Thursday, December 22, 2011

KAMA ABOUBAKAR YUMO KWENYE KUNDI LA HAMA(HR)BASI WAZENJI TUWE MACHO KWELI KWELI.

IMG_0100
Ndugu zangu Wazanzibar ikiwa tetesi zinasema kweli kuwa kuna kundi la watu wanaomunga mkono Hamad Rashid katika vita vyake na  Aboubakar yumo basi TUWE MAKINI KWELI KWELI MAANA WANAWEZA KUMTUMIYA HUYU KUTUMALIZA KWENYE KATIBA WANAYOTAKA KUILETA ZANZIBAR NA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA WILAYA YA PWANI WAZENJI TUWE MAKINI KATIKA JAMBO HILI.Mimi binafsi sijawa na uhakika kamili lakini tujihadhari kinga ni bora kuliko tukaja kujuta kama tunavyojuta sasa kuwa kwa nini father karume aliungana na hawa. hakuna mtu hata moja alio tegemea kuwa Hamadi HR, Jidawi, Salum Msabaha wanaweza kutugeuka kwa matamanio tu yakidunia (kuhongwa vijipesa)Sasa na huyu Abou inasemekana ni mtu mwepesi wa kipato sasa isije ikawa katika tetesi za kuhongwa millioni mia 700 alizo pewa Hamadi na best Friend wake Mizengwe Pinda ikawa na Abou yumo?. Itakuwa hatari kwa Zanzibar .Maana  Hamadi anajinata kuwa anao wenzake nyuma ya Pazia sasa Wazanzibar tuweko alart na tetesi kuzipuuza, kuna siri nyingi tu nyuma ya pazia moja ni kesi ya Mkapa kusema Cuf watamfungulia mashataka katika mauwaji ya 2001 tarehe 26/27.aliyo yafanya zaidi ya dungu zetu na hatujamsamehe mpaka na yeye apelekwe mahakamani kwa kuuwa rai wasi na hatia.Hii inasemekana  Hamad Rashid alikula hongo na akaifificha(kuizima) kesi hii ili isije juu na alikuwa sio peke yake kwa hio Wazanzibar imekuwa hutolewa chambo kwa kuwanufaisha wachache katika maslahi yao binafsi.Sasa hofu ya Wazanzibar hivi sasa ni huyu Abou jee huyu ni Aboubakari Sadiki kweli au ni wa Magogoni..?Kama sie basi ashughulikiwe haraka kabla haja tuweka pabaya Wazanzibar na katiba ijayo ya unafiki wa kuitaka kuimeza zanzibar hatuna haja ya katiba tunahaja ya kuvunja muungano tu basi, maana viongozi wa Tanganyika hawaoni tabu kutowa million 700 au zaidi lakini tu lau lipite, hii kwao ni pesa ndogo tu hata kodi ya siku haifiki ni kama pesa ya kununuwa chapati na namaharangwe pale gerezani asubuhi sio jambo kubwa.Na hutumia ujanja hivi sasa wa kurubuni vile viungo muhimu ili mambo yao yawe, kuna mifano mingi tu hivi sasa ya kuwalahai Wazanzibar ili kero za Muungano zizimike mfano.
Hivi sasa utaona katika misafara mingi ya njee huchukuliwa Wazanzibar moja au wawili tena cuf ili wajihisi wamefadhiliwa waje kulipa fadhila kwa watawala wa Tanganyika wazitakapo.lakini zanzibar ikijitawala hizo safari zitakuwepo tena nyingi sana kuliko hizo wanazozitowa wakoloni wausi tanganyika tena zitakuwa za hishima zaidi maana mutakwenda kama nchi kamili inayojulikana umoja wa kimataifa sio uchochoro wa jumanne pale mtendeni kupata supu chapati.kwa hiyo viongozi amkeni.Hii ilikuwa zamani hakuna safari za kimataifa ni wao tu Watanganyika Wazanzibar haziwahusu kama vile sio sehemu kubwa ya huo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupatikana Tanzania.Tulikwishazowea Wzanzibar kuwa sisi tasisi za kimataifa hatushirikishwi ,sana ukienda katika tasisi hizo utakuta kuanza juu mpaka chini ni wao tu akina John,Lukasi,Jalome etc lakini humuoni Mzanzibar.Hii ndio iliotusababisha Wzanzibar kusema hakuna faida ya nchi yetu kuitika katika Muungano usio fanya haki upande moja, na tulihisi kuwa Wazanzibar tumepoteza pakumbwa nchi yetu kungana.Hali yakuwa Zanzibar ilikuwa Dola huru na lenye mambo yeke ya ndani na njee ya kimataifa sasa vipi leo tuhukumiwe ki-mkoa kwa udogo wa nchi yetu na watu wake.pia tukumbuke father karuma alisema