Friday, September 16, 2011

CUF YATOWA TAKWIMU MPYA YA WATU WALIYO KUFA KTK KUZAMA KWA MELI NUNGWI

WATU WALIO KUFA PEKE YAKE  GANDO 418
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE KOJANI 108
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE MICHEWENI 88
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE MGOGONI 184
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE WETE 149
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE MTAMBWE 214
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE KONDE 96
WATU WALIO KUFA PEKE YAKE MTAMBILE 100

WAKATI habari zikisema Waziri wa Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hamad Masoud Hamad, amesema yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake kutokana na ajali ya meli ya Spice Islander iliyozama hivi karibuni katika eneo la Nungwi na kuua mamia ya watu, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema watu waliokufa katika ajali hiyo, ni zaidi ya 1696.Waziri Masoud, ambaye ni mwanachama wa CUF, alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na BBC jana, akasema kuwa uamuzi wa kuwajibika ni jambo jema kwake, ila anangoja ripoti ya tume inayochunguza kiini cha ajali hiyo. Lakini chama chake kimemtaka ajiuzulu kabla ya tume kufanya kazi yake.Hamad alisema kwa sasa anasimamia jukumu la kuopoa miili ya watu waliokwama kwenye meli hiyo. Wazamiaji kutoka Afrika Kusini wapo Zanzibar tangu juzi, lakini wameshindwa kufanya kazi ya kuopoa miili hiyo kutokana na kuvurugika kwa hali ya hewa katika eneo la Nungwi mahali ilipozama meli ya Mv. Spice Islander.“Kuwajibika ni jambo jema, na nitafanya hivyo kama kuna uzembe ulitokea katika wizara yangu pamoja na vyombo vilivyo chini yangu lakini katika hili hebu tuvute subira kidogo kwani hivi sasa tunafanya juhudi za kuhakikisha mabaharia wa uokoaji kutoka nchini Afrika ya Kusini wafanye kazi, nami nikiwajibika katikati ya janga hili nitakuwa sijatenda haki,” alisema Hamad.
Mmoja wa viongozi waandamizi wa CUF aliliambia gazeti hili: “Kama atajiuzulu atakuwa ametusaidia sana.” Juzi Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo, hata kama hakuhusika katika janga hilo.Mtatiro alisema pamoja na CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa muda wa mwaka mmoja sasa lakini ni jambo la hatari kwa wizara inayoongozwa na waziri anayetoka Chama hicho kufanya uzembe huo kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.
“Japokuwa Chama chetu cha CUF tupo katika serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini hili ni jambo la hatari kwa Wizara inayoongozwa na waziri wetu kufanya madudu haya hata kama alikuta utamaduni wa ‘ku-overload’ umezoeleka alipaswa kulisimamia hili na kuliondoa kwa haraka” alisema na kuongeza kuwa ni vema aachie ngazi hata kama hakuhusika na janga hilo zito kwa Taifa.Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF ameshauri serikali impumzishe Waziri Hamad badala ya kungoja ashurutishwe na nguvu ya wananchi.Alisema uzito wa janga hilo unaondoa suala la ushabiki wa vyama, badala yake ni kujali na kuthamini maisha ya watu Wakati suala la kujiuzulu kwa waziri huyo likiwa bado bichi, CUF kimetoa takwimu mpya zinazoonesha kuwa watu waliokufa katika ajali ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba 12, mwaka huu ni 1696, si 203 kama ilivyotangazwa na serikali.Wabunge wa CUF wenyeji wa Pemba wamesema wamehakiki na kuthibitisha idadi hiyo kwa siku tatu mfululizo.Mbunge wa Jimbo la Ziwani Ahmed Juma Ngwali amesema Jimbo la Gando ndilo linaloongoza kwa kupoteza watu 418 katika ajali hiyo.“Bado tuna kazi nzito na kila nyumba tunayoingia ni msiba. Jimbo langu peke yake ni zaidi ya watu 182 hadi sasa hawajaonekana. Watu wameshakata tama ya kuwaona ndugu zao.”CUF imesema Jimbo la Kojani watu waliopoteza maisha ni 108, Micheweni watu 88, huku Jimbo la Ole anatoka Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Hamad Maoud Hamadi, likiwa limepoteza watu 157.Jimbo la Mgogoni limepoteza watu 184, Wete 149, huku Jimbo la Mtambwe analotoka Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seifu Sharif Hamad, likidaiwa kupoteza watu 214. Nalo Jimbo la Konde watu 96 wanadaiwa kufa, Mtambile ni 100.Kutokana na takwimu hizo zinazofanywa na wabunge hao nyumba kwa nyumba watu 1696, wanaodaiwa kuwamo katika meli hiyo hadi sasa hawajaonekana na wanahofiwa kupoteza maisha.Takwimu hizi mpya za CUF zimezidi kutia shaka juu ya idadi kamili ya abiria waliokuwa katika meli hiyo. Awali, serikali ilisema idadi ya watu 816 ndio waliokuwa ndani ya meli siku ya ajali. Hata hivyo, baadhi ya watu wawakiwemo wanaodaiwa kuwa ndugu wa marehemu wanadai kuwa watu 3,000 walikuwa ndani ya meli hiyo siku ya ajali.Wakati huo huo, watu saba wamenusurika kufa baada ya boti yao ya mizigo kuzama. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Bugi, amesema boti hiyo iliyokuwa ikitoka mkoani Tanga kwenda Pemba ilizama alfajiri ya jana, ambapo boti ya polisi ilifanikiwa kuwaokoa watu hao.

DR SHEIN UKILETA UPUMBAVU NA WEWE PIA UTAJIUZULU WACHENI KUFICHA FICHA MAMBO SISI TUSHA POTEZA DUNGU ZETU JAMAA ZETU RAFIKI ZETU TUPENI UKWELI JAPO UNAUMA AU TUTAISHENIKIZA SEREKALI NZIMA YA GNU MUSITULETE UPUMBAVU
Msiba
HIZI NI BATHI TU YA MAITI ZILIZO OKOLEWA NA WAVUVI WA SAMAKI BADO ZILIZO JAA NDANI YA MELI AMBAZO ZIKO CHINI YA BAHARI NA KM KM IMESHINDWA KWENDA KUZITOWA MAITI CHINI HUKO KWENYE MELI ILIYO ZAMA BAHARINI MPAKA WASOUTHA AFRICA WAMEKUJA KUZITOWA MAITI HUKO CHINI PIA HAPA ILIKUWA KUWE NA MANURSE NA COAST GUARD LIKINI UNA PICHA HAPA MAJESHI WAKITANGANYIKA WATUPU MOJA YA UTHIBITISHO KUWA TUMETAWALIWA TUKITAKA TUSITAKE SISI TUKO CHINI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MELI IMEZAMA MAJIRA YA SABA USIKU MPAKA ASUBUHI NDIO ATI SEREKALI NA MAJESHIWAKE WANAO TUTAWALA KWA MABAVU NDIO WALIPOWASILI USIKU KUCHA NI WASWALIHINA NA WAVUVI NDIO WALIO FANYA KAZI YA UWOKOWAJI JE SISI TUNA SEREKALI AU YAGUJUUUUUU....??????????

No comments:

Post a Comment