Friday, July 15, 2011

SENSA NDANI YA ZENJI OMAR YUSSUF MZEE ATAKA KUJUWA WAZENJI NI WAGAPI.JE WAKULETWA MULIYOWAPA VITAMBULISHO VYA ZENJI MUTAWAHESABU PIA KUWA NI WAZENJI..?

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaanza majaribio ya Sensa ya Watu na Makazi mwezi ujao na kuwataka wananchi kujitayarisha kwa kazi hiyo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema sensa kamili inatarajia kufanyika Agosti mwakani, na kitakachofanyika mwezi ujao ni matayarisho na maandalizi ya sensa hiyo ili kuona inapata mafanikio makubwa. “Nachukua nafasi hii kuwaomba wananchi wote wa Zanzibar kujitayarisha kwa ajili ya kuhesabiwa…hesabu sahihi ya wananchi wote wanaoishi Zanzibar ni muhimu sana kwa ajili ya mipango na maendeleo ya Serikali,” alisema Mzee na kuwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kufikisha ujumbe huo muhimu kwa maendeleo ya taifa. Alisema kwa mujibu wa taarifa zilizopo, maandalizi ya mchakato wa zoezi hilo kwa sasa unaendelea vizuri kwa ushirikiano na Taasisi ya Takwimu ya Tanzania Bara na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu ya SMZ. Aliwataka wajumbe wa Baraza hilo ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi kuanza kuwahamasisha wananchi kujiweka tayari kwa kazi ya kuhesabiwa.
Alisema lengo la kazi hiyo ni kujua idadi kamili ya wananchi wote wanaoishi Zanzibar ili Serikali ijipange kwa mikakati yake ya maendeleo na sio vinginevyo. “Hakuna sababu ya kuogopa au kuingiwa na wasiwasi kwa zoezi hilo wakati utakapofika….sensa malengo yake makubwa ni kukusanya takwimu ya idadi ya watu katika nchi ili kujua na Serikali kujipanga kwa ajili ya maendeleo yake,” alisema Mzee.
Zanzibar inayojumuisha kisiwa cha Unguja na Pemba katika mwaka 2011 inakisiwa kufikia idadi ya watu wapatao milioni 1.2. ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.2. Mzee alikiri Zanzibar inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kuwepo kwa kasi ya ukuaji wa watu inayotokana na uzazi usiokuwa na mpangilio.
Alisema idadi ya watu na kasi ya kuongezeka ni suala zito na ni changamoto kubwa kwa familia, jamii pamoja na Serikali na dunia kwa ujumla.

namnuku mzee((maandalizi ya mchakato wa zoezi hilo kwa sasa unaendelea vizuri kwa ushirikiano na Taasisi ya Takwimu ya Tanzania Bara na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu ya SMZ.))sasa kwanini takwimu ya tanzania bara ije kuhisabu watu zenji..?au ndio wanataka kujuwa kuna wabara wangapi na wazenji wangapi kisha ikija kura ya maoni kuhusu muungano kama wazenji wanautaka au hawautaki wajuwe vya kuubiruwa ili iyonekane kama wazenji wamesema yes kwa muungano feki sio..?au munataka kujuwa ni waburundi wangapi mumewapa vitambulisho vya kizenji..?je wale vichiibongo vilivyo letwa zenji wakati wakupinga kura mukawapa vitambulisho vya zenji pia mutawahesabu ni wazenji..?wauza vinyango walioja zenji na wauza karanga na beach boy wakutoka bara waliyokuja zenji kutafuta wazungu pia mutawahesabu ni wazenji au..? 

No comments:

Post a Comment