Thursday, February 23, 2012

JOYCE NDALICHAKO NAE PIA AITA ZANZIBAR NI MKOA RAISI SHEIN KUMBE SI RAISI NI MKUU WA MKOA WA PWANI ZANZIBAR DUUUUUUH!!!!!!!


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani NCHINI TANGANYIKA ((Tanzania)) (NECTA) Dk Joyce Ndalichako
HILI NDIO JINAMIZI LILILOWEKWA KTK BARAZA LA MITIHANI KUWAKATA ROHO KIZAZI CHA NCHI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

WASWAHILI WANASEMA BORA MTU AKUNYIME KULA KULIKO KUKUNYIMA ELIMU NA HAPA SASA NDIO TUNAONA KUWA HAWA WAKOLONI WAUSI WANATAKA KUWANYIMA ELIMU KIZAZI CHA ZANZIBAR KWA MAKUSUDI ILA IWEJE ILI TUSIWE NA WASOMI NA TUKIWA HATUNA WASOMI NDIO HIVYO TENA NIKUBURUZWA NA NCHI YATU YA ZANZIBAR MPAKA KIYAMA KISIMAME NAWAPA HONGERA WANAFIKI NA VITUMWA VYA WAKOLONI WAUSI WALIOKUWEPO UNGUJA NA PEMBA MAANA WAO NDIO WANAOKAZANIA TUWE NA MUUNGANO NA HIZI NDIO FAIDA ZA MUUNGANO HII NI BASHRAAFUU TU NGOJENI KARAMU SASA SHAMHUNA ASHACHINJA NGOMBE NI ILE BAHARI SASA BADO KUPIKWA BIRIANI NA KULIWA TUUUUUUU.