ni wa miaka 10 tu vipi leo umefikia miaka 47...?Zanzibar ni taifa (Dola) na sio wilaya wala Kata, huwezi kulinganisha Zanzibar na Arusha au Mbeya kwa kuwa ina watu wengi. thamani ya Zanzibar kimataifa na ki historia ni kubwa .Hatujawahi hata siku moja kusikia Arusha au Iringa ikawa na kiti chake umoja wa mataifa (UN).lakini zanzibar inacho kiti na walisima ni kanchi kadogo na tukawaonyesha kuwa ni nchi na ilikuwa ktk (UN)Sasa Zanzibar kui Treaty kama Mkoa kwa kigezo kuwa ina watu kidogo na ardhi ndogo hatuko tayari na sasa tulipo fikia hata wageuke kuwa wema na kusema OK OK ni nchi hatutaki tena nibora tuvunje Muungano na tubakie na ujirani mwema lakini katu hatuto salim amri au kuisalimisha Dola yetu.Kuna viongozi wengi tu wa ki-Tanganyika wakizani Wazanzibar ni ma-Foolish yaguju, wakisema maneno yakifedhuli na tharau kama vile kusema kijisehemu kidogo chenye watu kidogo kuliko hata Manzese kinataka haki sawa .Kuna badhi ya Wabunge wa Tanganyika wakifananisha majimbo yao eg kuwa na watu wengi mfano wao kama Murogoro kuwa na watu zaidi ya million 2 hali yakuwa Mbunge ni mmoja.Vipi Zanzibar ina watu million 1 ina wabunge zaidi ya 68 , huu ni upumbavu na ujinga wakutufanya sisi foolish, wao hawaoni kuwa Zanzibar ni nchi..? Na bila ya Zanzibar kusingalikuwa na huo Muungano uitwao wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.Na kama wanatuhukumu kutokana na idadi ya watu wetu na ardhi yake mbona Ushelisheli nchi yenye watu wasiopunguwa laki moja wana kiti cha kudumu umoja wa mataifa wala hawakuambiwa nyiyi hamupewi kwa udogo wenu, au marekani yenye nchi 54 zilizo ungana kuwa na kiti kimoja..?Huu ni ujinga na ufethuli wakutaka tusalimishe nchi yetu kwa udogo yaguju mukitaka nilazima muheshimu kuwa Muungano ni wanchi mbili Tanganyika na Zanzibar na katika Muungano hakuna mkubwa wala mdogo tumeungana sote ni nchi zilokuwa na Dola zake.na sasa imekuwa tafashaa tu kwa hiyo nauvunjike.Misituone kuwa Wazanzibar mabwege tunaweza kuwa foolish yaguju Wazanzibar tunajuwa kitugani tunafanya na tumesoma sio vichwa maji, maana hujinata kuwa sisi watanganyika tumesoma Bongo man? Lakini isabu fupi tu katika watu millioni 1 Zanzibar wasomi walio hitimu masomo ya juu niwangapi..? na millioni 44 za wa Tanganyika niwangapi walio soma= utapata wapi pumba...? Kwa hio Wazanzibar wengi ni wasomi na hatuko tayari kupumbazwa na nyinyi kwa kutufanya foolish tumieni ujanja wa kuwarubuni watapia mloo akina Hamad lakini tukiwabaini Wazanzibar wenye kutusaliti basi tunawatosa na kuwafanya wasi.
Maana inashangaza kuwa kila siku muna mipango mipya ya kuihujumu Zanzibar kwa njia hii au nyingine, alipo kuwepo Baba wenu wa Taifa mulitufanyia vitimbi vingi sasa kafa waliobakia wanaviendeleza.
Wazanzibar tuko macho na hatuko tayari kuhujumiwa enough is enough umetokea mzozo wa Hamad na Maalim nyinyi mumeuvalia njuga kutia moto petrol(fitna) ili ndugu kwa ndugu wafarikiane.hakuna munalolijuwa zaidi ya kufitinisha watu.Sasa chakujiuliza lengo lenu nini? Kama sio ubaya wa roho na kutaka Zanzibar na wazanzibar wasiwe watulivu.Mizengwe mingi tu yakutugonganisha vichwa mulitufanyia na ikawa Zanzibar haikaliki na kupandikizwa chuki na kuja kutuuwa kwa jeshi la wakuria sasa tumesha tulia tunavuta harufu ya amani na ya marashi ya karafu hao mushasimamisha mishipa ya fitina munachokora jengine.m/mungu atawashinda kwa ubaya wa roho zenu mulizo nazo kwa kuioneya choyo nchi yetu ya zanzibar.Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote na uwalani wale maaduwi wa Zanzibar.

