Friday, August 26, 2011

PEMBA ILITOWA SHERIA MWAKA 1928 HAKUNA KUINGIZA ULEVI WA POMBE YA AINA YOYOTE

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nasir amesema Sheria ya Kupiga Marufuku Kuingiza Vinywaji vyenye Kilevi katika kisiwa cha Pemba ya mwaka 1928 bado ipo na haijafutwa.
Kamanda Nassir alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Waislamu waliokuwa wakitishia kufanya maandamano kupiga kuwepo kwa ghala la kuhifadhi vinywaji vyenye kilevi huko Tibirinzi.
Nassiri alisema sheria hiyo inapiga marufuku watu binafsi kuingiza na kuuza vinywaji hivyo katika kisiwa cha Pemba isipokuwa kwa taasisi za ulinzi tu ikiwemo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika makambi yao.“Sheria ya Kupiga Marufuku Kuingiza Kinywaji chenye Kilevi kisiwani Pemba ipo na haijafutwa…. ni marufuku kuingiza kinywaji hicho isipokuwa kwa taasisi za ulinzi tu na kinywaji hicho kipatikane katika kambi za jeshi,” alisema.Aliwataka Waislamu waliokuwa wakitishia kufanya maandamano kuwa watulivu wakati shauri lao hilo likifanyiwa kazi na taaasi husika ikiwemo vyombo vya ulinzi.
 SASA MIMI NATAKA KUMULIZA HUYU KAMANDA HASSAN NASIR JE SIKU YA KIYAMA IKIFIKA UTAMUAMBIYA MWENYEZI MUNGU KUWA JESHI TU NDIO NILIYOWARUHUSU KULEWA MAKAMBINI KWAO..?NA IKIWA SABABU (JWTZ)NDIO MAANA WANARUHUSIWA KULEWA BASI KWA NINI MUSISAJILI VIJANA WA KIPEMBA WALIO FELI DARASA LA SABA NA FOM 2 NA FOM 4 KUWA NDIO JESHI LA JWTZ HAPO PEMBA NA UNGUJA SITHANI KAMA WAO PIA WATASEMA WANATAKA ULEVI KWA HIYO HATA MAKAMBINI PIA ITAKUWA HAKUNA HAJA YA KULETWA ULEVI MAANA WEWE KAMANDA HASSAN NASIR UMEKUWA UNAIPINGA AYAA YA M/MUNGU INAYOSEMA NA WALA MUSILE NA WALA MUSIKARIBIYE SWALA NA HUKU MUME LEWA WEWE UNASEMA INARUHUSIWA MAKAMBINI TUU JE UNA WAHALALISHIA ULEVI SIO KAMANDA HASSAN NASIR..?

No comments:

Post a Comment