Friday, July 15, 2011

PINDA ASEMA TANGANYIKA ISIFANANISHWE NA ZANZIBAR KWA KUWA MWISHO WAKE SIO MZURI

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameonya Muungano usiangaliwe kwa kufananisha Zanzibar na Tanzania Bara kwa kuwa mwisho wake si mzuri. Alifafanua kuwa Tanzania Bara, wapo Watanzania zaidi ya milioni 42 wakati Zanzibar milioni moja na ushee; watu wa namna hiyo wakiuangalia Muungano huo katika mazingira ya kufanana, itakuwa vigumu. Alikuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Mwanamrisho Abama (Chadema), aliyetaka kufanyike kura ya maoni ili Watanzania wa pande zote za Muungano kuamua kama wanataka Muungano na uwe wa aina gani. Abama pia alisema Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume, alisema Muungano ni kama koti, likikubana unaweza kuvua na kwa kuwa kuna kero za Muungano, anaona wakati umefika wa kulivua. Mbunge huyo wa Chadema ambayo ina sera ya kutaka Muungano wa na Serikali tatu, alisema ikiwa Zanzibar watataka kuvunja Muungano, je, Tanzania Bara itakuwa tayari kutoa baraka zake. Akijibu maswali hayo, Pinda alisema Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili zilizoungana ingawa yapo matatizo ya hapa na pale, kikubwa ni kuendelea kuzungumza. “Muungano umeleta heshima, mimi napata faraja kuona Wazanzibari wamejenga majengo makubwa Tanzania Bara na wanaishi bila wasiwasi, lakini kama kuna mambo, tuyajadili,” alisema. Kuhusu muda wa kuvunja Muungano, Pinda alisema sasa Watanzania wanazungumza kuhusu Katiba mpya na kuwataka katika mazungumzo hayo kuwa waangalifu kuendelea kuheshimu Muungano unaotambua kuwepo nchi ya Zanzibar, kwa kuwa kuifananisha na Tanzania Bara, mwishowe si mzuri. Katika hatua nyingine, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alimtaka Pinda aeleze lini watamuondoa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta katika nyumba anayoishi ambayo analipiwa Sh milioni 12 kwa mwezi.
Alisema, Sitta alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa heshima yake kama Spika, lakini tangu aache nafasi hiyo, ameendelea kuishi katika nyumba hiyo na kutaka Serikali iseme lini atahama na kwenda kuishi na wenzake Kijitonyama. Pia Mbunge huyo alitaka Sitta, mkewe na msaidizi wake wasisafiri katika daraja la kwanza la ndege kama alivyofanya hivi karibuni alipokwenda India. Lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisimama na kufafanua kuwa Sitta ni Spika mstaafu na stahiki zake zinagharamiwa na Bunge kama ilivyo kwa maaspika wastaafu akiwemo Pius Msekwa na hivyo anayepaswa kuulizwa si Waziri Mkuu, bali Bunge.

pinda anaona wazenji washachachama sasa ati anasema anafaharishwa na wazenji waliyojenga majumba makubwa makubwa bara na pia anafuraha sana kuwa zenji ni nchi waliyo ungana sialisema kama zenji sio nchi huu pia hawa ni sumuni bukumuni umyuni fahum laa yarjiuni  muungano nchi zikiungana haziangali wewe unawatu wangapi kwa nini kila tukizungumza sisi ni wengi wao kidogo basi vunjeni mukaugane na kenya wako wengi kama nyinyi na uganda na malawi duuuuuuuh vichwa vigumu kweli kusikia amakweli mtwana ni mtwana tu hata umuogeshe vipi bado atanuka kisha anasema tukae na kuzungumza hakuna cha kuzungumza ni mambo madogo WAZENJI HATUTAKI TENA MUUNGANO KWISHA.na huyu anne makinda ya jiwa anamtetea mwenzake maana na yeye anaishi katika jumba kama hilo na mamilioni yanalipiwa kodi ya nyumba wanazo ishii wakati watanganyika wanahaha machinga na wengine kama hamuja amkaa watanganyika mutaburuzwa na hawa viongozi wenu mpaka kufa hawawajali wao wanaishi powa na familia zao unasikia hata wake zao pia na watoto wao wanasafiri daraja la kwanza ktk denge kama wao ndio maspika au raisi na niwake tu na watoto na huku kariakoo mtaa wa kongo munanyanyasika na maisha munadanganywa tanganyika ni nchi masikini maweeeeeeeeee.

No comments:

Post a Comment