Wednesday, December 21, 2011

MAALIM SEIF ASEMA-MSIOGOPE KUITWA WAISLAMU

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia uwanja wa Taifa katika hafla ya kuchangia kituo kimoja cha televisheni cha kiislamu.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza Waislamu nchini kote kujitokeza kwa wingi kuchangia uanzishwaji wa kituo cha televisheni kiitwacho Imani, kwa sababu televisheni hiyo itatoa mchango mkubwa kufuta dhana potofu dhidi ya Uislamu, na kutoa taaluma ya maadili mema ndani ya jamii.
Alisema hayo leo alipokuwa akihutubia kwenye hafla ya kuchangia uanzishwaji wa televisheni hiyo, inayoanzishwa chini ya Jumuiya ya Islamic Foundation, ambayo pia inaendesha Redio Imani iliyopo mkoani Morogoro. Maalim Seif alisema vituo vingi vya televisheni hapa nchini mara nyingi huonesha vipindi vinavyokwenda kinyume na maadili mema ya jamii, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia kuharibu maadili ya jamii na zaidi vijana na watoto wadogo.
Makamu wa Kwanza wa Rais alisema mbali ya kujenga maadili mema kituo hicho cha televisheni pia kitaweza kufanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wanajamii, juu ya mazuri na mchango wa Uislamu na kufuta dhana inayoenezwa na baadhi ya watu, dhana ambazo zinapotosha na kuipaka matope dini ya Kiislamu.
“Waislamu jitokezeni kuchangia mambo ya kheri, kuanzishwa kwa televisheni hii ni jambo la kheri, wafanyakazi serikalini, Mashirika ya Umma na taasisi binafsi changieni, na wala msione haya kujuilikana nyinyi ni Waislamu, Uislamu ndio dini sahihi” alisisitiza Maalim Seif.
Alieleza kuwa wapo waislamu wenye uwezo mkubwa na nafasi ya kuchangia mambo kama hayo yenye faida kwao na Waislamu wote, lakini kuna wengi miongoni mwao , licha ya kuwa na uwezo huo wamekuwa wagumu kutoa, na badala yake kujikita zaidi katika kuchangia mambo ya anasa.
Katika hafla hiyo, Waislamu mbali mbali walijitokeza kuchangia ambapo, Makamu wa Kwanza wa Rais alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo hicho cha televisheni. Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Ali Basaleh alisema vyombo vingi vya habari nchini, vikiwemo vituo vya televisheni havina tabia ya kutangaza mambo mema yanayogusa Uislamu na Waislamu, na badala yake vyombo hivyo vimekuwa vikijikita zaidi kuripoti mambo mabaya dhidi ya Uislamu na kuyapa umuhimu mkubwa.
Basaleh alieleza kwamba televisheni hiyo ya Kiislamu ikianza matangazo yake itasaidia kutangaza na kutoa taaluma juu ya mambo ya Uislamu, ikiwemo kufuta dhana hizo potofu zinazoupaka matope Uislamu. Mkurugenzi wa Islamic Foundation, Sheikh Arif Nahad alisema Waislamu wakiamua wanaweza, kwasababu hivi sasa wameamka baada ya miaka mingi ya kujiweka nyuma na kufunga mikono katika shughuli za kimaendeleo.
Sheikh Nahad alieleza kuwa hakuna sababu televisheni hiyo ishindwe kuanza, na kwa kuwa jumuiya yake imeahidi itatekeleza hilo na kuwaahidi mamia ya watu waliohudhuria kuwa televisheni hiyo ipo njiani inakuja.

Wednesday, December 14, 2011

CUF WATWANGANA VIBAYA SANAA JE HAMAD RASHID NI ABDURAHMANI BABU WA PILI WA ENZI HIZI...?


VUGURU kubwa zilizosababisha kuharibiwa kwa magari na watu kadhaa kujeruhiwa  vibaya zilizuka jana kati ya makundi mawili ya wafuasi wa viongozi waandamizi wa  Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Jimbo la Wawi,  Hamad Rashid Mohamed.Mapigano hayo makali yalizuka baada ya kundi kubwa la vijana walinzi maarufu ‘Bluu Gurds’ waliokuwa wamebeba mapanga, visu na nondo kutoka makao makuu  ya CUF kuvamia ziara ya mbunge huyo eneo la Mabibo, Dar es Salaam wakiwa  na nia ya kuzuia mikutano yake.Tanzania Daima lililokuwa katika eneo hilo, lilishuhudia kundi hilo la vijana  lililowasili katika eneo la Mabibo kwenye Tawi la Chechnya ambako Hamad Rashid  alikuwa akitangaza nia ya kuwania Ukatibu Mkuu, na kuanza kumshusha kwa nguvu  kutoka katika jukwaa alikokuwa akihutubia.Hata hivyo, kitendo hicho kiliwaudhi wanachama na wananchi wengine waliokuwa  wamefurika katika mkutano huo, ndipo mapigano yalipoanza kwa kurushiana mawe, mapanga na  kila aina ya silaha iliyoonekana kuwa karibu kutumika.Katika vurugu hizo  ambazo hakukuwa na ulinzi wowote wa askari polisi kinyume  cha ilivyotarajiwa na wengi, vijana wa Bluu Guards walizidiwa nguvu na gari lao  likaharibiwa vibaya kwa kupigwa mawe.Aidha, mwanachama mmoja wa chama hicho aliyejulikana kwa jina la Adam Edo,  alikatwa mkono na kuachwa ukiwa unaning’inia na kukimbizwa katika Kituo cha Afya  cha Muna  kwa huduma ya kwanza, kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa  matibabu zaidi.
Mara baada ya kutulia kwa mapigano hayo, mbunge huyo alilaani kitendo cha  kuvamiwa na kundi la wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, akisema kuwa   ataendelea na dhamira yake ya kugombea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CUF, ikiwa ni  pamoja na kukifufua chama hicho ambacho alidai kuwa kimedodora.
Alisema endapo atagombea na kupata nafasi hiyo atahakikisha anafanya  mabadiliko ya katiba ambapo mwenyekiti atakuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati  ya utendaji ya taifa na kiongozi mkuu wa chama tofauti na ilivyo katika katibaya sasa.“Mimi nitahakikisha kuwa chama kinakuwa kama taasisi na sitofanya maamuzi  yangu mwenyewe kama ilivyo sasa ambapo viongozi wanaamua lolote bila kufanya  mikutano wala kuwashirikisha viongozi wengine,” alisema Hamad.Mapigano hayo yamethibitisha mgogoro wa siku nyingi uliopo, ambao umefanya  chama hicho kuanza kumeguka vipande vipande.Habari za uhakika zimebainisha kuwa viongozi hao sasa wameamua kuanza  mapambano rasmi ya kuwania uongozi, ambapo wakati Hamad Rashid anaanza ziara za  kampeni katika mji wa Urambo, mkoani Tabora Desemba 15, kabla ya kwenda Mkoa wa  Singida Desemba 17, Maalim Seif atakuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Na wakati huo huo Ismail Jussa, Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, amesema kinachojitokeza katika mzozo uliopo sasa ndani ya Chama hicho ni Mhe Hamad Rashid, kutumikia utashi na tamaa binafsi na maslahi ya baadhi ya watu ambao wanamsukuma kuleta mkorogano ndani ya Chama. ‘Lakini wanachama wamemuelewa, hawakubaliani nae kabisa katika mtazamo wake’, alisisitiza Jussa.
Akihojiwa na Sauti ya Ujerumani katika matangazo yake ya jana (Jumatatu Disemba 12,) Ismail Jussa alisema kinachoshangaza ni kuwa Mhe Hamad Rashid, mtu anaekifahamu vizuri Chama tokeo kilipoanzishwa, kuamua kutaka kuleta mkorogano. Jambo ambalo linaonekana linalengo la kutaka kuvuruga Maridhiano yaliyofikiwa baina ya Maalim Seif na Rais wa Zanzibar msataafu Dr Aman Karume.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF, alikwenda mbali na kudai kuwa wanazo habari kuwa Hamad Rashid katika siku za hivi karibuni, amekuwa na usuhuba mkubwa na kiongozi wa juu wa Serikali ya Muungano (bila kumtaja jina) na kuongeza kusema kuwa Chama (CUF) wanapata habari.Kuhusu madai ya Hamad Rashid, kutaka kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Mhe Jussa ambae pia ni Muwakilishi wa Mji Mkongwe, alifafanua katika KATIBA ya CUF kila mwanachama anayo haki kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chama kwa kufuata utaratibu.Aidha alisema CUF, itaingia katika mchakato wa uchaguzi kwa ngazi mbali mbali kuanzia mwaka 2013 kwa ngazi za matawini na kufikia mwaka 2014 kwa ngazi ya Taifa. “Kama Mhe Hamad Rashid, ana nia njema na hoja yake ilikuwa asubiri Chama kitakapofanya uchaguzi wa viongozi wake na si hivi sasa kuibua suwala hilo”; alibainisha Jussa.Hamad Rashid na Maalim Seif, wote ni miongoni mwa wanachama wa CUF waliopata misukosuko na mateso mengi, ikiwamo kukaa Gerezani kwa muda mrefu, kuhusiana na harakati za siasa kwa lengo la kuwatetea Wazanzibari

