Friday, July 8, 2011

TANG-WACHIMBA MAFUTA NA GASI-Z;BAR YASUBIRI RUHUSA KWA MUME WAO TANGANYIKA AWARUHUSU KWANZA.



MKUU Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali ya
Tanganyika haitaingia gharama zozote wakati meli ya
 Poisedon, itakapokuwa inafanya uchunguzi wa
 mafuta na gesi katika pwani ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu,
Pinda alitoa kauli hiyo jana baada ya kutembelea
 eneo la viwanda vya kujenga meli ili kuona hatua
 mbalimbali za ujenzi wa meli na kuikagua meli ya
uchimbaji mafuta.

alipokuwa akikaguwa meli hiyo ya kuchimba
mafuta

Meli hiyo ya Poisedon inajengwa katika
 Bandari ya Geoje, Kusini Mashariki mwa Seoul,
Korea Kusini.

Waziri Mkuu anatarajiwa kuizindua meli hiyo
 leo saa 4 asubuhi katika Bandari ya Geoje.

Alisema wanachofanya sasa  wataalamu kutoka
 Kampuni ya Petrobas ya Brazil ni kutafiti na
 kubainisha maeneo mawili ambako meli hiyo
itachimba endapo matokeo yatakuwa mazuri.


"Tunaishukuru Serikali ya Brazil kwa kuamua
 kuisadia Serikali ya Tanzania kufanya utafiti
huo muhimu," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alisema hatua hiyo ni dalili njema kuwa uwekezaj
i unawezekana kufanyika Tanzania na kuahidi
 kuwa Serikali ya Tanzania  itafanya kila iwezalo,
kuweka ulinzi wakati wataalamu hao wakiwa kazini ili
kuzuia hatari ya kupambana na maharamia.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu kuhusu
 ujenzi wa meli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa
 Kampuni Petrobas Tanzania, Samuel Miranda,
alisema wanatarajia kwamba meli hiyo itafanya kazi
 katika ukanda wa pwani kwa muda wa miezi 20
 katika maeneo ya kati ya Mafia na Mtwara.

Kuhusu uendelezaji wa miundombinu, Miranda
 alisema hadi sasa wameshawekeza kiasi cha dola
za Marekani milioni 11 na ifikapo Desemba mwaka
huu watatoa Dola za Marekani milioni 14 ili
kuendeleza Bandari ya Mtwara.

Kuhusu utoaji ajira kwa Watanzania, alisema
 wameanza kutoa mafunzo kwa vijana 50 wa
 kike na wa kiume wa kutoka Mtwara ambao wakifaulu,
 watafanya kazi katika meli hiyo.

"Meli hii itakuwa Mtwara na tunatarajia kuanza
 kazi mwanzoni mwa Septemba. Tumeanza na
vijana 50 kuanzia Julai mosi, watapewa mafunzo
 maalumu ya miezi mitatu ya umeme,  umakenika
 na masuala ya uchimbaji mafuta na si kitu kingine," alifafanua.

"Mafunzo haya yanaendeshwa kwa ubia baina ya
 TPDC, Veta, Petrobas na Taasisi ya Cenal ya Brazili
 ambayo inafanana na Veta ya hapa Tanzania,
 nia yetu ni kupata wanafunzi ambao wataendelea
kufundisha vijana wengi zaidi katika fani hii,"alisema.

Mbali na hatua hiyo, Miranda alisema wana
mkataba na wahandisi wanne wa Kitanzania
 ambao tayari wamepelekwa Brazil kwa mafunzo
 ya muda mfupi na kisha watapelekwa Uingereza
ili kujifunza zaidi masuala ya uchimbaji mafuta.

Meneja Mradi wa Kampuni ya Ocean Rig ya
 Uingereza inayosimamia ujenzi wa meli hiyo,
David Gray, alimweleza Waziri Mkuu kwamba
 kwamba meli hiyo yenye urefu wa mita 242 na
 upana wa mita 52, imegharimu Dola za Marekani milioni 800.


ona kazi hii walivyo wajajnja wana chimba mafuta
 na kujenga bandari mpya mtwara na gasi na
 mbona wao hawakusema hatuchimbi wala hatujengi
 bandari mpya mpaka tupate ruhusa kutoka znz..?
 pia na kuchukuwa vijana wao kwenda kusomeya
kuchimba mafuta na kathalika sisi znz tunasubiri
mpaka mume aseme ndio tuchimbe watakaposema
 chembeni watakuwa vinaja wao washasomeya ndio
watakao letwa pemba tunarudi pale pale ya
 TRA-HIV-AIDS ndio yatakayokuwa kwa
mafuta tukisema vunjeni muungano munasema
 tutachochoya fujo mara sijuwi ndugu zetu bara
 watakwenda wapi upumbavu mtupu znz nzima
 tumekuwa kama mazumbukuku ulimwengu uko huku.kulaleki
tanzania ndio pamoja na znz kila siku wanasema
 au sio. haya mafuta
hayooo yanachimbwa na znz kimya viongozi
majuha wakubwa mbona ktk hao vijana 50
hakuna kijana wa kutoka znz...? yatachimbwa
watayauza sisi tume kaa tuu kidumu kidumu
nchi nzima inanuka inanuka znz nzima uvudoo.

No comments:

Post a Comment