Saturday, July 23, 2011

WALIOPEWA HEKA NA VIWAJA VYA KUPIMA NA SEREKALI BAADA YA MAPINDUZI 1964 NA WAKAJENGA NA YALIKUWA NI MASHAMBA YA WATU JE GNU-SUK-ITAMUWA VIPI KESI ZAO..?

  Kabla ya Serekali ya Umoja wa Kitaifa GNU kuingia madarakani Maalim Seif Shariff aliulizwa jee suala la mashamba yawatu yalio gawanywa baada ya Mapinduzi ya 1964 na Serekali ikagawa maeneo ambayo hivi sasa imekuwa miji mashamba hayo vipi watarudishiwa wenyewe au Serekali itachukuwa hatua gani kulitatua tatizo hili?.Maalim Seif alisema Serekali ijayo haito mnyanganya mtu Nyumba alokwisha jenga na kurudisha Shamba lakini itawalipa fidia wenyewe au kuwatengea maeneo yakuwapa.

Sasa jee Serekali ya Umoja wa Kitaifa ikiongozwa na CCM na CUF akiwa Maalim Seif ni Makamo wakwanza wa Rais imefanya hivyo.? maana hivi sasa kuna kesi nyingi zimerundikana bila Serekali kutowa jawabu nihatua gani itachukuwa kuondosha utata huu ulopo zidi ya jamii.?Jee Serekali ya Umoja wa Kitaifa GNU inayongozwa na Chama cha CCM na CUF kweli imetimiza kauli yao, ambayo alitowa Maalim Seif Shariff kabla ya kunda Serekali hio ya Kitaifa..?Hivi sasa kuna kesi nyingi tu Zamadai baada ya kuingia Serekali ya umoja wa Kitaifa SUK  na kutaka kusibitisha kauli ya Maalim Seif alioitowa kipindi cha nyuma kabla ya kuingia ktk Serekali ya SUK.Katika kauli yake hivi sasa kuna wadai wa aina mbili kuna wadai waliokuwa wamiliki wa mashamba ambayo yalichukuliwa na Serekali baada ya mapinduzi na wakayagawa viwanja ambayo takribani nusu na robo ya unguja na Pemba Nyumba zilizo jengwa zimejengwa ktk mashamba ya watu.Na walio jenga wamepewa nyaraka za serekali na kupimiwa viwanja vya plan na Serekali na yako majumba ambayo yalibomaka kutokana na uchakavu na badae Serekali kuuza eneo hilo au kuuza baathi yao kwa raia na yako yalibakia kuweko mpaka leo ktk Mji mkongwe wa Unguja na Pemba haya yamemilikiwa na Serekali na kuitwa msajili wa Majumba je wenyewe wakija kudai watapewa na hao wanaishi ktk hayo majumba watakwenda wapi..?Sasa kwa kuondosha utata huu na kuisafisha nchi yetu kutokana na mambo yalio fanyika nyuma yasiendelee kufanyika tena na nivuzuri sana maana unaodowa haramu iliyofanywa na kukaribisha halali,hivi sasa walokuwa na mashamba baathi ya mwahali hayapo tena kuna Majumba yamejengwa ktk mashamba yao na imekuwa miji kusema zivunjwe nyumba zote na arudishiwe mwenye shamba itazidi kuleta mfarakano tena mpya ktk jamii? kwa vile miji mingi ya unguja na Pemba iko juu ya mashamba ya watu.Sasa ili Zanzibar ivuke na tupate rehma na baraka za M/mungu ktk nchi yetu isizidi kwenda kwenye thulma, nilazima Serekali ya Umoja wa kitaifa SUK ichukuwe hatua ngumu ya wadai kama alivyo sema Maalim Seif kuwa hatuto wanyanganya watu majumba yao walokwisha kujenga na tukawarudishia viwanja wenyewe kwa vile ni Serekali ilio chukuwa viwanja na kuvigawa na kuwapa hati za serekali.lakufanya Serekali tutalipia fidia kwa wale waasili waliokuwa na mashamba yao na hivi sasa yameshajengwa nyumba za raia na pia wao wakubali kulipwa na kusamehe amaa ikiwa bado shamba liko basi arudishiwe laa kama ndio pashajengwa majumba basi alipwa na yeye awe na imani na huruma ya kusamehe ili nchi yetu ya zanzibar isonge mbele.Sasa chakujiuliza jee Serekali itafanya hivyo.? maana hivi