WANANCHI WA ZANZIBAR NAFIKIRI NILISHAWAMBIYA HAPA MARA NYINGI SANA KUWA TUKISUBIRI VIONGOZI WATUKOMBOWE TUTA SUBIRI SANA SANA. MAANA MAMBO NDIO KAMA HIVI WAZANZIBAR WAMEUNGANA NA SASA WANATAKA KUJIKOMBOWA HUYU HAMAD RASHID ASHAZUKA NA YAKE. SASA WATU WATATENGANA TENA KISHA TUNARUDI KULE KULE TULIKOTOKA KWENYE SIASA ZA CHUKI NA KUBAGUWANA. KISHA MKOLONI MWEUSI ANACHEKA SANA ANASEMA WANGALIYE WENYEWE KWA WENYEWE WANATAFUNANA KWELI WATAWEZA KUJITAWALA..? NA HAYA SIO YA LEO WALA JANA HABU NIWAKUMBUSHE KIDOGO MIAKA YA NYUMA YA WAKATI WA CHAMA CHA HIZBU PIA KULIKUWA NA MKORONGANO MWISHO BABU AKAFUKUZWA NA AKANZISHA CHAMA CHAKE NYERERE AKAONA MWANYA AKAMLETA OKELLO NA VIKAPTURA WAKATUUWAA VIZURI SANA  KISHA WAKATUTAWALA MPAKA LEO SASA HAMAD RASHID NAE ANA ANZA KISHA KUTAZUKA LA KUZUKA MWISHO KUTATOKEYA MAPINDUZI YASIYOJULIKANA MIGUU WALA KICHWA MWISHO WAKE TUTAJIKUTA TUNATAWALIWA TENA NA WATU HATA SIO WAZANZIBAR KWA MIAKA MENGINE 47 KWA HIYO WAZENJI FUNGUWENI MACHO NA FINIKENI KOMBE MWANAHARAMU APITE ASIJAKUTULETEA BALA ZANZIBAR.

Wednesday, December 7, 2011

MAMBO MAZURI ALIYOFANYA GADDAFI KTK NCHI YAKE NA RAI WAKE AMBAYO LEO HAYASEMWI



Now let us get to the unknown facts about the Libyan dictator Muammar
Gaddafi:



1. There is no electricity bill in Libya; electricity is free for all
its citizens.

2. There is no interest on loans, banks in Libya are state-owned and
loans given to all its citizens at 0% interest by law.

3. Home considered a human right in Libya - Gaddafi vowed that his
parents would not get a house until everyone in Libya had a home.
Gaddafi's father has died while him, his wife and his mother are still
living in a tent.

4. All newlyweds in Libya receive $60,000 Dinar (US$50,000) by the
government to buy their first apartment so to help start up the family.

Traditional wedding in Tripoli, Libya

5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi
only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.

6. Should Libyans want to take up farming career, they would receive
farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to
kick-start their farms - all for free.

7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need
in Libya, the government funds them to go abroad for it - not only free
but they get US$2,300/month accommodation and car allowance.

8. In Libyan, if a Libyan buys a car, the government subsidized 50% of
the price.

9. The price of petrol in Libya is $0.14 per liter.

10. Libya has no external debt and its reserves amount to $150 billion -
now frozen globally.

Great Man-Made River project in Libya... $27 billion

11. If a Libyan is unable to get employment after graduation the state
would pay the average salary of the profession as if he or she is
employed until employment is found.

12. A portion of Libyan oil sale is, credited directly to the bank
accounts of all Libyan citizens.

13. A mother who gave birth to a child receive US$5,000

14. 40 loaves of bread in Libya costs $ 0.15

15. 25% of Libyans have a university degree

16. Gaddafi carried out the world's largest irrigation project, known as
the Great Man-Made River project, to make water readily available
throughout the desert country.

