama chake. Wanaojitambulisha kama makada siwakapinge kanda huko bara wacheze wasitulete ubathirifu z;bar wanampangia zengwe. Utaratibu uleule wa kishetani wa kutunga vipeperushi wamefanya ili  kumsakama.Makada hao wanamwambia: “Wewe ni Mjumbe wa NEC-CCM; Mjumbe wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar; Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar ukiongoza Idara ya Uchumi na Fedha, kwanini hukusema hayo katika vikao halali vya chama?”nasi tunawauliza vikao halali ni vipi vya DODOMA ambavyo ukisema kweli wanapanga kukuuwa au vikao vipi..?Wanamtuhumu kwa msimamo wake huo dhidi ya serikali mbili kwamba “anataka kuvuruga tena wana-CCM na kuzorotesha umoja wa kitaifa uliopo tangu kuasisiwa kwa Muungano mwaka 1964.”kisa cha CCM na CUF kuungana ni kuitetea z;bar na kuleta maendeleyo sasa yeye anaitetea wanamshutumu nyinyi makada tutawatia ndani ya azizi nyote murudi musoma mukalime musitulete upumbavu.Hakuna historia ya Polisi kushughulikia vipeperushi vya namna hii maana viliwahi kuwa vingi kuchapishwa na kuenezwa sehemu za mikusanyiko ya watu katika mji wa Zanzibar na kama ndio wao waliofanya basi watashatakiwa wote walio husika maana polisi ni kulinda usalama sio kujingiza ktk siasa.Hivi vilieneza siasa za chuki dhidi ya wanasiasa wa CCM wenyewe na kwa upande mwingine vikilenga kuchafua CUF na viongozi wake, hasahasa Maalim Seif.Ninaamini Polisi ambao hawakufanya chochote juzi na jana kuhusu vipeperushi, hawathubutu kuchunguza leo wakati CCM na CUF wanapanga na kutekeleza mipango mimoja chini ya “siasa za maridhiano.”Ni hapo pananishawishi kuamini katu CCM haina nafasi ya kusikiliza upumbavu wa makanda kwa kumchukia  Mansour ambaye yuko hapa kwa kutetea haki ya wazenji maana ikifanya hivyo, itazidi kutanua wigo wa mazonge yaliyojaa na ambayo yanahatarisha amani na umoja wetu wa watu wa z;bar ili kujikombowa na huyu mkoloni mweusi tanganyika na mansour ataendele kubaki  madarakani mukitaka musitake nyinyi makada na ole wenu tusiwajuwe ila tukiwajuwa z;bar mutaiyona chungu kuliko shubili hatutaki wanafi zenji tunataka wasema kweli na wajasiri kama  Mansour hana hofu; ametulia. Huyu jasiri.

No comments:

Post a Comment