Baadhi ya wazee ambao walishiriki katika kongamano la kutathmini matokeo ya mtihani yaliotangazwa na baraza la elimu Tanzania (NECT) ambalo limewafutia jumla ya wanafunzi 3303 kwa madai ya udanganyifu wengi wao wakielezwa ni kutoka Zanzibar
Na Ally Saleh
Wiki iliyopita ilikuwa ni kubwa kwa habari za matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne kwa taifa lakini zaidi kwa upande wa Zanzibar. Ni hizo zilitikisa bahari ya Hindi hadi visiwa vikawa vinatetemeka. Ilibidi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Joyce Ndalichako afanye ziara ya kuja Zanzibar kuelekezea nini kimejiri mpaka yakatokea yaliotokea ambayo wazee na wanafunzi bado hawajaamini.
Chanzo ni habari za kufutiwa na matokeo na kufungiwa kufanya mitihani kwa wanafunzi zaidi ya 3,000 kote Tanzania kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa ni udanganyifu unaotokana na mfanano usio wa kawaida.
Lakini pia ikaelezwa kuwa kuna mambo mengine yasio ya kawadia yaliotokea kama vile wanafunzi kuandika matusi, kuchora picha kadhaa lakini pia kuandika nyimbo za Bongo Fleva, si matunda ya kizazi kipya bwana. Basi hiyo ikawa ndio habari.
Ila kwa Zanzibar, kama mshirika kamili katika Muungano, wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli za sekondari wakaona maelezo ya Mama Ndalichako hayakutosha na nafikiri habari hii akaijua na akaamua kuja Unguja, lakini basi hapa akaonana na waandishi wa habari, waalimu na maafisa wa Serikali.
Katika kongomano la siku moja liloitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo WAHAMAZA wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli walisema wangefurahi wangekutana nae wao Mama Ndalichako na mzee mmoja akasema “angetafuta mahala pa kukimbilia.”
Kwa nini akasema hivyo? Amesema hivyo kwa sababu anaamini kuwa Mama Ndalichako hakutoa ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kumekuwa na udanganyifu na baya kuliko yote ametoa maelezo aliyoyaita kuwa ni ya jumla jumla, mzazi Ahmed Ali alisema.
Mzazi Ahmed kama watu wengi katika kongamano hili alisema Mama Ndalichako ametoa maelezo mengi ya kujilinda na akikwepa kabisa kukubali ukweli kuwa mtihani ulivuja na hicho ndio sababu ya yote yaliotokezea ambayo yeye anadai hajui chanzo chake.
“Nasema mtihani ulivuja kwa hakika. Mimi mwenyewe niliupata nikiwa katika cyber cafĂ© moja mjini Dar es Salaam. Na nakala ya mtihani huo ambao ulikuwa kwa Kiingereza na uliokuwa ukisambazwa kwa internet ninayo mpaka leo.”
Washiriki wengi walisema Mama Ndalichako anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa sababu mtihani ulivuja na kadri anavyojitetea na kutoa maelezo ndivyo ambavyo anazidi kujizonga na kujikaanga.
Moja katika maelezo ya Katibu Mtendaji ya kuwepo kwa udanganyifu ni kule kutokea kuwa kumekuwa na karatasi za majibu ya wanafunzi zikiwa zimeandikwa na watu kadhaa na akisema anashindwa kuelewa hilo limetokezeaje wakati wanafunzi wanaodaiwa kuhusika hawakuwa wamekaa jirani kwenye vyumba vya mitihani au chumba cha mithani kwa sababu hakueleza kuwa hilo limetokea shule moja au shule kadhaa.
Kisha akatoa mifano kadhaa iliyoonyesha kuna baadhi ya karatasi za maiibu ambazo wanafunzi waliandika neno kwa neno jambo ambalo halina jawabu nyengine zaidi ya kuwa kulikuwa na udanganyifu tena wa hali ya juu.
Wazee na waalimu walikiri na wala kuwa kulikuwa na udangayifu lakini hoja yao ni kuwa udanganyifu huo ulitokana na kuvuja kwa mitihani ambao sio tu iko chini ya dhamana ya Mama Ndalichako lakini pia inalindwa chembilecho mtu mmoja “ kuliko hata ulinzi anaoupata Rais Kikwete au Dk. Shein.”
Kwa hivyo hoja ya wazee ni kuwa mitihani ilipatikana mitaani. Wanafunzi wakaifanyia kazi. Vitabu vya majawabu vilipatikana mitaani. Wanafunzi wakavitumia kuandika jawabu zao. Na kwa bahati mbaya kila eneo la jawabu akapewa mtu mmoja na ndio maana kitabu kimoja kikaonekana na hata za watu tofuati lakini hati hizo hizo zikaonekana kwenye vitabu vyengine.