sasa kuna tatizo kubwa sana Zanzibar ktk kesi za madai hayo na mlengwa mkubwa ni serekali kwa vile wao ndio walio chukuwa mashamba na wakakata viwanje vya plan na kufanya miji ambayo takribani kila mji wa Zanzibar utaona umejengwa ktk mashamba ya watu.?Sasa vipi Serekali italikwepa jambo hili au mutatimiza ahadi muliyo itowa.? walipwe fidia ili kujisafisha na thulma ilio fanyika ktk mkono wa serekali au walio jenga wenyewe nyumba hizo na serekali ndio iliyowapa basi wao wamlipe mwenye shamba maana wao walipewa na serekali bure na kama sio bure basi serekali ndio ilipe ama ikiwa mwenye nyumba hiyo aliuziwa kiwanja na mtu mwengine ambaye mtu mwengine huyo ndiye aliyepewa kiwanja hicho na serekali basi huyu wa sasa alipwe na  serekali maana yeye hakujuwa na aliyepewa na serekali ashahama au ashakiuza kiwanja hicho au serekali iwalipe hao wenye mashamba basi kise ishee na wao wakubali kusamehe maana kusamehe ni bora walipwe ilaa wasiwe waganganize kuwa sisi tunataka shamba letu na wakati hakuna tena shamba ni mji sasa walipwa na wasamehe yaliyotokea na tuishi kwa amani na utulivu na halali kwa kila moja wetu.Hivi sasa unaweza kukaa na kujishtukizia umeletawa barua kutoka Wakfu na mali ya amana kwa kupitia kwa Sheha au naibu Sheha kuwa unaitwa Wakfu.Ukifika Wakfu unakutana na familia ambayo inakuambia pale ulipo jenga lilikuwa ni shamba letu ambalo lilichukuliwa na Serekali na likagawiwa viwanja, kwa hio sisi tuna pataka wenyewe, sasa kuna mambo mawili hapo kukubaliana kukusamehe kwa vile umesha jenga na hukujuwa na badae ukalipa fidia wewe mwenyewe binafsi, au kukwambia sisi hatutaki chochote tunataka sehemu yetu tu.Sasa ili serekali iondowe utata huu uliowaingizia wananchi hivi sasa nilazima iyashughulikie mambo haya haraka kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu na m/mungu aingize mkono wake wa kheri ili isafike.Hapa kuna thulma  mbili hapa kuna mthulumiwa wa mwanzo alokuwa na Shamba na wapili ni alopewa na serekali kiwanja kujenga bila kujuwa kama hili lilikuwa shamba la mtu aliyenyanganywe miaka hiyo ya mapinduzi ya 1964.Wote hawa ni walengwa na Serekali ndio muhusika mkubwa wa utata huu wa kuchukuwa mashamba na kuyageuza miji.Kuna jamaa wengi hivi sasa wenye asili za kiswahili walio kimbia wakati wa mapinduzi na walikuwa na mashamba yao na  kiarabu na kihindi wanadai majumba yao ya mji mkongwe,mengine bado yapo lakini mengine yamesha anguka na kuzwa kwa watu wa kawaida na kujengwa nyumba nyingine juu yake au bado yako ila yamefanywa hoteli za kitali na bar na disco na kathalika.nilazima serekali itowe jibu haraka ya utata huu ambao wao ndio wahusika wakubwa ili kila moja apate haki yake na kila moja awe anaisha mahali hapo kuwa ni halali na hapo tutapinga hatuwa kubwa sana z;bar na tutaendeleya kupendana kwa kila hali na mali maana sote sasa ni dungu ima wasamehe hivyo viwanja au walipwe na walio jenga kama wenye shamba wanataka shamba lao basi serekali imlipe huyu aliye jenga au imlipe yule mwenye shamba ili yaishe isikae tu kimya kimya na kuwacha watu wakiparurana hii ni serekali ya GNU-SUK ambayo wananchi wengi wana moyo nayo sasa nyinyi onyesheni ujasiri wenu ili sote tuishi kwa furaha inshaa allah m/mungu ibariki zanzibar yetu.

No comments:

Post a Comment