Thursday, July 7, 2011

MWANZA KUNANI..? HAYA WAESHIA WA MWANZA WASHAA ANZWA WAZANZIBAR MULIYO TANGANYIKA TIENI MAJI MUKIONA MWENZENU ANYOLEWA.

Risasi, mambomu vyarindima Mwanza,wamachinga
 wapingwa risasi na mabomu ya machozi jijini mwanza
 mpaka sasa hatujajuwa kama mambo nishwari au laa
watu wanye asili ya kieshia wavunjiwa maduka yao
 na nyumba zao na kuibiwa mali zao ndani ya
 maduka yao leo hii jijini mwanza.
Thursday, 07 July 2011 11:24
Gari likiwa limechomwa moto katika mkoa wa
Mwanza kufuatia vurugu zilizotokea kati ya jeshi la
 polisi na wafanya biashara wadogo(wamachinga)
Mwanza
RISASI za moto, mawe na mabomu ya machozi
jana viliyateka majiji ya Mwanza na
Dar es Salaa, kufuatia kuibuka kwa vurugu
 zilizowalazimisha polisi kutumia silaha
za moto katika miji hiyo.

Jijini Mwanza mapambano yalikuwa ni baina
 ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama
wamachinga, ambao waliingia vitani na askari
polisi hali iliyosababisha maduka, ofisi na huduma
 mbalimbali kusimama kwa muda wa saa saba.

Katika vurugu hizo askari Polisi walikuwa wakihaha
 kila kona ya mji kuzuia uharibifu wa mali kutokana
 na watu wanaodaiwa kuwa wafanyabiashara
ndogondogo (machinga) kuchoma magari moto,
kuvunja magari vioo na maduka huku wengine
 wakipora mali madukani na hotelini.

Vurugu hizo zilianza majira ya saa 3:45 asubuhi
 baada ya wamachinga kumiminika katika mitaa
 ya Makoroboi, Rwagasore na Lumumba na
 kukuta polisi na mgambo wa jiji wametanda
 kuzuia wasifanye biashara. Askari hao walifika
katika mitaa hiyo kuanzia majira ya saa 12: 00 asubuhi.

“Polisi waliowahi asubuhi walikuwa wachache,
 na kutokana na machinga kuwa wachache muda
huo walifanikiwa kuwazuia, lakini kumbe machinga
walikuwa wakikusanyika, kadri muda ulivyokuwa
 ukisonga,”alisema mmoja wa wafanyabiashara na kuongeza:

“Baadaye  walifika machinga wengi, na ndipo
 walipoanza kuzomeana na polisi na kisha kuwarushia
mawe polisi kiasi cha kuzidiwa nguvu”.

Kutokana uchache wao, polisi walizidiwa
 nguvu na wamachinga waliokuwa wakiwashambulia
 kwa mawe, hivyo polisi hao kuanza kutimua
 mbio huku wakitumia radio za mawasiliano
 kuomba msaada kwa wenzao.

Kati ya askari hao, ni wawili tu waliokuwa na
 silaha za moto na wengine walikuwa na virungu,
 hivyo ikawa rahisi kwa wamachinga
kuwazidi nguvu kwa kutumia mawe.

Kauli ya polisi
Taarifa ya kuzidiwa kwa askari hao zilimfanya
 kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,
Simon Sirro kutembelea eneo la tukio na
 kuzungumza na machinga na kuagiza
askari wake kuondoka eneo hilo la Makoroboi,
 kauli iliyoshangiliwa na wamachinga.

mkuu wa polisi mwanza akishangiliwa na machinga

Baadaye Sirro aliwaambia waandishi wa habari
 kuwa jeshi lake liliombwa kusaidia mgambo
wa jiji kuzuia wamachinga kufanya biashara
 katika baadhi ya maeneo wasiyoruhusiwa na
walifanya hivyo, lakini ghafla hali ilibadilika na
kutolewa taarifa kwamba waruhusiwe.

“Hatuwezi kufanya kazi katika migongano,
sisi tumekwenda kuzuia wamachinga huku
 nyuma tena ikatoka kauli kuwa hilo eneo
waendelee tusiwazuie, sasa nilichoamua ni
 kuwaondoa askari wangu, wakishakubaliana
 wao watatuambia la kufanya,” alieleza kamanda Sirro.