Inawezekana kabisa kuwa baadhi ya waalimu na shule zilishiriki katika mchezo huo, walisema washiriki na kwa hivyo ni muhimu kutoa maelezo ya shule kwa shule na mwanafunzi kwa mwanafunzi ili kila mtu ajiridhishe na sio maelezo ya jumla kama aloyatoa, walisema washiriki. “ Kila mzazi anataka kuona mwanawe alishiriki katika visa hivyo au la. Na kila shule inataka kujua shutuma dhidi yake,” alisema Mzee Ali Hassan, Mlezi wa Laurette International.
Walimu na wamiliki wanasema wanajua mitihani ilivuja kwa sababu waliona jinsi ambavyo maafisa wa usalama walivyopekua wanafunzi wao na Mama Ndalichako akikataa hilo ni “kwa sababu ya kulinda kitumbua chake. Lakini kwa hili kitumbua hicho kimeshaingia mchanga na hakiliki” alisema Mwalimu Ameir Hassan.
Wazee na waalimu walishangaa kwa nini Mama Ndalichako alikuja Unguja bila kujitayarisha kujua idadi kamili kuhusu wanafunzi waliohusika kwa upande wa Zanzibar na walikasirishwa na jawabu yake nyepesi tu, “ Sijafanya hesabu ya mkoa kwa koa,” na washiriki wakasema yale yale ya kuona Zanzibar kama mkoa au mikoa mengine tu.
Na ndipo hapo hisia za Muungano zilipokuja na watu wakajaribu kunasibisha tukio hilo na matatizo na kero za Muungano. Walifika hata kuhoji idadi ya Wazanzibari katika Bodi ya Baraza la Mtihani na wakaenda mbali zaidi kuhoji iwapo chombo hicho kikiwa ni cha Muungano kimetoa ajira ngapi kwa Wazanzibari leo au hata jana na juzi kwa sababu kimeundwa tokea 1973 pale jambo hilo lilipofanywa kuwa la Muungano.
Litolewe katika Muungano watu walisema, Tuwe na Baraza la Mitihani letu watu wakapiga kelele suala hili lazima liwe katika ajenda wakati wa Mjadala wa Taifa wa Mabadiliko ya Katiba ambao uko njiani unakuja.
Wengine wakasema tukio hilo lina udini. Matokeo mengi yaliofutwa hapa Zanzibar yanahusu vyuo vya Kiislamu na kudai shule kadhaa za Kikristo huko Bara zinapasisha hadi mwanafunzi mmoja kuwa na kikapu cha alama za “A” lakini hapatiwi shaka au baadhi ya shule kupasisha darasa zima lakini hapatiwi ila katika matokeo kama hayo.
Halili kadhalika walizungumzia juu ya kutokuwepo hatua zinazofanana kwa kesi za aina moja ambapo mwaka jana baada ya kufutwa matokeo ya Darasa la Saba wanafunzi iliamriwa warudie mitihani, lakini pia kuukubwa wa adhabu ya wanafunzi na Professa Abdul Sheriff akiandika katika mtandao alisema, “ Haiingii akili utoe adhabu sawa kwa aliyeandika matusi, aliyechora picha na aliyedaiwa kudanganya katika mtihani.”
Pia yalikuwa ni maoni ya wadau kuwa kufungia wanafunzi kufanya mithani kwa miaka mitatu ni kuwahujumu kisaikolojia lakini pia wakasema ni mbinu za makusudi kuwakosesha Wazanzibari fursa ya kukuza wataalamu wake, maana kitachotokezea athari ya muda mrefu kwa Zanzibar kielimu lakini pia kijamii.
Hivyo wito ukawa kwamba hilo ni janga la taifa. Kama si kwa Tanzania basi kwa hakika ni kwa Zanzibar na kwa hivyo washiriki wakataka hatua za haraka zichukuliwe ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete kumuwajibisha Mama Ndalichako, kuunda tume kuchunguza tukio hilo na kutafuta suluhu ya kudumu ya kuvuja mitihani.
Lakini pia waliitaka Serikali ya Zanzibar kuchukua hatua kwa upande wake na sio kulaza shingo kwa maamuzi ambayo yanaathari kubwa kwa Zanzibar kama nchi. Lakini kubwa zaidi waalimu na wazee hao wamemtaka Mama Ndalichako aje Zanzibar kukutana nao uso kwa uso wakisema hawakutendewa haki kwa yeye kupita katika vyombo vya habari. “ Yeye ni mzazi na aje kwa wazazi wenziwe.”
SHEIN TWAMBIYE UKWELI ZANZIBAR NI NCHI AU MKOA WA PWANI ZANZIBAR...???
AU NDIO KUKU WA IKULU WASHAKUFANYA MASIKIO YAKO YAZIBE UWE HUSIKI
LOLOTE LINALOTOKE HAPA ZANZIBAR......???

