Monday, August 1, 2011

VIONGOZI WA CCM Z;BAR WANAOTETEA SEREKALI MBILI NI WATUMWA WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA .

Makamu Mwenyekiti wa CUF Zanzibar, Machano Khamis Ali, amewafananisha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na watumwa kwa kutetea mfumo wa serikali mbili katika Muungano wa Tanganyika na visiwani.Akizungunma na wananchi wa Mkokotoni, nje kidogo kutoka mjini hapa jana, Machano alisema anawashangaa viongozi hao wanatetea mfumo huo, huku wakiungana na wananchi wengine kudai Katiba mpya inayozingatia utaifa wa Zanzibar.“Nazungumza hili wasikie CCM, wanaotaka serikali mbili, muwaone kama sumu, sio sumu hii ya samaki aina ya Bunju.. sumu hatari ya “chini” isiyokuwa na dawa,” alisema Machano.Alisema viongozi hao ni sawa na watumwa wanaofanyakazi ya kutetea mambo ambayo wenyewe rohoni mwao hawayapendi.Machano alisema anafuatilia sana vikao vinavyoendelea Dodoma na Zanzibar vya Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi, kauli za Wabunge na Wawakilishi wa CCM na CUF zinaonyesha mshikamamo wao katika kutetea utaifa wa Zanzibar.Akitoa mfano, alisema Mansour Yusuf Himid, ni kiongozi wa ngazi ya juu wa CCM na waziri katika serikali ya umoja wa kitaifa, amepinga mfumo wa serikali mbili ndani ya kikao cha baraza, akiwataka Wazanzibari kuweka kando ukereketwa ili kuungana katika kudai haki ya Zanzibar kwa njia ya kutoa maoni juu ya Katiba mpya.
Machano alisema viongozi wa CCM wanaotetea serikali mbili kwa maelezo kuwa, mfumo huo ndio sera ya chama chao, wanapingana na viongozi wa serikali ya mapinduzi.“Ilani gani, wakati viongozi ndani ya serikali ya mapinduzi wanataka serikali tatu,” alisema Machano na kuongeza kuwa, CCM Zanzibar hawajui kwamba CCM bara nia yao ni serikali mbili, hata kama wanaumia kuibeba Zanzibar, lakini watafarijika kwa kuipotezea utaifa.Mbali na Waziri Mansour, Waziri wa Fedha, Omar Yusuf Mzee, akitoa ufafanuzi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi juu ya uwakilishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano, alisema hakuna hata chombo kimoja ambacho bodi yake inaongozwa na Mzanzibari, ingawa Zanzibar ina wataalam wengi, akiwemo yeye.“Tatizo ni mfumo, kila moja, pamoja na wawakilishi tushiriki kuwahamasisha watu wetu kuboresha Katiba,” alisema Mzee.Juu ya mchango wa wananchi katika kudai haki ya Zanzibar katika Muungano, Machano aliwataka Wazanzibari kushiriki katika mchakato ujao wa kutafuta maoni yao juu ya rasimu ya mapitio ya Katiba mpya.

No comments:

Post a Comment