Monday, November 21, 2011

SITTA NA MAJINAMIZI WENZAKE HOI BEN TABANI NCHINI ZANZIBAR

 “Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano”.
  • Wajumbe wa Baraza wamchachafya
  • Atakiwa alete Katiba ya Tanganyika
  • Wengine wakerwa na “Uwaziri wa Rais”
Na Waandishi wetu,free Zanzibar people from mkoloni mweusi.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na mazingira magumu ya pingamizi juu ya Muswada inayousimamia.
Muswada huo ni ule wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 uliowasilishwa wiki hii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma, na Waziri Celina Kombani, na pia kujadiliwa katika vikao mbali mbali vya kitaifa na vya kijamii.Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Waziri wa Afrika ya Mashariki, Bw. Samwel Sitta, ilikutana na mazingira hayo katika Semina Maalumu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, iliyofanyika mwanzoni kabisa mwa wiki, ndani ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Mnazi Mmoja mjini hapa.“Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano”.
Ni Kifungu cha 132 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Toleo la mwaka 1995 ambacho takriban Viongozi wote wa Serikali na wa Kisiasa waliochangia katika Semina hiyo walikinukuu usoni mwa Kamati ya Mhe. Sitta.Wawakilishi walikitumia pia Kifungu hicho cha 132 (2) kinachotamka “sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika”.Wawakilishi walitumia Vifungu hivyo vya Katiba wakisisitiza msimamo uliochukua sura ya kushikamana miongoni mwa pande zote za kisiasa, pamoja na wenye nyadhifa za juu za Serikali, kueleza kile umma wa Wazanzibari wanachohitaji sasa.
Miongoni mwa waliolitumia jukwaa la semina hiyo ni pamoja na Waziri wa Kilimo Bw. Mansour Yussuf Himid, ambaye kwa maneno ya mkato alisema, kuja kwa muswada huo wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi kunaambatana na maamuzi halali ya iwapo wenye mamlaka ya kuitetea Zanzibar sasa watafanya hivyo au wataitelekeza kwa kushindwa kuinasua na ili ije kuwa lawama kwa vizazi vijavyo.Waziri wa Nchi, Mstaafu, wa Afisi ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mjini Unguja, Bw. Hamza Hassan Juma, akitumia vifungu hivyo vya Katiba, alisema, iwe iwavyo kwa mujibu wa heshima ya kisheria, na kwamba licha ya juhudi za kuuimarisha muswada huo, kwa mashirikiano baina ya Serikali mbili, lazima ieleweke kwamba upande wa Visiwani utakuwa na maamuzi yake.Alisema kwa minhaji hiyo hapatakuwa na nafasi ya kuburazana tena wala kuudhoofisha upande huru wa Jamhuri ya Muungano kama ilivyokuwa hapo kabla, yaani upande wa Zanzibar.Naye Mwakilishi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar, Bw. Ismail Jussa Ladhu alisema, pamoja na ulazima wa kuurejesha Muswada huo ili Wazanzibari nao wachukue maamuzi yao ijapokuwa kwa utaratibu wa thuluthi mbili za Wajumbe wa Baraza hilo, lakini pia wao kama Wawakilishi wa wananchi wanawasilisha hoja na matakwa ya msingi ya watu wa Visiwa vya Unguja na Pemba juu ya Muswada huo.Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na kuitaka Kamati ya Bw. Sitta na mamlaka zake kwanza kuitafuta Katiba ya Tanganyika ili kuweka mazingira fasaha ya kujadili Muungano wautakao sasa wananchi wa Zanzibar na huenda Tanzania kwa ujumla.Waliochangia na kusisitiza hoja hizo ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar , Bw. Ali Mzee Ali, na pia Katibu wa sasa wa Baraza hilo , Mwanasheria Ibrahim Mzee.Pamoja na hayo katika hoja iliyoleta hisia za aina yake ni pale kwa masikitiko na hali ya kusononeka alipoibuka Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar , Bi. Asha Bakar Makame.Mwakilishi huyo ambaye aliwahi kushika Wadhifa wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Vijana wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Zanzibar, alisema ni jambo la kuhuzunisha na ambalo si rahisi kuzituliza nyoyo za umma wa Wazanzibari, kumuona Rais wa Nchi huru ya Zanzibar akiapishwa kushika cheo cha uwaziri tena hata usio na wizara maalumu ya Jamhuri ya Muungano, alisema “hili linauma sana”.Kwa ujumla kuwapo kwa hoja hizi na namna Viongozi na Watendaji mbali mbali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, walivyosimama juu ya msimamo mmoja wa kujali haki na utaifa wao, ni kama kwamba kulipelekea Mhe. Sitta na Kamati yake kuondoka na nyoyo zilizosinyaa, huku wakiamini kuwa sasa Wazanzibari hawatanii katika kuidai nchi yao

No comments:

Post a Comment