Sunday, July 17, 2011

PINDA NA UMEME WAKE WA MITUMBAAAAA NDANI YA TANGANYIKA


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali inafikiria kubadili kanuni ili  kuruhusu ununuzi wa mitambo iliyotumika ya kuzalishia umeme ili  kulinusuru taifa dhidi ya mgao unaoendelea.Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana bungeni, alipokuwa  akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Iramba Magharibi-CCM)Mwigulu Nchemba.Katika swali lake mbunge huyo alihoji saabu za serikali kutochukua hatua za haraka za kubadilisha kanuni za manunuzi ya vifaa vya umma, ili kuruhusu ununuzi wa mitambo ya umeme iliyotumika na kuliwezesha taifa kuzalisha umeme.Alisema hatua hiyo itasaidia kunusuru taifa katika hatari ya kuzalisha wezi hasa baada ya kusimama kwa shughuli za uzalishaji mali kunakotokana na kukosekana kwa umeme.Nchemba alisema kwa hali ilivyo sasa, kuna hatari ya taifa kuzalisha vibaka hasa kama serikali haitachukua hatua za haraka na za makusudi, kumaliza tatizo la umeme.Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema kanuni za zamani zilikataza kununua mitambo iliyotumika na  haikuwa kazi rahisi kupata mitambo mipya ya kufulia umeme kwa sababu mchakato wake, unachukua zaidi ya miaka miwili.Alisema hata hivyo kutokana na hali ilivyo sasa nchini, serikali inafikiria kubadili kanuni hizo na kwamba mchakato huo, utashirikisha kamati zote za Bunge, ili zikubaliane na kufikia muafaka wa kununua mitambo ambayo itakuwa haijatumika sana."Kamati zote zitashirikishwa ili kuona namna bora ya kuboresha jambo hili na tukikubaliana tutanunua mitambo iliyotumika kwa haraka ndani ya miezi miwili hadi mitatu, ili kuondoa tatizo la umeme ambalo kwa kweli ni janga. Hata hivyo mitambo hiyo inapaswa isiwe imetumika zaidi ya miaka miwili,"alisisitiza  Pinda.Mapema, mbunge wa Mikumi-CCM, Abdulsaalam Ameir, alitaka kujua kama serikali ina mpango wowote wa kupeleka umeme katika Kata za Ulaya, Zombo, Kisangi na Kijiji cha Mhenda katika jimbo hilo.Mbunge huyo pia alitaka kujua kama serikali itakuwa tayari kuiruhusu taasisi ya kidini inayotaka kuweka umeme katika Kata ya Kisanga, kwa kutumia maporomoko ya Mto Ruvu.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, alisema katika Jimbo la Mikumi lina vijijini  vinavyopata umeme kutokea katika Kituo cha Kilosa na vingine vinapata umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha Kidatu.Malima alisema Kata za Zombo, Ulaya na Kijiji cha Mhenda, bado havijapatia umeme na kwamba Tanesco inafanya tathimini ya kujua gharama za utekelezaji wa mradi wa kufikisha umeme katika maeneo hayo.Kuhusu taasisi ya kidini kutaka kuwekeza katika mradi wa umeme katika Kata za Kisanga, Naibu Waziri alisema hilo linawezekana na kwamba kinachotakiwa ni taasisi hiyo, kuwasiliana na wizara Wakala wa Umeme Vijijini.

MARA UTASIKI MBUNGE HUYU ANALIPA KODO YA NYUMBA MILLIONI NGAPI SIJUWI MARA SPIKA HUYU ANALIPA KODI YA NYUMBA ANYO ISHI BILLIONI NGAPI SIJUWI MARA UTASIKIA MBUNGE HUYU AMEKODISHA VYUMBA 4 KATIKA HOTEL NA ANAISHI NA FAMILIA YAKE NA ANLIPA KODI BILLIONI NGAPI SIJUWI ILA KUNUNUWA VIFAA VIPYA VYA UMEME NA KUWAPA RAI UMEME WA UHAKIKA HAKUNA WANANUNULIWA MITUMBA KISHA MAKODI MAKUBWA MAKUBWA KILA KUKICHA KISHA ATI NCHI HII MASIKINI MAWE NDIO WAZENJI HATUTAKI TENA MUUNGANO MAANA TUNAJUWA HAWA VIONGOZI WA TANGANYIKA KAZI YAO KUISHI VIZURI NA FAMILIA ZAO NA HUKU RAI WANASAFA NA MAISHA NA NYINYI WATANGANYIKA MUSIAKE ENDELENI KULALA TU HIVYO HIVYO NA KUDANGANYWA ATI NCHI INA AMANI NA UTULIVU NDIO KWAKUWA WAO WANAISHI VIZURI NDIO WANA MSEMO HUO WANAHOFIA NYINYI MUNATESEKA NA KULA UGALI NA PEREGE KILA SIKU HATA HAWAWAJALI.

No comments:

Post a Comment