Wednesday, July 20, 2011

NCHI YA Z;BAR YA ISHINDA NCHI YA TANGANYIKA VIBAYA VIBAYA KTK MCHEZO WA JUDO


MASHINDANO ya 5 ya mchezo wa Judo ya Afrika Mashariki na Kati yamemalizika jana usiku katika ukumbi wa Landmark Hotel Ubungo na wenyeji nchi ya tanganyika kushika nafasi ya mwisho katika mashindano hayo.Katika mashindano hayo timu ya nchi ya Zanzibar ilijinyakulia medali 5 za dhahabu, 4 za fedha na kikombe cha ushindi wa kwanza huku nchi Kenya ikishika nafasi ya pili kwa kushinda medali nyingi ambazo ni dhahabu 4, fedha 6 na shaba 6.Mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni nchi ya Burundi ambayo ilijinyakulia medali 3 za dhahabu,3 za fedha na 6 za shaba na nchi ya  Tanganyika ilijinyakulia medali moja ya dhahabu na kikombe cha kupokea medali ya dhahabu kwa mara ya kwanza tangu mashindano hayo yaanze miaka 5 iliyopita pamoja na medali 5 za shaba.Pia,nchi hiyo ya  Tanganyika ilipongezwa kwa kutoa mchezaji chipukizi mwenye umri wa miaka 16, Andrew Thomas ndiye aliyewatoa kimasomaso Watanganyika kwa kupata medali hiyo ya dhahabu kwa mara ya kwanza kwenye historia katika nchi hii.Mgeni rasmi katika ufungaji wa mashindano hayo Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Juliana Yasoda alisema Watanganyika wamefarijika na hatua aliyotufikisha kijana Andrew Thomas na kuahidi kumfikisha mbali zaidi na kuwapa vijana wetu ushirikiano wa kutosha ili wafanye vizuri zaidi katika mashindano yajayo.Aidha, kwa upande wa wachezaji bora wa wanaume, Hassan Bigirimana kutoka Burundi alijinyakulia nafasi hiyo huku mwadada, Esther Akinyi kutoka nchini Kenya alijishindia nafasi hiyo kwa upande wa wanawake.

No comments:

Post a Comment