Wednesday, July 20, 2011

ZENJI TUNATAKA KUVUNJA MUUNGANO TANG WATAKA KWANZA WALIPWE DENI LAO LA UMEME


WIZARA ya Nishati na Madini imesema kuwa Tanesco haitaweza kulisamehe Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco) hadi utaratibu mwingine utakapofanyika, Bunge lilielezwa.Naibu Waziri wa wizara hiyo, Adam Malima alisema deni la Tanesco kwa Zeco limefikia Sh 50.4 bilioni ambalo linatokana na Tanesco na Zeco kutawaliwa na uhusiano wa kibiashara kupitia mkataba maalumu wa kuuziana umeme.Malima alisema chimbuko kuu la deni hilo linatokana na ongezeko la asilimia 21.7 la Januari 2008 kwani Zeco hawakukubaliani na maelekezo ya EWURA.Alikuwa akijibu swali la Rukia Kassim Ahmed (Viti Maalumu-CUF) aliyetaka kujua ni kwa nini Tanesco isiifutie Zeco deni ikiwa ni hatua ya kusaidiana kati ya mashirika hayo na Watanzania wa pande hizo mbili.Malima alisema kuwa madeni ya Zeco kwa Tanesco ni yanayotokana na uhusiano wa kibiashara unaotokana na makubaliano ya kimkataba baina ya taasisi hizo mbili na hivyo mikataba hiyo inatarajia patakuwa na vigezo vitakavyofafanua namna ya kusamehe au kufuta deni hilo.Alitaka kigezo kikubwa cha Tanesco kufuta deni la umeme kwa mteja ni kufilisika kama kampuni au mteja kutopatikana sehemu yoyote.Kuhusu bei ya umeme kuwa ni kubwa katika Visiwa vya Pemba na Unguja kuliko maeneo mengine, Naibu Waziri alisema tangu mwaka 2005, Serikali ilikabidhi jukumu la kupanga bei kwa EWURA hivyo ndiyo yenye majukumu hayo ambayo hupanga kulingana na namna inavyoona kati ya gharama za uzalishaji na usambazaji

HAPA NI HOSPITALI NA PIA HAKUNA UMEME AIBU GANI HII..?

No comments:

Post a Comment