Which other dictator has done much good to his people?

YEYE NI DIKTETA LAKINI KAFANYA MAMBO MAZURI KWA RAI WAKE NA NCHI YAKE SASA LAKUJIULIZA NI NINI KILICHOFANYA MPAKA RAI WAKE WAKAMCHUKIYA NA KUMTOWA MADARAKANI..? PIA TUNAWEZA KUJIULIZA KATAWALA MIAK SIO KIDOGO NA KAFANYA MAZURI NA MABAYA KTK NCHI YAKE LAKINI ALIPO ONA WATU WAKE HAWAMTAKI TENA KWA NINI AKAWA BADO ANAKAZANIYA KUKA KWENYE KITI....?   JE WAHAFIDHINA WA WATANGANYIKA MULIOKUWEPO ZANZIBAR MUNASUBIRI HAYA NA NYINYI NDIO MUJUWE SOMO...?

Tuesday, December 6, 2011

VIONGOZI WA ZANZIBAR PELEKENI UJUMBE HUU DODOMA NA NCHINI TANGANYIKA WAAMBIYENI WAZANZIBAR-HATUTAKI MUUNGANO


KARUMA NA NYERERE WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZI
KISHA WANASEMA ANATIA SAINI YA MUUNGANO MAWE
WATANGANYIKA MUNA MASIKIO YA CHINI NINI TUSHASEMA HATUTAKI MUUNGANO,HATUTAKI MUUNGANO,HATUTAKI MUUNGANO.

Jamani hamuoni mbali, munaangalia karibu mbele yenu tu. Kwanza siungi mkono kuwa tuijadili katiba na makubaliano ya muungano.MAANA TANGANYIKA HAIPO SASA VIPI TUNAJADILI KATIBA NA MAKUBALIANO YA MUUNGANO...?? Halafu wanalete hili suala la katiba ili kutupotezea lengo la muungano. Sisi tunachokitaka ni kuondoka muungano kabisa. Kutokana na kauli zao za kipuuzi na kijeuri kina Kikwete na wenzake, sasa hatutaki tena kujadili muungano wala katiba. La msingi ni sisi kuingia barabarani tu kama kuna kibali au hakuna maana sasa imekithiri mno.

Niliposema kuwa hatuangalii mbali nakusudia kuwa kura ya maoni kwa sasa haina hadhi kwa sisi Wzanzibari. Nifahamuvyo mimi ni kwamba kwa sasa Zanzibar kuna wahamiaji wengi kutoka bara na hao hawakuja kwa kwa bahati mbaya tu, bali wamekusudiwa.kuletwa kwa makusidi ili wazanzibar tukidai haki ya nchi yetu watulete kwanza jadilini mswaada hatukutaka watasema basi kura ya maoni maana wanajuwa kuwa washawajaza watu wa hapa zanzibar kwa hiyo hao watasema wanataka muungano kwa hiyo wazanzibar tutakuwa tushamezwa na tukumbuke kuwa Wao ndiyo wanaopewa vitambulisho vya Zanziabar na wananyimwa Wazanzibari wenye haki. wao ndiyo watakaosema kuwa muungano uendelee. Mimi nawapinga wale wanaotaka kura ya maoni kwa sasa hivi. Tutakuwa tumejipaalia makaa kipweza.
Mrfroasty suala la sheria na wanasheria kwa sasa halikubaliki kwani hata huo muungano asili haukuwa wa kisheria. zile picha zinazo oneshwa kuwa Karume anatia saini siyo kweli kuwa anatia saini ya muungano, inaweza kuwa anatia saini kitabu cha maombolezi au cha wageni. Siki ya kutia saini mkataba alitakiwa mwanasheria wa Zanzibar siku hizo, DAURADO awepo, lakini aliotewa yuko nje ya nchi ndiyo akapewa karume makaratasi atie saini bila kujua kilichomo na aliharakishwa ufanya hivyo na nyerere kabla Dourado kurudio. Kwa hiyo suala la kuwa tuende na sheria na wanasheria litoke vichwani mwetu kama kweli tunataka Zanzibar yetu. halafu matokeo ya kufuata sheria ni haya tunayoyaona kuwa kila siku danganya toto tu huku tunazungumzia muungano wao wanazungumzia katiba what the hell is this!!!!
Kama tunataka nchi yetu tuache maneno na tudai Zanzibar na siyo kujadili katiba na muungano. Tuingie njiani kama walivyofanya wamisri. Tuingie huku tukiwa tumejitayarisha kwa lolote na pia kwa jina la ALLAAH.

SOTE ZANZIBAR NZIMA NASEMA ZANZIBAR NZIMA TUSEME KWA SAUTI MOJA. HATUTAKI KURA YA MAONI,HATUTAKI KUJADILI KATIBA NA HATUTAKI MUUNGANO TUNATAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR IWE NCHI HURU.

HAYA NDIO MANENO YA KUSEMA KAMA KWELI TUNAITAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR M/MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA KIZAZI CHAKE CHOTE AMIIIIIIIIIIIIIIIIIIINI

Friday, December 2, 2011

FIKRA ZA WATANGANYIKA NA YALIYO NDANI YA NYOYO ZAO ZAIDI YA ZANZIBAR


Tanzania ni nchi gani.............???