Friday, February 17, 2012

BILALI ASEMA MSIUVUNJE MUUNGANO MAANA KUNA WATU WANATAKA KULETA USULTANI.

MSIVUNJE MUUNGANO ~~BILALI MAANA KUNAWATU WANATAKA KULETA USULTANI.ALISEMA BILALI

BILALI 
Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano amewataka Watz wasikubali kuuvunja Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba mpya.Aliyasema hayo jana Mlandizi Kibaha Vijijini wakati wa sherehe za kutimiza miaka 35 za kuzaliwa CCM Mkoa wa Pwani na kusema kuwa Watanzania wanapswa kudumisha Muungano na wasikubali kurubuniwa na wanasiasa wasioitakia mema nchi.((KWA NINI HUSEMA NI NCHI NGANI UNASEMA NCHI KAMA NI NCHI ZIPO NYINGI SANA HATA ZIMBABWE,ZAMBIA,MOZAMBIKI PIA NI NCHI.
Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kutumia marekebisho hayo kutaka kuvunja Muungano na kuleta USULTANI jambo ambalo si zuri kwani Muungano umeleta mambo mazuri na kikubwa kikiwa ni amani iliyopo.((AMANI ILIYOPO WEWE UNAKULA VIZURI NA FAMILIA YAKO NA KULALA VIZURI NA GARI ZURI NA POLISI WAKUKULINDA NA KUSAFIRI NCHI YOYOTE UNAYOTAKA AU SIO SISI JE TUNAKULA NINI..?TUNA LALA WAPI..?HATUNA HATA PESA YA KUNUNUWA PANADOL WACHA ZA KUSAFIRIA WATOTO WETU HAWANA SKULI NZURI WALA NINI UNAPO SEMA AMANI UNAMANISHA TUDUMISHE AMINI ILI WEWE UWENDELE KUISHI VIZURI NA FAMILIA YAKO NA SISI TUENDELE KUNYANYASIKA NA FAMILIA ZETU UNAJUWA WAZI YAKIJA MABADILIKO UTAKUWA MIONGONI MWA WALIOKUWA WAKILA RUSHWA NA MALI YA UMMA NDIO MAANA UNATULETEYA PROPAGANDA YA USULTANI SAWA HUWO USULTANI NA WEWE NANI BORA HEBU ANGALIA NCHI ZA KISULTANI RAI WAO WANAVYO ISHII NA SISI HAPA TUNA WEWE MIJINO MIKUBWA ANGALIA TUNAVYO ISHII UNASEMA NINI WEWE SERA HIZO ZIMEPITWA NA WAKATI UMECHELEWA)) “Kama mtu anakuja kuwaambia mvunje Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba