Monday, July 11, 2011

SAMIA MUUNGANO TANG-Z;BAR ULIPO UNGANISHWA WAKATI ULE NANI ANGELIULIZWA..?

HILI NDIO JINAMIZI JIPYA LINALO IYUWA ZANZIBAR
Waziri wa Muungano, Samia Hassan Suluhu, amesema hakuna haja ya kuangalia namna muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyofikiwa kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kufukua makaburi.
Waziri Suluhu aliyasema hayo bungeni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge hususani mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye aliitaka serikali iweke bayana namna muungano ulivyofikiwa na sio kuonyesha picha za waasisi wake wakichanganya udongo.
Lissu pia alisema Muungano ulifanyika kwa usiri mkubwa na kwa shinikizo la mataifa makubwa, bila kushirikisha wananchi wala Wawakilishi, jambo ambalo linachangia kero.
Akijibu, Suluhu alisema kuweka hadharani nyaraka hizo ni kuuchokonoa Muungano na kwamba kwa sasa Zanzibar imetulia hivyo iachwe iendelee na maisha mapya.
“Muungano ni kama mtoto ukianza kutafuta amezaliwa vipi, sijui alizaliwa kwa wembe au kawaida haitasaidia kwa sababu tayari ni mtoto, mtoto hakosi kasoro…tuzungumze Muungano lakini tusifukue makaburi,” alisema.
“Tuacheni Zanzibar…imetulia, tafadhalini msitufukulie makaburi, unavyosema wananchi hawakushirikishwa, hivi wakati ule nani angeulizwa jamani?” alihoji.
Badala yake, aliwataka Watanzania kuyajadili na kuyapatia ufumbuzi mambo yanayoukabili Muungano hivi sasa.
Baada ya maelezo hayo, Lissu alihoji watu kadhaa waliokufa wakati wa harakati za kuunda muungano “kutokiri makosa sio kutoa elimu kwa Watanzania, hivi wako wapi akina Kassim Hanga, Abdallah Tula, Mdungi Usi na wengine? Itakuwa bora sana kama wananchi wataelezwa ukweli wa jambo hili.”
MAJINAMIZI YANAYO IYUWA ZANZIBAR NDIO HAYA NA MENGINE YAMEJIFICHA ILA SIKU ZA MWIZI NI ARUBAINI YATAFICHUKA TU MOJA BAADA YA JENGINE MAJINI

SAMIA WAKATI ULE WATU HAWAKULIZWA MAANA KULIKUWA NA DIKTETA NYERERE UKIULIZA TU UNAULIWA SASA WATU WATAULIZA KWALI NA SASA KAMA WEWE NI KWELI UNAITAKIA ZNZ MEMA BASI NIWAKUTOWA KARATASI NA KUONYESHA UKWELI MSEMA KWELI MPENZI WA M/MUNGU OOOOPP WEWE HATA HUYO M/MUNGU HUMJUWI WAJUWA DODOMA TU HAKUNA CHA KUFUKUWA KABURI WALA NINI KAMA NDIO HAKI BASI YAFUKULIWE TU ILI HAKI ITENDEKE  WAKO WAPI KINA KASSIM HANGA,ABDALLAH TULA ,MDUNGI USI NA WENGINE WALISHI WAPI NA WAO NDIO WANAMAPINDUZI YA ZNZ AMBAYO WEWE SASA INAKULISHA MPAKA UMEVIMBA KAMA CHURA WAKO WAPI......? JIBUNI WAUWAJI WAKUBWA NYINYI FETHEHA INAWASHUKIYA SASA MAPINDUZI MULIYOKUWA MUKIRINGIA YATAWATOKEYA PUWANI MUNACHEZA NA HAKI NA M/MUNGU NYINYI BORA MKUBALI SASA KUTENDA HAKI KULIKO KUJA KUIBIKA KAMA MKE WA BAGBO NA WENGINE.  

No comments:

Post a Comment