Thursday, July 7, 2011

WABUNGE DODOMA WASEMA BORA SEREKALI TATU KULIKO KUVUNJA MUUNGANO.


kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imependekeza kuundwa kwa serikali tatu; ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar, ili kuondoa hisia za upande mmoja wa Muungano kunyonywa pamoja na mambo yanayoonekana ni kero.
Pia imependekeza mafuta ya Zanzibar yaamuliwe na wananchi wa visiwa hivyo kwa kuwa vina rasilimali chache.
Waziri Nchi Kivuli, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Pauline Gekul, aliliambia Bunge jana kuwa kuundwa kwa serikali tatu kutaondoa kero za Muungano na kuufanya uwe endelevu kwa maslahi ya wananchi wa pande zote.
“Ni vyema serikali ikazingatia umuhimu wa kuwapo serikali tatu kwenye mchakato wa Katiba mpya…suala la mafuta liachwe mikononi mwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwa visiwa hivi vina rasilimali chache sana za kiuchumi,” alisema Gekul.
Alisema ili kudumisha Muungano, serikali inapaswa kujenga utamaduni wa kuitisha mikutano maalum ya kikatiba kati ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ili wawakilishi waweze kujadili masuala yanayohusu uhusiano wao.
“Pia tunashauri kuwapo kwa kikao cha pamoja cha uongozi wa ngazi ya taifa kutoka pande zote za Muungano,” alisema Gekul.
Kambi hiyo imependekeza uanzishwaji wa Mahakama ya Muungano ya Katiba itakayosuluhisha malalamiko yanayohusu Muungano.
“Masuala ya rasilimali nyingine yatajadiliwa ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na rasilimali za Tanzania na inatoa mchango wake sahihi katika uchumi wa taifa,” alisema Gekul.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia walishauri serikali iwachukulie hatua watumishi wanaoonekana kuchangia kero za Muungano.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mbunge wa Viti Maalum (CCM) wa kutoka zanzibar, alishauri kwamba kuna haja ya wabunge kupewa semina na ili wauelewe Muungano kwa kuwa asilimia 55, ni vijana ambao hawauelewi vizuri.
Alisema kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wamekuwa wakitaka Muungano uvunjwe bila kuelewa athari au sababu za kuwepo kwake, kwa kuwa michango yao mingi imekuwa ni ya kusoma au kusikia.
Alisema inashangaza kusikia baadhi ya wabunge wakieleza kwamba Zanzibar imemezwa na serikali ya Muungano wakati ndani ya Bunge wapo wabunge wanaotoka Zanzibar kupitia Muungano.
“Wengine wanasema Zanzibar imemezwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania wakati hata mimi leo ni mbunge kutokana na Muungano huo sasa tumemezwa wapi na mimi natokea Zanzibar,” alisema mbunge huyo aliyetokeya ktk tiketi ya(( CCM))zanzibar.
Mbunge huyo alisema Muungano una manufaa kwa Watanzania wote na kwamba, unapaswa kulindwa kwa nguvu na gharama yoyote.
hii ndio acha tufe na njaa lakini muungano udumu AMIII .?

Alisema wanaobeza Muungano wanamkatisha tamaa Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuhakikisha Muungano unadumu.
Mbunge wa Wete (CUF), Ali Mbarouk, alisema kuna kero ndogondogo za Muungano, ambazo zimeingizwa kwenye kamati inayozishughulikia na kuchukua mchakato mrefu bila sababu za msingi.
Alisema inashangaza kuona kero kama ya kutoza ushuru bidhaa zinazotoka upande mmoja wa Muungano kwenda upande mwingine.
Mbunge wa Meatu (Chadema), Meshack Opurukwa, alisema serikali tatu ndilo jibu pekee la kuondoa kero za Muungano zilizopo.
Alisema nia ni kuhakikisha kuwa serikali ya Muungano itakuwa na jukumu la kutatua matatizo ya serikali zote mbili.
Opurukwa alisema masuala kama kodi, umeme na rasilimali, yataweza kutatuliwa na serikali husika na iwapo kutakuwapo kero yoyote, itashughulikiwa na serikali ya Muungano.
Awali, Waziri wa wizara hiyo, Samia Hassan Suluhu, alisema serikali imekuwa ikishughulikia kero za Muungano na kwamba, jukumu hilo ni endelevu hadi zitakapokwisha
ona wananvyo mtesa mnyama kweli hawa ni watu wa kuwa nao ktk muungano.? ikiwa wana roho mbaya ya kufanya mnyama kama hivi basi na binadamu pia hawashindwi. sasa hili juha bunge la CCM lililoshikilia muungano omba mungu udumu ukivunjika usije zanzibar. maana ukija unajuwa tutakavyo kufanya watu kama nyinyi ndio munao irudisha zanzibar nyuma na huyu kikuwadi cha watanganyika suluhu. nyote nyinyi jengeni bara toka sasa maana muungano ukivunjika tu basi watu kama nyinyi z;bar nyote jela. tutawashatki kwa kuisaliti nchi ilipokuwa ktk hali ngumu ya maisha na kusababisha rai kusafa na kuteseka.
Ahsante umejitahidi angalau kidogo unaonekana unafahamu na umesoma alama za nyakati. Hata hivyo, bado unahitaji kupewa darsa zaidi kwani Wazanzibar tumedai sana haki zetu kutoka muungano. Hatma yake ni kutubeza na kutudharau kama vile hatukuhusika na muungano.
Darsa unalohitaji kupewa ni kuwa Wazanzibar hawataki serikali, Wanachotaka ni muungano kujadiliwa upya. Waulizwe wananchi jee wanataka kuendelea na muungano au laaa. Pale watakapochagua kuendelea na muungano ndio wao wachaguwe mfumo wanaoutaka.
Wazanzibar hawako na hawakubali kupangiwa au kuchaguliwa muundo wa muungano. Jaalia umewachagulia hizo serikali tatu, jee utawapa uraia wao? Utawapa ulinzi wa nchi yao? Utawapa utambulisho wa kimataifa wa nchi yao pamoja na kiti chake cha umoja wa mataifa?
Endeleeni kuliburuza, lakini hakikisheni muungano huu haudumu. Karibuni hivi mutajuwa ukweli wake. Wazanzibar hawataki tena muungano, wanachotaka ni kuwa huru na kuondokana na ukoloni wa Kitanganyika.
Wazalendo shimeshime na mwenye mbwa yuko nyuma. Ni wakati wa kukaza kamba. Muungano upate kuamuliwa. Waamuzi ni sisi wenyewe.
Uzanzibar kwanza.

No comments:

Post a Comment