Wana jamvi nimejaribu kujiuliza mara nyingi kuwa Tanzania ni nini???
Kutokana na historia niliyofundishwa ni kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Zanzibar na Tanganyika.Lakini swali linakuja, Je baada ya muungano Tanganyika ilikwenda wapi? Bona zanzibar ipo? Na hata wazanzibar wanatambua kuwa Zanzibar ni nchi? (nikumbushe kauli ya mtoto wa mkulima ambaye kiuelewa anapaswa kuuelewa muungano lakini kidogo limtokee puani baada ya kutamka kuwa Zanzibar siyo nchi).Je naweza kuamini kuwa baada ya muungano basi Tanganyika iligeuzwa kuwa koloni la zanzibar??
Je leo muungano ukifa sehemu ya bara tutaiita jina gani? Nasema hivyo kwa sababu wanasiasa wanatuhadaa kuwa huu muungano ni wa nchi mbili – ni zipi hizo kwani mimi naifahamu Zanzibar lakini kwa sasa hakuna taifa linaloitwa Tanganyika. Naomba ieleweke kuwa hakuna document yeyote inayothibitisha kuwepo kwa taifa linaloitwa tanganyika zaidi ya historia ya vitabu.
Kimsingi yapo mambo yanayotambulisha taifa .
Bendera ya nchi
Wimbo wa taifa
Raisi wa nchi
Kutoa uwakilishi wa mabalozi na mengine ambayo pengine wengi tunayaona.
Kupigiwa mizinga
Zaidi zanzibar wako kwenye mchakato wa kupata katiba. Vyote hivi Zanzibar vipo.
Swali: Leo muungano ukifa Kikwete atakuwa raisi wa nchi gani??????? Sehebu ya bara itatumia bendera gani, katiba gani na wimbo wa taifa upi? na taifa litakalobaki litaitwa jina gani au historia itajirudia?
Kuna kila dalili zioneshazo Kuwa Watanzania wa Visiwani Hawawapendi Wenzao Watanzania Bara na hili lipo wazi kabisa.kwani huwa wanakuja juu sana likitokeapo jambo litatizalo na huwa wanaonesha wazi kuwa hawautaki huu Muungano wa Karume na Nyerere.. Choko choko huwa Nyingi sana na mwishowe wabara wakiona maji yamezidi Unga hugawa Nyadhifa zao uongozi kwa Wavisiwani Mifano ni Mingi Sana.
Sasa kwa Mwendo huu hizi Nyadhifa zitatolewa hadi lini siku wakitaka kupewa hadi ardhi yao ya kimagumashi ya pwani maybe Wabara ndipo watapoamka na kuwaona hawapendwi..
Ningeona jambo jema Tuwajue kuwa kama hawa Wavisiwani Wanatupenda au la! siku nyingi wanaomba wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni kama wanauhusudu huu Muungano au La .. It means kwa sasa wamelazimishwa kuwa nao kwani hawajisikiii kabisa haki ya Mama Kuitwa wao ni Watanzania kama huamini muulize Mtu yeyote mwenye asili ya Visiwa vya Pemba na Unguja.
Na sie wabara Tunahitaji kujuwa kama ”Wazanzibar they are with us or Against Us”
Mie kwangu Ningependa Kujua hili. Katiba Mpya Watanganyika kuwa Serikali Yao.
Hakika tufike sehemu tuseme ENOUGH IS ENOUGH,YANI IMETOSHA IMETOSHA,na kusema UKWELI watu wazima kimri walioko kwenye madaraka wajue kizazi cha watuchini ya umri wa miaka 45 kushuka chini Muungano wetu na Zanzibar hauna faida yoyote kwao zaidi ya kwenda Zanzibar kutalii kama Mtanzania wa Bara anavyoenda Bagamoyo ambako ni Tanzania huru kwake.
Hivi lini tulisikia Mtanzania mzaliwa wa Moshi na Mbunge wa Moshi akaenda Zanzibar kuwa Waziri au katibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Lakini wao wakizidisha choko choko zao kidogo tu utasikia wamewagawiwa Uwaziri tena zile sekta nyeti kama Waziri wa Mambo ya Ndani,kwa maisha haya mpaka lini.
Hivi tunajambo gani hilo zito la SIRI KUU ambayo haipo kwa faida ya umma.Manake kwa sie tulio chini ya umri wa mika 45,Tanzania ya kesho ni yetu,yani kwa mwenye umri wa miaka 45 Mungu akimpa uzima anamiaka 35 ya kutumikia Taifa kama Mtanzania mwenye ushiriki Mkubwa wa Tanzania ya kizazi kipya kijacho.
CCM watu wazima wajue vijana wao wanaowaaanda kulithi matendo yao ya kushabikia MUUNGANO WA KIMABAVU,USIO NA TIJA KWA UMMA,BALI TIJA ZA KIDOLA NA MATAJILI WA KIDUNIA,HAWAWEZI KUJA KUSHINDANA NA KIZAZI KIPYA AMBACHO KILA SIKU YA MUNGU KINAZIDI KUWA NA UFAHAMU MKUBWA TOKA WAKIWA NA UMRI MDOGO [Kwa wale wenye watoto wadogo nyumbani wa umri wa miaka mitano mpalka nane wanaweza kuona ufahamu wa watoto hao wadogo kupitia jinsi watoto wao hao wanavyocheza na vyombo ya kieletlonia vitu kama simu,televisioni,computer games,na stimulation games zinginezo katika uwezo wa ajabu ambao hata mzazi wake mwenye hana uwezo huo].”
