Friday, July 15, 2011

PINDA APINGA MUUNGANO WA AINA YOYOTE ASEMA HUU NDIO MZURI

Mizengo Peter Pinda
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema mfumo wa sasa wa muungano ni mzuri na kusema hatua yoyote itakayobadili mfumo huo ni utahatarisha uimara wa muungano wenyewe.
Akijibu maswali ya papo kwa pao bungeni mjini Dodoma amesema kwa vile marekebisho ya katiba yatafanyika wananchi watakuwa na fursa ya kuchagua mfumo unaofaa ambao utakuwa na maslahi kwa pande mbili.Hata hivyo amesema mfumo wowote wa muungano utakaoziweka Tanzania bara na Zanzibar katika hali ya kufanana mfumo huo utakuwa mgumu kuutekeleza kutokana na idadi ya watu ya kila upande.
Hivyo waziri mkuu Pinda amewataka watanzania kuendelea kudumisha muungano kwa kuangalia matatizo yanayoukabili kwa umakini badala ya kutumia jazbaKipindi hicho cha maswali na majibu ya papo kwa papo kimechukua muda mkubwa wa hoja za masuala ya muungano, umeme na mafuta

mimi nauliza watanganyika AU sisi WAZENJI.? mimi naona  wasubiri marekebisho ya katiba maana wao katiba yao ndio iliyogeuzwa na kuwa ya muungano sasa wao wasubiri marekebisho ya katiba ili wajuwe katiba ya muungano ni ipi na yatanganyika ni ipi maana sasa wanataka kututia katika serekali moja kwa kini macho cha katiba sisi katiba ya tanganyika haituhusu kwanini tuchangiye..?watu million 44 hawatoshi kuchangia katiba hiyo mpaka sisi wazenji pia tuchangie nawambiyeni tukichangia katiba ya bara mujuwe ndio tushajitia tanzi la koo nawala halitatutoka mpaka tutakufa.sisi tuna katiba yetu na kila kitu wao ndio walijifanya wajanja kuigeuza katiba yao kuwa ya muungano sasa wanatupeleka kwenye serekali moja maana tukichangia tu watasema simulichangia mukasema munataka hivi na vile tumewapa sasa nini tena hawa ndio plani yao.namnuku alivyosema((Hata hivyo amesema mfumo wowote wa muungano utakaoziweka Tanzania bara na Zanzibar katika hali ya kufanana mfumo huo utakuwa mgumu kuutekeleza kutokana na idadi ya watu ya kila upande.))je munaona sasa walivyo kigeuza kisahani sasa ndio wanajuwa kuwa wao wako wengi kuliko sisi ila miaka 47 wametonyonya nakutunyonya mpaka tumekuwa mafukara hawakusema kitu kama nyinyi muko kidogo chukuweni hichi na kile ili maisha yawe mazuri hata wamebana kimya sasa motu unawawakiya kwenye miguu ndio haitawezekana tanzania na zanzibar kuziweka katika hali ya kufanana kama hawatake nusu bin nusu ndio pakuvunjwa kila moja akangalia maisha yake kwa salama kabisa maana huu ni ujinga wa mwisho skanavia yani sweden,norway na denmark wameugana na denmark ni kinchi kidogo kweli ila hujasikia upumbavu huu ati haitawezekana hiyo E.U.tunayo isikia sasa kuna vinchi vidogo vidogo tele ndani na vinapewa haki sawa hakuna ati germany ni kubwa wao wale zaidi au spain ni kubwa wao ndio wachukuwe kingi hakuna upumbavu huu uko hapa kwa hawa wanyarugusu tu nie yao nikuiyuwa znz ila watakufa wao znz iko pale pale yuko wapi nyerere mbona kaiwacha na wao watafuatia kwa uwezo wa m/mungu.

No comments:

Post a Comment