msikubaliane naye, kwani haitakii mema nchi yetu((KAMA NI NCHI YETU BASI NA NYUMBA ZAKO ZOTE ULIZO JENGA NA MAGARI ULIYOWANUNULIA WAKE ZAKO NA WANAO NA JAMAA ZAKO NI ZETU PIA JE UTATOA NYUMBA YAKO MOJA TUWAWEKE WALE WAGOGO MASIKINI VIPOFU WA PALE KARIAKO KATIKA NYUMBA YAKO MOJA....? UTATOWA KTK MAGARI YAKO TUFANYE NI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA VIJIJINI UTAUZA NYUMBA ZAKO ILI TUJENGE HOSPITALI VIJIJINI UKIFANYA HIVYO HAPO NDIO TUTAJUWA KWELI NI NCHI YETU ILA KAMA WEWE UNAISHI RAHA MUSTAREHE NA SISI TUNAENDELEA KUISHI KTK HALI DUNI BASI HII NCHI SIO YETU NI YENU NYINYI VIONGOZI WA DODOMA NA MATUMBO YENU NA WAKE ZENU NA WATOTO WENU NA SASA UKOLONI MWEUSI LAZIMA UNGOKE TU MUKITAKA MUSITAKE. kwani amani(( AMANI NDIO NA HATA MUUNGANO UKIVUNJIKA PIA KUTAKUWA NA AMANI HATUTAKUWA NCHI ZA MWANZO KUVUNJA MUUNGANO WALA HATUTAKUWA NCHI ZA MWISHO KUVUNJA MUUNGANO)) na upedo((UPENDO HAMUNA MAANA VIONGOZI NYOTE MUNA NYUMBA ZAIDI YA 7 KILA MOJA NA MAGARI YAKILA AINA NA MABIASHARA KILA KONA NA SISI TUKO KTK HALI DUNI NA MBAYA ZAIDI NA NYINYI KAZI KUTUPINGA DOMO TU AMANI NA UPENDO AMANI NA UPENDO KUANZIA 1962 TANGANYIKA ILIPOPATA UHURU WAKE NYIMBO NI HIYO AMANI NA UPENDO MPAKA LEO 2012 HATUTAKI TENA NYIMBO NI MUDA WA VITENDO NA NYINYI NYOTE MUNGOKE MADARAKANI MAANA HAMUTUFAI.)) vimedumu kwa kupitia Muungano hivyo tusikubali kudanganywa:((NYINYI NDIO MUMETUDANGANYA MUMEUNGANISHA NCHI MBILI BILA YA KUTULIZA SISI WANANCHI NA SASA TUNA MATATIZO BADO MUNALAZIMISHA NCHI MBILI KUKA KIMYA KAMA HAKUNA KITU VILE HUU NI UDIKTETA PILI MUMEIUWA TANGANYIKA SASA WATU WA TANGANYIKA HATUJIJUWI TENA KAMA SISI NI WATANGANYIKA AU WATANG AU WATANZA AU WATANZANIA HATUJIJUWI KWAHIYO KAMA NI KUDANGANYA NYINYI NDIO WAONGO NA MATAPELE WAKUBWA.)) alisema Dk. Bilal

