Wednesday, November 23, 2011

TAARIFA YA MAANDAMANO YA KUPINGA MUUNGANO NA ZANZIBAR KUWA NCHI HURU

UHURU WA NCHI YETU YA ZANZIBAR KWANZA,KUJITAWALA WENYEWE KWANZA,ZANZIBAR KWANZA TUSHIKANE SOTE WAZANZIBAR WALIO NJE NA TULIOKUWEPO HAPA ZANZIBAR PIA EKA PEMBENI KILA KITU TUJIKOMBOWE KWANZA KATIKA MIKONO,DOMO,JITUMBO,MIKUCHA YA WAKOLONI TANGANYIKA
Kundi la Wazanzibari leo hii imefika ofisi za UN Mjini Zanzibar na kuongozwa na Rashid Salum Adiy kutaka Zanzibar itambuliwe kuwa ni nchi na kwamba Muungano si halali
TAARIFA KWA WAZANZIBARI POPOTE PALE WALIPO JUU YA SUALA LA MAANDAMANO YA KUPINGA MUUNGANO WA KISIASA WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Uwongozi wa ZARFA unawaarifu Wanzanzibari wote kwamba matayarisho ya maandamano yanaendelea. Hivyo kila Mzanzibari anaeipenda Nchi yake ajitayarishe kushiriki kwa hali yoyote pale siku itakapo tolewa taarifa rasmi ya maandamano yatakayokuwa na mfumo maalumu endelevu kama ifuatavyo:-
  1. Polisi wakikubali kuja kutulinda yatakuwa ni maandamano ya amani na yenye mpango maalum.
  2. Polisi wakikataa kuja kutulinda na wakikusudia kuja kuvunja pia yatakuwa ni maandamano ya amani na yatakuwa na utaratibu maalumu katika kufanyika kwake ndani ya Zanzibar.
  3. Wazanzibari waliyo nje ya nchi watakuwa na utaratibu maalum wa kuunga mkono siku hiyo namna tutakavyo waarifu Wazanzibari nyote tunakuombeni muwe na subira kidogo ili tuje tufuzu.

No comments:

Post a Comment