Wednesday, January 11, 2012

NCHI YA ZANZIBAR MAJI HAKUNA UMEME WA MGAO VYAKULA VIMEPANDA BEI LAKINI SHEREHE ZA MAPINDUZI LAZIMA ZIFANYWE NA TAYARI MILLIONI700 AU ZAIDI ZITATUMIKA NIAKILI HIZOOOO

HAYA NDIO WALIYOYAFANYA VIKAPTURA MACHONGO KUWAUWA DUNGU ZETU WA HAPA ZANZIBAR NA KUWANAJISI DADA ZETTU NA MAMA ZETU NA KUTUIBIYA MALI ZETU NA KUTUTHALILISHA NA KUTUKANDAMIZA NA KUTUTAWALA KWA NGUVU MPAKA LEO HII ZANZIBAR HAIKO HURU INATAWALIWA NA NYINYI WAPUMBAVU WAKUBWA NDIO KWANZA MANAPLANI KUFANYA SHEREHE ZA KULIWA MAMA ZENU,BABA ZENU,DADA ZENU,KAKA ZENU NA KUPORWA KWA NCHI YENU NYINYI MUNASHANGILIYA HAYO AMAKWELI USIMUAMBIYE KIPOFU TAZAMA.HAKUNA HATA MAHALI PAMOJA KATIKA ULIMWENGU HUU SASA AMBAPO WATU HAWAJUWI NINI KILICHO TOKEZEYA 1964 ZANZIBAR ILA MUNAJIFANYA KAMA PUMBUWANI SIO HAYA SHEREHEKEANI KULIWA KWA DUNGU ZENU.HIZO PESA KWANINI ZISIFANYIWE MPANGO MAALUM WA MAJI AU UMEME AU KUSHUSHA BEI YA VYAKULA.SI NDIO YA MUHIMU HAYA LAKINI WAPI MUNAONA BORA MUSHEREHEKE KULIWA KWA DUNGU ZENU KULIKO KUWA NA MAJI,UMEME,NA CHAKULA MIAKA NENDA MIAKA RUDI MAMBO NI YALE YALE TOKA 1964 HAYA SHEREHEKEANI TOWAONE.JIONE MWENYIWE MAITI ZA WAZANZIBAR ZILIVYO JAZWA KWENYE MALORI KUTOKA MASHAMBA NA BAHARINI MBALI WALIOULIWA NA KUFUKIWA KATIKA KABURI MOJA KISHA NYINYI MUNASHEREHEKEYA MAUWAJI HAYA ILIKUWA WATU MUKUSANYIKA NA KUSOMA HITMA NA KUOMBA DUWA M/MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI NA AWASAMEHE WAZANZIBAR WALIOFANYWA MAJUHA KWA UROWO WA MADARAKA WAKAWAUWA WANZAO NAMWISHO WAO WENYEWE PIA WAKAULIWA LAKINI HAYA HAYAWAINGI KATIKA VICHWA VYENU NYINYI MUNASUBIRI SHEREHE TU BASI MUKAI MUKIJUWA MUNASHEREHEKEYA KULIWA NA KUNAJISIWA NA KUIBIWA NA KUCHUKULIWA NCHI YETU YA ZANZIBAR HAYO NDIO MUNAYO SHEREHEKEYA SIO UKOMBOZI KAMA MUNAVYODANGANYWA KUWA MULIKOMBOLEWA MAWEEEEEEEEEEEEEEE
Zaidi ya Shs. Million 700 zinatarajiwa kutumika katika kuadhimisha Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12 Mwezi huu huko katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Vuga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa fedha hizo ni kwa makisio tu lakini taarifa kamili ya matumizi hayo itatolewa baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo
Amesema kuwa sherehe za mwaka huu zitakuwa ni tofauti kidogo tu ukilinganisha na miaka iliyopita kwani wanafunzi hawatoshirikishwa wakiwa wamevaa sare zao kwani imeonekana kuwa wananchi wengi watahudhuria sherehe hizo.
Amesema kuwa Kiwanja kilichokuwepo kwa sasa hakikidhi haja ya kuweza kuwachukua wananchi wanaokadiriwa kuzidi uwezo wa uwanja huo ambao ni watu 15 Elfu tu.
Hata hivyo Waziri Aboud amesema kuwa Wanafunzi hawakatazwi kuja kusherehekea wakiwa wamevaliwa nguo zao kama wananchi wa kawaida
Akizungumzia suala la Sherehe hizo kuitwa za Mapinduzi wakati Zanzibar inaendesha Chaguzi zake kwa njia za kidemokrasia, amesema kuwa Neno Mapinduzi ni kitu ambacho kilichowagomboa wananchi wa Zanzibar kwa hivyo Serikali imeona iko haja ya neno hilo lienziwe kwani Mapinduzi ndiyo yaliyowagomboa Wananchi wa Zanzibar kutoka katika makucha ya Wakoloni.
Aidha amewapongeza wananchi wa Zanzibar pamoja na waandishi wa habari kwa mashirikiano yao makubwa ambayo wameyaonesha katika kusherehekea sherehe hizo za miaka 48 ya Mapinduzi tangu kuanza kwake tarehe 4 mwezi huu.
Waziri Aboud ametoa wito kwa wanachi kuhudhuria kwa wingi katika sherehe hizo ambazo milango yake itafunguliwa kuanzia saa 12 za asubuhi siku ya kilele

No comments:

Post a Comment