Friday, July 15, 2011

WAZIRI MANSOOR YUSSUF HIMID AUVUWA UKEREKETWA NAKUTETEA HAKI NA UHURU WA Z;BAR

Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid, amevunja ukereketwa na kusema mfumo wa serikali mbili katika sura ya Muungano umepitwa na wakati na kwamba, sasa unaruhusu kuwapo kwa serikali tatu.“Hapa mpango wa serikali moja hatutaki kulisikia. Mfumo huu butu wa serikali mbili. Sasa basi twende kwa jambo, ambalo kila mmoja wetu analizungumza, la serikali tatu na mengineyo,” alisema Mansoor katika mchango wake kwa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati.
Alisema sura ya sasa ya Muungano imegeuka ndoana kwa Zanzibar na inatumika kuwa uwanja wa vitisho kwa Zanzibar inapodai haki zake kama nchi iliyochangia kuundwa kwa Tanzania baada ya kuungana na Tanganyika.Alisema inashangaza kuibuka kwa viongozi katika Bunge la Muungano kushikia bango suala la mafuta kuwa si raslimali ya Zanizbar kwa maelezo kuwa yapo katika mpaka wa bahari kati ya Tanga na Zanzibar.“Mimi sitaki kuwataja kwa majina, lakini niseme nawaonea huruma tu, wameishiwa. Lakini hawa ni wale wenye fikra za miaka hiyo ya kutisha Zanzibar hii kwamba wanaona kusimama bwana mkubwa, watu wanaanza kutetemeka,…huku hayo yamepitwa na wakati,” alisema Mansoor.Ingawa hakuwataja, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hivi karibuni kwa nyakati tofauti kila mmoja alitoa kauli ya kukemea tabia ya kuzungumza suala la Muungano kwa jazba na kuonya kuwa kuanzisha mfumo wa serikali tatu ni kuunda mpinzani dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Mansoor alisema ili kuondokana na vitisho vinavyotolewa dhidi ya Zanzibar, kazi kubwa inayowakabili wawakilishi, akiwamo yeye, ni kuwandaa Wazanzibari juu ya namna ya kushiriki kwa ufanisi katika utoaji maoni ya katiba mpya.“Tukawaelimishe na kuwaandaa Wazanzibari namna ya kujadili na kuzungumza upya makubaliano ya Muungano,” alisema Mansoor ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Mweka Hazina wa CCM na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM).Aliongeza kama wapo Wazanzibari wanaogopa kuanzisha suala hilo, kwa kauli hii yeye ndio anaanzisha mchakato huo. Kuhusu suala la mafuta na gesi asilia, alisema uamuzi uliopitishwa na BLM na Baraza la Wawakilishi (BLW) wa kuiondoa sekta hiyo katika orodha ya mambo ya Muungano ndio wa mwisho wa malumbano yanayohusu suala hilo.

ASANTE SANA hivi ndio tunavyotaka viongozi wa zenji kuwa kama simba sio wakitishwa wanakuwa mabubu upumbavu ngani huu wasilete mikwara ya kuku kutunisha manyoya ya shingoo kama wabunge wote na wawakilishi wote mungelikuwa hivi zenji ingelikuwa mbali sana tena sana ila hatujachelewa bado bali tuwe makini ili wasije wakajidai oohh basi hivi na vile mushawajuwa sasa hakuna tena cha kunde wala mbazi na wakileta nuksi tunavunja muungano wakituvamia tunawashtaki U.N. kwisha moja moja atakwenda deen hugea akanyie ndoo kama wengine.M/MUNGU IBARIKI ZENJI NA WATU WAKE WOTE.

No comments:

Post a Comment