Monday, August 15, 2011

BALOZI IDD SEIF ATOWA TV MIAKA 47 YA MUUNGANO YEYE ANAWAPA WATU TV HII NI 2011 BADO ANAKUJA NA SERA ZA TV NA MAPANGA HAAHAHHA

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 15th August 2011 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Idd amesema mfumo wa Muungano wa Serikali mbili ndio chachu ya maelewano na umoja uliopo miongoni mwa Watanzania.Alisema jamii ya Watanzania imeshuhudia faida nyingi za mfumo huo, tangu kuasisiwa kwa Muungano huo ikilinganishwa na kero zilizopo zinazoendelea kupatiwa ufumbuzi.Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapindizi Zanzibar (SMZ),alisema hayo alipokuwa akizungumza na mabalozi wa wadi ya Upenja katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika ziara yake ya siku tatu katika Jimbo la Kitope ambalo yeye ni Mbunge.Aliwaomba mabalozi hao kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kuongoza dola katika vipindi vyote vijavyo kwa lengo la kulinda maendeleo yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa sera za CCM.Alisema kuwa CCM inaelewa kuwa kazi ya kuimarisha uhai wa chama iko ndani ya uwezo wa mabalozi kwa vile wako karibu na wanachama na wananchi hasa vijana.Balozi Seif alitoa seti ya television kwa maskani ya CCM Upenja na kuahidi kuliwasilisha kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein suala la nguzo za umeme ambalo lilikuwa ahadi ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

No comments:

Post a Comment