Monday, July 11, 2011

SITTA AU SABA AU TISA Z;BAR NGOJENI TUMSOMESHE MAANA HAKUSOMA HUYU VIZURI AU KASOMA LAKINI HAKUELEWA MASOMO.

WEWE MAMA SITTA SINYORITA SIKILIZA KWA MAKINI

Asalam-alaikhum ndugu wazanzibari wa ndani na nje ya Nchi yetu tukufu ya Zanzibar. ama sina mengi yakusema ila kumshukuru (AS) kwakutupa Uhai, Uzima, Afya, Umoja na Amani katika Nchi yetu. Hii leo tumesikia kauli ya baadhi ya Wabunge kule DODOMA jinsi wanavonguruma juu ya Uharamu wa muungano na kutokuwepo kwa Uwiano wa magawanyo na mapato ya Muungano.
Kama tulivoona habari ya Samuel Sitaa kwamba kuanzishwa kwa Serikali TATU ni bora tusiwe na MUUNGANO kabisa: Naam wazanzibari hayo ndiyo wanayoyataka kama serekali TATU haitawezekana.
Hizi zote ni cheche za moto wanazotishiwa wazanzxibari ili wasiendelee kudai haki zao. Mfano:
Sitta kasema (ati) kuwepo kwa Tanganyika nikuanzisha ushindani na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ushindani huu tunaoutaka sisi sio wakupigana makombora bali niwakushindana Kibiashara na kukuza uchumi na kuwa maisha mazuri wananchi wote bila ya kusema huyu ni mtoto wa mbunge au mtoto wa muakilishi ndio maana anamaisha mazuri laa kila moja awe na maisha mazuri ndio tunavyotaka sisi hapa zanzibara na ndio nchi zilizo endeleya zilivyo rai wao wote wanamaisha mazuri . Na zipo nchi nyingi tu zenye muungano wa Seriakli Tatu bila ya Matatizo. Mfano:
UK na Scandanavian zina muungano ambao Mdenish, Mnorway, Msweeden, wanahaki yakuishi katika nchi hizi na wanatumia pasport zao za nchi wanazotoka kama itahitajika wote wana pasport za nchi zao lakini nchi zao zina serekali tatu. Lakini ikija wakati wa Ulipaji Tax (kodi) Mdenish kama anafanyakazi Sweeden analipa ile kodi ya Sweeden katika GDP na katika GNP anaipatia nchi yake ya Danmark kwani Serikali ya Denmark ina recordi ya Wadenish wangapi wanaoishi katika nchi hizi za scandanevian.Na nchi nyengine kama Norway na Sweeden zinafanya hivo2. Mashindano walionayo (Offcaourse ) ni yakibiaashara na kila nchi inatakiwa afanye vizuri kunyanyua uchumi wake wa ndani na rai waishi vizuri na amani sio amani lakini njaa imeja nchini ukiuliza ahh tuna amani na umoja na mashirikiano chakukila hatuna tuna amani tu.na  
Muungano wao upo na unaingilia mambo machache tu kama shirika la Ndege la Scandanevian ni la Muungano na wafanyakazi wanatoka sehemu zote Tatu na faida inagawanywa sawasawa sio hapa jambo la muungano watatoka watu 200 bara znz hata 1 hakuna ktk hao 200 kisha munasema muungano mawe labda. kwani hakuna weye mdogo kipopulation na kinchi utapata kidogo katika faida ya Muungano . au mie mdogo nataka kubebwa na weye na badala yake silipi kodi. Laa.
Danmark ni Nchi ndogo katika Scandenevia kieneo na kipopulation lakini inalipa kodi sawa kama nchi nyengine za scandanevian na inapata faida sawa. kila mtu anamuheshimu mwenzake na kila nchi ina pesa yake. japokua ni Koroner hiyo hiyo lakini koroner ya Danmark ni kubwa kuliko ya Norway na Sweedan. Na Norway nitajiri kuliko hizi nchi mbili kwasababu kuna mafuta.
Kwahivyo Nawaomba ndugu WABUNGE wetu na Wazanzibari wote watakao soma Makala hii. musiogope maneno ya SUITA wala SWABA, kamba iwe hii hii na tudai Serikali Tatu au kuvunjwa kwa muungano.
Sitta alisema Tukiwa na Serikali TATU itakayopata hasara ni Zanzibar kwasababu itatakiwa ichangie Serikali ya Muungano ambayo ( amekusudia itakua ni ndogo) Hii Ndugu wazalendo ni Ujinga wa Mzee huyu aliesoma lakini hakufahamu. Kwanini zanzibar ipate hasara wakati Faida na hasara zitakazopatikana kwenye Muungano zitakwenda 50% kwa zanzibar badala ya 0.4% na 50% kwa Tanganyika badala ya 99.6%…? huu sio ujinga tunaoukataa. Ikiwa Mambo ya Muungano yatapunguzwa na kila Serikali itakua na uchumi wake huru na kujitangaza kwake kiuchumi kwanini wazanzibari tusiofika watu millioni tatu tushindwe Kuwa Matajiri wakati resources tunazo na ziko na Manmpower tunayo.
Wazalendo hizi ni sababu zisizowasha jiko na inaonyesha Watanganyika CCM wanafuata kanuni za DICTATOR NYERERE  kwakutaka kuimeza zanzibar . hii sio nyengine ila CHOYO CHAO HAWATAKI KUIONA ZANZIBAR INAKUA TAJIRI NAINANYANYUKA KIUCHUMI.
Wembe ni huu huu tusirudi nyuma wakati umefika wakurekebisha Muungano huu feki kwa Serikali TATU au Kuvunjika. kama sitta hataki Mahakama ya Dunia hawatokataa wakati wazanzibari tunaushahidi wote na Vielelezo vyote vyakukataa Kukandamizwa na Kutawaliwa kimabavu na MKOLONI MWEUSI MTANGANYIKA.

No comments:

Post a Comment