Tuesday, December 6, 2011

VIONGOZI WA ZANZIBAR PELEKENI UJUMBE HUU DODOMA NA NCHINI TANGANYIKA WAAMBIYENI WAZANZIBAR-HATUTAKI MUUNGANO


KARUMA NA NYERERE WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZI
KISHA WANASEMA ANATIA SAINI YA MUUNGANO MAWE
WATANGANYIKA MUNA MASIKIO YA CHINI NINI TUSHASEMA HATUTAKI MUUNGANO,HATUTAKI MUUNGANO,HATUTAKI MUUNGANO.

Jamani hamuoni mbali, munaangalia karibu mbele yenu tu. Kwanza siungi mkono kuwa tuijadili katiba na makubaliano ya muungano.MAANA TANGANYIKA HAIPO SASA VIPI TUNAJADILI KATIBA NA MAKUBALIANO YA MUUNGANO...?? Halafu wanalete hili suala la katiba ili kutupotezea lengo la muungano. Sisi tunachokitaka ni kuondoka muungano kabisa. Kutokana na kauli zao za kipuuzi na kijeuri kina Kikwete na wenzake, sasa hatutaki tena kujadili muungano wala katiba. La msingi ni sisi kuingia barabarani tu kama kuna kibali au hakuna maana sasa imekithiri mno.

Niliposema kuwa hatuangalii mbali nakusudia kuwa kura ya maoni kwa sasa haina hadhi kwa sisi Wzanzibari. Nifahamuvyo mimi ni kwamba kwa sasa Zanzibar kuna wahamiaji wengi kutoka bara na hao hawakuja kwa kwa bahati mbaya tu, bali wamekusudiwa.kuletwa kwa makusidi ili wazanzibar tukidai haki ya nchi yetu watulete kwanza jadilini mswaada hatukutaka watasema basi kura ya maoni maana wanajuwa kuwa washawajaza watu wa hapa zanzibar kwa hiyo hao watasema wanataka muungano kwa hiyo wazanzibar tutakuwa tushamezwa na tukumbuke kuwa Wao ndiyo wanaopewa vitambulisho vya Zanziabar na wananyimwa Wazanzibari wenye haki. wao ndiyo watakaosema kuwa muungano uendelee. Mimi nawapinga wale wanaotaka kura ya maoni kwa sasa hivi. Tutakuwa tumejipaalia makaa kipweza.
Mrfroasty suala la sheria na wanasheria kwa sasa halikubaliki kwani hata huo muungano asili haukuwa wa kisheria. zile picha zinazo oneshwa kuwa Karume anatia saini siyo kweli kuwa anatia saini ya muungano, inaweza kuwa anatia saini kitabu cha maombolezi au cha wageni. Siki ya kutia saini mkataba alitakiwa mwanasheria wa Zanzibar siku hizo, DAURADO awepo, lakini aliotewa yuko nje ya nchi ndiyo akapewa karume makaratasi atie saini bila kujua kilichomo na aliharakishwa ufanya hivyo na nyerere kabla Dourado kurudio. Kwa hiyo suala la kuwa tuende na sheria na wanasheria litoke vichwani mwetu kama kweli tunataka Zanzibar yetu. halafu matokeo ya kufuata sheria ni haya tunayoyaona kuwa kila siku danganya toto tu huku tunazungumzia muungano wao wanazungumzia katiba what the hell is this!!!!
Kama tunataka nchi yetu tuache maneno na tudai Zanzibar na siyo kujadili katiba na muungano. Tuingie njiani kama walivyofanya wamisri. Tuingie huku tukiwa tumejitayarisha kwa lolote na pia kwa jina la ALLAAH.

SOTE ZANZIBAR NZIMA NASEMA ZANZIBAR NZIMA TUSEME KWA SAUTI MOJA. HATUTAKI KURA YA MAONI,HATUTAKI KUJADILI KATIBA NA HATUTAKI MUUNGANO TUNATAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR IWE NCHI HURU.

HAYA NDIO MANENO YA KUSEMA KAMA KWELI TUNAITAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR M/MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA KIZAZI CHAKE CHOTE AMIIIIIIIIIIIIIIIIIIINI

No comments:

Post a Comment