Kwa sasa sio kizazi cha kulazimisha kufuata bila kuhoji,ni kizazi cha majadiliano na majibu yenye ukweli mwingi kuliko uongo usio na msingi.
Tufike wakati kabla wazee hao hawajaondoka watuondolee utata huu,tujue moja JE WAZANZIBAR WAKO NASI AU HAWAKO NASI [ARE THEY WITH US OR NOT-ni msemo wa sauti ya kimarekani kuwambia washirika wake wanapokuwa wanataka kujua ushiriki wao].
Kama wanzanzibar watesema wako nasi basi jibu ni Serikali moja tu,. ((HAHAAHAHAHAAHAHA NACHEKA SANA MTANGANYIKA AKISEMA SEREKALI MOJA MAWE)) hakuna cha Serikali Tatu,wakigoma wapewe Serikali yao ya Wanzanzibar ambayo tayari wanayo wakiwa na kila kitu soon wataomba Bank Of Zanzibar [BOZ] yote hayo kwishney nasi tuchukue Tanzania iwe yetu the game is over.
Kwa Wanzanzibar walioko Tanzania kama Watapenda kuishi Tanzania wakane uraia wa Zanzibar wao na Watoto wao,na kwa wale watakao taka kuludi kwao Zanzibar wapewe mabegi yao kwaheri na wasitoke na chochote,unyambilis unyambilisi, kwa kuwa vyote walichuma Tanzania barana((HAHAHAHAHAHAHHA HAYO NDIO ALIYO YAFANYA IDDI AMINI DADA KUWAFUKUZA WAHINDI NA MABEGI TU HAWAKUCHUKUWA KITU NCHI IKAFILISIKA MPAKA WAKAWAOMBA WAHINDI WARUDI UMESOMA WAPI RAFI YANGU.......??))
 kwa wasukuma,wanyamwezi,wangoni,waha na wanyakyusa walioko Zanzibar nao masharti ni hayo hayo kama wanataka kubali Zanzibar wabaki wakiona wanatka kuludi bara fungasha beki ludi kwenu Tanzania.((WATANGANYIKA KURUDI BARA NI RAHISI SANA MAANA HAWANA KITU CHOCHOTE HUKU ZANZIBAR ZAIDI YA BEGI LA VINYANGO,POMBE,BANGI,UNGA YANI DRUG,MALAYA,WIZI NA UJAMBAZI WAKUINGILIYA WATU MAJUMBANI USIKU AMBAYO MAMBO HAYA HAYAKUWEPO ZANZIBAR TULIKUWA TUKILALA MLANGO WAZI KWA HIYO WAKIRUDI BARA NA KWENDA KUYAFANYA HAYA HUKO ITAKUWA NI MSAADA MKUBWA MAANA SISI HATUYATAKI KABISA KTK NCHI YETU YA ZANZIBAR.))
Kwa wale waliobahatika kuwa viongozi wetu wakajua siri zetu tutaishi nao kimarekani, all Eyes on Them.Tufike sehemu watu wazima wajue kuwa kizazi chetu new generetion dotcom ni aina gani ya watu hao, yani vijana kama Tindu Lissu,Nape, Zitto, Mnyika ,Mdee,na wengineo wenye akili timamu ndani ya Bunge ni wachache mno yani ni cha Mtoto mno [A Tip oga na Iceber] ya vijana wa kitanzania wenye uwezo wa kufanya maajabu kwa Nchi hii.Ukitaka kuwajua walivyo wabaya tembelea mabenki na mashrika ya umma waulize wanavyopata shida na watyu hao.Wengi baada ya kuona Nchi haileweki wameamua kuiga matendo ya wasure/madingi wazee wao nayo ni kuchota na kusepa.Lakini laiti kama wangekuwa na heshima kwenye Serikali yao nao Serikali ikatambua ikawapa nafasi hakika Nchi hii miaka kumi na tano mingi,ingekuwa Nchi ya Pilia Afrika kuendelea baada ya South Africa.
Wapo vijana kibao uku mitaani,ebu muone Sugu,hivi watu wazima ndani ya CCM madaraka, hawajiulizi,kuhusu kijana kama huyo ambae elimu yake ni ya wastani [Kasoma Kayumba Sekondari School-ambayo ndio wengi ya vijana wa Watanzani-Akaenda Chuo Kikuu Mitaani Universty Dot Com-Chuo pekee cha Watanzania walio wengi kati ya Laki tano [500,000] wanaomaliza kidato cha sita na wanapata nafasi ya chuo kikuu ni elfu hamsini [40,000] kati ya hao laki tano].Lakini leo hii SUGU anauwezo wa kuwatuliza Watanzania Millioni na ushee wenye gadhabu na Serikali yao ambayo imewachokoza na kushindwa kuwahudumia.
Hivyo wasitegemee kwa kupindisha ukweli wataendelea kufanikisha mahitaji yao,bali ni kuwa wamechukua bomu wakategua pin wamelishikilia mkononi huku wanakula ole wao wakipitiwa na usingizi,au wakastukizwa ghafla kama tukio la Mbeya, na kisha watu aina ya SUGU wakago,ma kukaa upande wa SERIKALI ILI KUTULIZA WATU,wakasimama upande wa WANANCHI KISHA wakafanya kuwaongoza kumsaka mmoja baada ya mmoja kwenye majumba yao na hakika RISASI ZILIZO KWENYE MAGHALA YA JESHI,MALI YA HAO AMBAO LEO HII WAMEGOMA HAZITATOSHA KUMALIZA HASIRA ZAO.TUSIOMBE KUFIKA HUKO LAKINI WAZIMA HASWA VIONGOZ WA SERIKALI KUPITIA CCM WAJUE MFUMO WA NDIO MZEE UMEKWISHA SASA.