Thursday, February 16, 2012

KATIBA YA ZANZIBAR NDIO KATIBA YA KUFUATWA NA WAZANZIBAR SIO KATIBA YA VIRAKA NA SHERIA MPYA YA NAMBA 8 HAITUHUSU KITU SISI WATU WA ZANZIBAR.

JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR      KWANZA

JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR LAZIMA IRUDI ILI KIZAZI KIJACHO
KISIZALIWE TENA NCHI JIRANI BALI KIZALIWE NA KUKULIA HAPA HAP
NCHINI KWAO KTK JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.
Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar.
Vipi sheria ya Mabadiliko ya Katiba iweze kufanya kazi Zanzibar wakati Zanzibar ni Nchi iliyo na mipaka yake Kikatiba? Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi wazi katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza kwamba: “Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR”. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba kupitia kifungu chake cha 19-(1) kinachohusiana na makosa na adhabu kwa watakaotoa maoni nje ya hadidu rejea za rasimu ya Katiba: kifungu hicho pamoja na sheria yenyewe ya marekebisho ya Katiba, mwisho wake CHUMBE tuna sema tena na tena mwisho CHUMBE CHUMBE !!
Pili, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi kuwa, Katiba ya Zanzibar ndiyo yenye nguvu za kisheria nchini kote, ambapo ikitokezea sheria yo yote kutofautiana na Katiba ya Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana. Hii ni kuonesha nguvu na uwezo iliyonayo Katiba ya Zanzibar mbele ya sheria namba 8 ya mabadiliko ya Katiba, na kwamba, Katiba ya Zanzibar ndio “(The Grundnorm, which is the highest form of validity, being of the highest authority, providing efficient and affordable legal representation).
Tatu, hata hiyo Mahakama ya Rufaa, nayo haina uwezo, wala mamlaka, wala haki Kikatiba ya kuitafsiri Katiba ya Zanzibar maana Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza katika kifungu cha 99 kinachohusiana na kazi na uwezo wa Mahakama ya Rufaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA((Tanzania)) haiwezi kutafsiri Katiba ya Zanzibar. Kwa maneno mengine, Katiba ya Zanzibar inajitegemea, na kwa mantiki hiyo, Wazanzibari watahukumiwa kwa yao tu, na si kwa sheria ya mabadiliko ya Katiba wala nyengine yo yote ile tuna sema tena mwisho CHUMBE CHUMBE.
Nne, pamoja na vitisho vilivyomo kwenye kifungu cha makosa na adhabu ndani ya muswaada na sheria ya mabadiliko ya Katiba, bado sheria hiyo haiwezi kuwa JUU ya Katiba. Na sheria yo yote, itakayokwenda kinyume na Katiba, sheria hiyo pia inakuwa batili (unconstitutional). Tunakusudia kusema kwamba, hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA ((Tanzania)) ya 1977, yenyewe, ambayo bado inatumika hadi sasa na imeja viraka, inadhamini UHURU wa wananchi kutowa mawazo na maoni yao kwa uhuru kabisa. Kifungu cha 18, kinachohusiana na haki ya uhuru wa mawazo kinaeleza: “Kila mtu – (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake”. Aidha, kifungu kinachofuata cha 19-(1) nacho kinaeleza: “Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo”. Pia, Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano, Sehemu ya Tatu, inayohusiana na haki na wajibu muhimu, inaeleza kwenye kifungu cha 13-(2) kuwa: “Ni marufuku kwa sheria yo yote iliyotungwa na mamlaka yo yote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lo lote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”. Neno ubaguzi, linatafsiriwa na Katiba hiyo hiyo ya Muungano kwenye kifungu cha 13-(5) kuwa ubaguzi ni pamoja na kunyima haki ya maoni ya kisiasa. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba inakwenda kinyume na Katiba kwa kuikana haki hiyo muhimu ya maoni ya kisiasa.JE MUNATULETEA KATIBA AU MUNATUONGEZEA UDIKTETA NA KUTAKA KUTUMALIZA....?
Tano, UHALALI wa sheria ya mabadiliko ya Katiba hauwezi kupatikana kwa kupitishwa na Bunge pekee. Ni LAZIMA sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba, pia ipitishwe na kuridhiwa na kukubaliwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Baada ya hoja na maelezo hayo, ni ukweli usio na shaka kuwa, sheria ya mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar, na kwa ajili hiyo, Wazanzibari Kikatiba, tunao uhuru na haki ya kutoa maoni yetu bila ya hofu wala woga; kama ambavyo Serikali yetu nayo kupitia Katiba ya Zanzibar, ina wajibu wa kudhamini uhuru huo. Ikiwa ni kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba, na si ule Muungano wa Katiba pia ni haki yetu ya Kikatiba. Zama za kutishana na kupigana zimekwisha. Hata Rais Kikwete katika hotuba yake alilisema hilo, na namnukuu: “Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya,                                               

 nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Tutofautiane bila kupigana”. Mwisho wa kunukuu. Tunamtaka Rais Kikwete atembee juu ya kauli yake hiyo kama ambavyo nasi tutatofautiana kwa misingi ya HOJA bila ya kupigana.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. KWANZA!

HR,TIBAIJUKA,SHAMHUNA,BILALI,SAMIA NYAMBIZI,KUFUTWA KWA MITIHANI NA SASA LA UZINI HIZI ZOTE NI MBINU ZA MKOLONI MWEUSI ILI WAZENJI WASAHAU KUDAI NCHI YAO NA KUSHUGHULIKIA MAMBO MADOGO MADOGO YA KIPUMBAVU WAZANZIBAR AMKENI AMKENI

MIMI SITAKI KUWA KAMA HUYU KAKA ZETU ZANZIBAR INUKENI MUIHAMI NCHI YETU ILI NIENDELE KUWA KAMA NILIVYO INUKENI KAKA ZETU NA BABA ZETU MUIKOMBOE NCHI YETU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
WEZENJI TUNASUBIRI MPAKA DADA ZETU NA WAKE
ZETU WAFANYWE KAMA HIVI NDIO TUPIGANIYE NCHI YETU..?
Imetolewa na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar
TUMEJIFUNGIA na WAZEE na tumekaa tukanong’ona ! Kwanza Serikali ya Tanganyika walituletea sakata la Hamad Rashid, na watu wakalivamia. Ikawa mwezi na nusu Wazanzibari hatujadili tena kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae likaja suala la kuongezwa kwa mipaka ya bahari kuu la Tibaijuka na Shamhuna. Akina Bilali, Samia Suluhu na wenziwao tutajuwana nao BAADA ya kuiweka mezani JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Pia kwa makusudi, wamelizusha suala la kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne. Tunalopaswa kufanya ni kuhakikisha Waziri wa Elimu wa Zanzibar, anatoa ripoti juu ya kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne, pamoja na kutueleza kwa kina mfumo wa mzima wa elimu duni uliopo Zanzibar.
Hivi sasa limezuka suala la uchaguzi mdogo wa Uzini na Chadema kuchukua nafasi ya pili baada ya kuwanunua wapiga kura mamluki. Tujue kwamba, Tanganyika iliyojificha ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitosita na haitolala mpaka tuifuate MILA yao ya kuijadili Katiba ya Muungano KWANZA bila ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Tukiyafuata waliyoyakusudia na wanayoyapanga, tutakuwa tumetoka nje ya kuidai HAKI yetu ya kimsingi ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Hamad Rashid, Bilali, kufutwa kwa mitihani na uchaguzi wa Uzini, zote hizi ni mbinu,kama ile ya popo bawa kama munakubuka na huu ni ujanja na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Kamwe hatutaicheza ngoma yao!
Zamani ilikuwa ni UHAINI kujadili Muungano. Juzi tu, wajanja hawa hawa kwa kutaka kuiendeleza falsafa hiyo yao YAUJINAMIZI NYERERE, wamepitisha sheria Bungeni ya kumchukulia hatua yo yote atakaejadili lo lote ambalo liko nje ya hadudi rejea za rasimu ya Katiba. Kwa mantiki hiyo, yo yote atakaetoa NGUVU ya HOJA ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA na/au Muungano wa Mkataba na kuukataa Muungano wa Katiba wakati wa mchakato wa Katiba utakapokuja, atachukuliwa hatua za kisheria kwa kufikishwa Mahakamani, ili wengine waogope kuendelea kuidai JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR, na badala yake iendelezwe HOJA ya NGUVU na ya UDIKTETAA inayotakiwa ya kujadili Katiba iliyosimama juu ya misingi ya KIKOLONI inayopinga uwepo wa JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR ambayo ndio mbia mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hizo zinazodaiwa kuwa ni hati za Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zilijengwa juu ya taswira ya Muungano baina ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini ya wakati ule, pale Ireland ya Kaskazini ilipokuwa ni koloni la Uingereza.
Kudhihirisha njama za wajanja hawa, juzi tarehe 12 Februari 2012, Halmashauri Kuu ya CCM kwa makusudi, imeifanyia marekebisho Katiba ya CCM yenye lengo la kuwaangusha na kuwadhibiti – MASHUJAA wa MARIDHIANO yetu yaliyo HALALI Kikatiba, na badala yake, kuwabeba VIBARAKA ambao wameonesha wako tayari kuiuza Zanzibar na Wazanzibari kwa UTASHI wa UBINAFSI unaoongozwa na uroho na ulafi wa madaraka.
WAZANZIBARI po pote tulipo duniani TUMESHA AMKAA na KUSIMAMA KIDETE kwa kuelewa kuwa, yote haya ni katika mbinu chafu, hadaa, ghilba na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuipigania na kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Tusikubali, na kwa hakika HATUTAKUBALI kuondolewa kwenye njia na lengo letu hilo HALALI la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye hadhi yake kitaifa na kimataifa; maana sisi wananchi wa Zanzibar, tuna mamlaka na haki ya Kikatiba katika kuendesha nchi yetu kama Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inavyoeleza kwenye Sura ya Pili: (a) “Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe”.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA! SIO KISHEIN,IDDI AMINI DADA WALA MWENGINE YOYOTE YULE ZANZIBAR LAZIMA IWE NCHI HURU KAMA ILIVYOKUWA HAPO AWALI HAKUNA HILI WALA LILE.