Maduka yaporwa
Baada ya Sirro kuondoka, wamachinga walizusha
 upya vurugu ambapo safari hii kundi moja likiwa
 linamsindikiza kamanda na kumuimbia
‘Sirro..Siroo..’ kundi lingine lilianza kuvamia
 maduka na kupora mali za watu.


Miongoni mwa maduka yaliyopowa ni Zara Solar Ltd
 mali ya Mohamed Papia, ambako wavamizi
wapatao 50 waliingia dukani humo na
kupora fedha na vifaa mbalimbali vya umeme
baada ya kuvunja vioo vya duka hilo pamoja na mlango
.

FFU ikijaribu kwenda kuzima fujo hilo
 lililotokea mwanza

“Wameingia kundi, wamefanya wanavyotaka,
 kila aliyeingia amebeba alichoweza…
wamebeba mpaka hela,” alieleza Papia.

Wakati polisi wakutuliza ghasia katika duka la Zara,
 kundi lingine la wamachinga lilivamia
Mwanza Hosipitali iliyopo mtaa wa Rufiji ambako
 walivunja vioo vya jingo hilo na kuharibu jenereta.

Kundi jingine lilivamia Hotel za Florida
ambako watu hao walipora viti, meza na
vinywaji, huku hoteli ya Kembice iliyopo
 katika mtaa huo ikipondwa kwa mawe na
vioo vyake kuvunjwa.Katika vurugu hizo
mgari kadhaa pia yaliharibiwa vibaya.

moja ktk majengo ya waeshi
yaliyo pata kipigo cha mawe

Habari zilizopatikana jijini Mwanza zilisema
 wavamizi hao walisikika wakisema watakuwa
 wakipambana na wafanyabiashara wenye
 asili ya kiasia kutokana na kuamini kuwa
wao ndiyo wamekuwa wakifaidi kwa kufanya
 biashara salama wakati wao wakipigwa na
 kuporwa vitu vyao.

“Leo wameingia kwangu kupora wakisema
 tunarudisha mtaji wetu ambao tumekuwa
 tukiporwa na jiji, hii ni hatari sana,”
alieleza mmoja wa wafanyabiashara hao.

moja wa machinga mwenye hasira
akijitayarisha kurusha jiwe lake


moto uliyo washwa na machinga
jijini mwanza kwa hasira.

Majeruhi wa Risasi
Habari kutoka Hospitali ya mkoa wa Mwanza,
 Sekou Toure zimeeleza kuwa walipokea
majeruhi wanne ambapo wawili hali zao
zilikuwa mbaya hivyo kuhamishiwa hospitali ya rufaa
 ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo
 ambaye hakutaka kutajwa jina lake,
aliwataja majeruhi hao kuwa
Omari Abdalah (25) mkazi wa Nyashana
 ambaye ni fundi wa Koroboi, Kelvin Jeremia (16)
ambaye amejeruhiwa kwa risasi mgongoni,
 Pastory Brison (25) ambaye alijeruhiwa kwa risasi
 kiunoni na mwingine aliyefahamika kwa
 jina la Juma ambaye alifikishwa akiwa hajitambui.

Muuguzi huyo alisema Juma na Pastory
walihamishiwa hospitali ya rufaa ya Bugando
 kutokana na majeraha yao kuwa makubwa,
 hivyo kuhitaji matibabu zaidi.

Kauli ya Jiji
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,
Frances Mkabenga alisema mpango wao
 ulikuwa ni kuwahamisha wamachinga hao
 kutoka eneo la Makoroboi kwenda katika
eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

“Tulikuwa na kazi mbili leo (jana) ya kwanza
 ni kuhamisha machinga na kituo cha daladala,
askari waliwahi asubuhi na mapema sana na
 tulifanikiwa, lakini ghafla saa nne walitueleza
kuwa kuna vurugu zimezuka na sasa hali ndiyo hii,
 hatujui nini kilifanya vurugu kuzuka pengine labda
 kuna mtu kawashawishi, hatujui,”
alieleza kaimu mkurugeni huyo.

watu wakikimbizana jijini mwanza baada
ya machinga kutiya moto maduka ya waesia

wauzaji wa soko kuu mwanza
wakishuhudiya tukio hilo

moto uliyo washwa na machinga
 ukiendeleya kuwaka jijini mwanza

hapa ndio jijini mwanza watu wakishuhudiya
 tukio wengine wanatembeya hata hawajali

hii ni moja ya dala dala iliyo pata bahati baya
 ya kuchomwa moto ila ulizimwa haraka

No comments:

Post a Comment