Friday, July 22, 2011

MUWAZA INAWAPONGEZA WAZENJI WOTE KUANZIA VIONGOZI MPAKA RAI WENYE KUPINGANIA HAKI NA UHURU WA ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Mustakabal wa Zanzibar (MUWAZA) Dr. Yussuf Saleh Salim
MUWAZA YAPONGEZA UJASIRI NA USHUJAA..MUWAZA inapenda kutoa pongezi zake za dhati kwa misimamo ya Wazanzibari ya hivi karibuni kwa kujitokeza kinaga ubaga kutetea maslahi ya Zanzibar. Maslahi ambayo yamekuwa yakipokonywa tokea siku za awali za kuundwa kwa Muungano.Hii si mara ya kwanza kwa Wazanzibari kujitokeza kwa uwazi kukemea dhulma waliotendedewa Wazanzibari. Maafa waliyoyapata viongozi wa Kizanzibari wakati wakipigania mustakbal wa Zanzibar si siri.Tumeshuhudia jinsi Rais wa Zanzibar Alhajj Aboud Jumbe alivyouzuliwa kidikteta.Tumeshuhudia namna Waziri Kiongozi Sh. Ramadhan haji alivyotimuliwa.Tumeshuhudia jinsi Rais Mstaafu Dr. Salmin Amour alivyoadhiriwa na Bara
Tumeona jinsi akina Marehemu Shaaban Mloo, Maalim Seif na wengine walivyofukuzwa Chamani kwa kuitetea Zanzibar.Tumeona jinsi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado aliyotupwa korokonin bila ya kupandishwa mahakamani.Tumeshuhudia jinsi Mwanasheria Mkuu Bashir E. Kwaw-Swanzy alivonyan´ganywa uraia na kufukuzwa nchi.Tumejionea jinsi Makatibu wakuu wa Wizara tofauti za Zanzibar namna walivyoparaganywa Wote hao na wengi wengineo walipigwa vita vikali kwa sababu ya kutetea haki za Zanzibar.Dhulma tofauti za kuifisidi Zanzibar ni nyingi sana na ziko dhahiri kwa wengi wa Wazanzibari bila ya kuwa na haja ya kuzitaja moja baada ya moja. Juu ya kwamba viongozi wa Kizanzibari wamepata maafa tofauti kwa kupigania haki za Zanzibar, maafa na mateso hayo hayajawatisha si viongozi, si wataalamu, si taasisi wala Wazanzibari wa kawaida.Wazanzibari walio wengi wamesimama pamoja na wako imara kulinda mustakbal wa Zanzibar bila ya uoga au kujali yatayowafika binafsi.MUWAZA inapenda kutoa pongezi za dhati kwa wale wote wanayoipenda na kuitetea nchi yao ya Zanzibar Khususan Viongozi washupavu kama Rais Mtaafu Dr. Aman Abeid Karume na Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuondosha khitilafu za kisiasa na kutetea mustakbal wa Zanzibar.MUWAZA inawapongeza Wawakilishi na Wabunge wa Kizanzibari kwa misimamo yao madhubuti kutetea maslahi ya Zanzibar bila ya kujali vitisho vya kina Mazengo Pinda na Samuel Sitta,saba,tisa MUWAZA inawapongeza Wanasheria na Wataalamu wa Kizanzibari, pamoja na waandishi wa habari, kwa taaluma walio na wanayoendelea kutoa kwa Wazanzibar kuhusu haki za Zanzibar
MUWAZA inapongeza taasisi zote ikiwemo UAMSHO kwa ushupavu wao wa kuelimisha Umma wa kizanzibari kutetea haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii na za kidola za Zanzibar.MUWAZA inawapongeza wazee wa Kizanzibari, kwa kusimamia maslahi ya Zanzibar na kutokubali kuburutwa.MUWAZA inawalaani vikali vibaraka na vitimba kwiri wasambazaji wa vipeperushi za kifitina. Hawa ni wale wale waliopinga maridhiano, kutaka watu waendelee kuuwana na kukubali kutumiliwa na Bara kwa maslahi yao binafsi.
MUWAZA inawatangazia vita kwa kuwaomba Wazanzibari wote wawaandame usiku na mchana na kuwafichua kwa unafiki wao wa kuwasujudia mabwana zao wa Bara.MUWAZA inampongeza Waziri Mansoor Yussuf Himid kwa ujasiri na ushujaa wake wa kutetea Wazanzibari na rasimali zake na nchi yake kwa ujumla.MUWAZA inamtupia changa moto Rais wa Serikali ya maridhiano, Dr. Mohammed Ali Shein, achukuwe msimamo wa dhahiri kutetea mustakbal wa Zanzibar, kutanabahisha na kujitenga na wale wasioitakia Zanzibar kheri kwa kuleta fitina ikiwemo ya vipeperushi vya fitina.
Dr. Yussuf S. Salim
Mwenyekiti wa MUWAZA
Copenhagen
Denmark

No comments:

Post a Comment