Thursday, December 1, 2011

WATANGANYIKA WAANZA KUTOKA USINGIZINI SASA BAADA YA MIAKA 50


JE NI MIAKA 50 YA TANGANYIKA AU TANZANIA
HAHAHAHHAHAHAHAHAHAHAHAH NACHEKA SANA
JINSI NYERERE ALIVYOWECHEZEYA WATANGANYIKA
NA SASA KIKWETE PIA ANAFANYA YALE YALE YA NYERERE
                                                         Utata wa Tanganyika na Tanzania.
SINA muda wa kupoteza leo isipokuwa naomba tujivue unafiki na kisha kila mmoja wetu ajihoji Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea Uhuru wa miaka 50 ya taifa lipi...?????????
Nahitaji jibu la moja kwa moja si siasa za upotoshaji, anayejibu swali hili anapaswa kujiweka katika nafasi ya mtoto mdogo anayepaswa kujua jambo fulani kiundani.Desemba 9, mwaka 1961, kulikuwa nchi yetu inaitwa Tanganyika ambayo ilipata uhuru wake. Ilipofika mwaka 1964 Rais wa Tanganyika Julius Nyerere na mwenzake wa Zanzibar Abeid Amani Karume, waliona ipo haja ya mataifa hayo kuunga.
Muungano ni kuunda umoja na ushirika wa pamoja lakini nje ya hapo kila mtu anabakia kuwa kama alivyokuwa awali. Hii kwa bahati mbaya sivyo ilivyokuwa kwa huu muungano wetu.
Baada ya Muungano kufanikiwa na kuundwa Tanzania, nchi moja ya Tanganyika ilinyongwa na ikabakia Zanzibar. Na ndani yake zikaletwa siasa za Tanzania Bara na Tanzania Visiawani.
Hivi mtoto wa kizazi cha leo anapohoji kujua ilipo Tanganyika tunaweza kumweleza nini mbali na siasa? Zanzibar ipo Tanganyika ilikufa ikazaliwa Tanzania Bara ambayo kimsingi ndiyo hiyo hiyo Tanzania.
Hii ndiyo historia ya nchi yetu, na tunathubutu kutembea kifua mbele tukijiaminisha kuwa tumekomaa kifikra vya kutosha wakati tunapotosha ukweli kuhusu Taifa letu...??????????????
Leo watoto, vijana, watu wazima na mbaya zaidi viongozi kila mmoja anaimba kuwa Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ( Hii ni nchi ipi..?????????????).
Zanzibar wana vielelezo vya utambulisho wao kama taifa, wana wimbo wa taifa, bendera, katiba yao, Bunge lao na mengineyo. Nchi inayoitwa Tanzania Bara haina bendera, wimbo wa taifa, Bunge badala yake wanatumia vielelezo vya taifa la Tanzania lililotokana na muungano wa (Tanganyika na Zanzibar).
Hivyo, hata Desema 9 mwaka huu, kinachosherehekewa si miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Maana siku hiyo utaimbwa wimbo wa taifa wa Tanzania, itapeperushwa bendara ya Tanzania, Rais atakuwa wa Muungano, sasa hapa tutasemaje ni uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara kama tunavyojidanganya)?
Hivi ndivyo tumeendelea kujidanganya kwa miaka yote. Tumekuwa na Bunge la Muungano ambalo linawashirikisha wabunge kutoka Zanzibar, kimsingi linapaswa kujadili mambo yale yanayohusu muungano tu.
Lakini kutokana na udhaifu wa muundo wa muungano wetu hata kwenye mijadala ya mambo yasiyo ya Muungano wabunge wa Zanzibar wanaendelea kuwemo wanashiriki kutuamulia wakati kule kwao wana Baraza la Wawakilishi ambalo linajadili mambo yao pekee.Huu mfumo wa muungano wetu lazima tukubaliane kuwa una kasoro hata kama hatutaki kuambiwa ukweli. Ni bora kujitathmini kuanzia hapa ili itafutwe suluhu ya kuondosha upotoshwaji wa historia ya nchi yetu ya Tanganyika badala ya kuendelea kuzika vichwa mchangani kama kanga tukidhani tumejificha hakuna shida.Mfano mdogo wa mkorogano huu unajitokeza kwenye michezo hasa kwenye mashirikisho yanayotutambua kama nchi mbili. Kwa sasa hapa Tanzania yanaendelea mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).Katika michuano hiyo Zanzibar wameingia kama nchi, wanatambulika kwa timu yao ya Zanzibar Heroes wakiwa na bendera ya taifa lao na wimbo wao wa taifa halafu eti sisi tumejibadilisha kutoka Taifa Stars tunajiita Kilimanjaro Stars.Lakini kinachofanyika kwenye timu ya Kilimanjaro Stars ni kile kile cha Taifa Stars, kwani wimbo na bendera wanavyotumia ni vile vile vya Tanzania. Na hata kocha kabadilishwa tu mwaka huu baada ya Wazanzibari kuhoji maana huyo huyo wa Taifa Stars ndiye alikuwa anafanywa wa Kilimanjaro Stars.Mimi ni mmoja wa waumini nisiyeona aibu kusema kuwa tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, lakini siku hiyo ya Desemba 9 mwaka huu, sitasherehekea maana hakutakuwa na bendera ya Tanganyika wala wimbo wa Tanganyika ili kuniletea hisia za kumbukumbu ya kuachana na ukoloni.Naogopa sana unafiki na uongo wa kujidanganya kushiriki kuimba wimbo wa Mungu ibariki Tanzania wakati huo bendera ya rangi nne ya Tanzania ikipeperuka halafu nijiaminishe kuwa nimesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Tafakari!