Tuesday, February 14, 2012

MAALIM AKIMWAGA VITU VYAKE KAMA KAWAIDA YAKE KACHUKUWA KAWEKA BWAAA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili HALI YA SIASA ZANZIBAR huko hoteli ya Bwawani. Mkutano huo umeandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia ((Tanzania))TANGANYIKA (REDET)
Huwezi kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kwa ufasaha kabisa bila ya kugusia suala la Muungano wa Tanzania, na ndio maana utaona masuala ya Muungano kwa Zanzibar hupewa uzito na umuhimu wa kipekee na wananchi wetu. Hivi sasa wananchi wana shauku kubwa na hamu ya kutoa maoni yao juu ya Katiba mpya, wakiamini kwamba ndio njia muafaka kumaliza malalamiko yao ya siku nyingi. Miongoni mwa hayo ni yale yanayogusa uchumi wa Zanzibar na siasa kwa ujumla. Utaona ni kwa jinsi gani Wazanzibari wanavyoguswa na suala hilo, pale walipoletewa rasimu ya awali ya mswada wa sheria ya kuweka utaratibu wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya walivyojitokeza kwa wingi kuujadili na kufikia hatua ya kuukataa kwa sauti moja. Kwa Wazanzibari ambao wao wanayo katiba yao iliyo sawa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, suala kubwa kwao katika kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ni nafasi ya Zanzibar katika Muungano utakaotoa haki sawa kwa washiriki wa Muungano huo, bila ya kuwa na dhana ya mkubwa na mdogo au BIG BROTHER. Mambo gani yawe ya Muungano. Aina ya Muungano: Je uwe kama ulivyo sasa, uwe wa serikali tatu au uwe ni Muungano wa mkataba kwa mambo tutakayokubaliana, badala ya kuwa Muungano wa kufungana Kikatiba.
HOTUBA YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MHESHIMIWA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA PILI WA HALI YA SIASA ZANZIBAR HUKO HOTELI YA BWAWANI, MJINI ZANZIBAR – TAREHE 13, FEBRUARI, 2012
Mheshimiwa Mwenyekiti wa mkutano,
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala,
Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Waheshimiwa Wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,
Waheshimiwa Mabalozi na Wana Diplomasia,
Waheshimiwa waalikwa wote, Mabibi na Mabwana.
Assalam Alaykum
Kwanza kabisa sinabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwa wazima wa afya nakuweza kukutana hapa leo kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya siasa na maendeleo ya nchi yetu. Tumshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa kutuwezesha kufika salama katika ukumbi huu, hasa kwa vile miongoni mwetu wamo waliotoka mbali, kuja kujumuika nasi katika mkutano huu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kuufanya mkutano wetu huu na kumaliza kwa salama na amani na kile kitakachozungumzwa kiwe ni kwa manufaa na chenye maslahi kwa nchi yetu na watu wake. AMIN.
Kwangu mimi binafsi najiona ni mwenye bahati kubwa kwa kualikwa hapa Hoteli ya Bwawani kufungua rasmi mkutano ulioandaliwa kujadili kwa kina `Hali ya Siasa Zanzibar’, ambapo mada kuu ni UIMARISHAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR.
Nimeambiwa kwamba huu ni mkutano wa pili wa namna hii kuitishwa. Ninawapongeza waandaaji wa mkutano huu, yaani Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kutualika sote kwa mara nyingine tena, kuja hapa kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu siasa hapa Zanzibar. Napenda pia kuwashukuru waandaaji kwa kutenganisha sehemu mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na mikutano hii ya hali ya siasa kwa sababu kwa muda mrefu kulikuwa na mkutano mmoja tu kwa ajili ya Tanzania nzima.
Kutokana na kuanzishwa kwa utaratibu huu wa sasa, Zanzibar ina nafasi kubwa ya kuangalia na kujadili siasa zake kama Zanzibar, jambo ambalo naamini litaleta manufaa zaidi kwa siasa katika visiwa vyetu. Katika kuthibitisha hilo, hata mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ambayo ni “Uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar”, inalenga zaidi kupata mawazo na michango itakayozidi kuleta ufanisi katika utendaji wa serikali yetu, tukumbuke pia mafanikio ya Zanzibar ni maslahi ya Watanzania wote.
Kwa mtazamo wangu, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni imara. Mada ijikite katika kuimarisha zaidi mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hivyo naamini katika siku mbili hizi za mkutano huu, wajumbe watapata nafasi ya kuangalia, kurejea na kupendekeza namna ya kuufanya mfumo huo uwe madhubuti zaidi na kupendekeza pia jinsi ya kuendesha siasa hapa Zanzibar kwa manufaa ya wananchi wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imetokana na matakwa ya wananchi wenyewe wa visiwa hivi, baada ya kuona mfumo uliopita yaani mfumo tenganishi hauna faida kubwa katika kujenga umoja na kukuza maendeleo ya Wazanzibari. Na kama ilivyo katika mataifa mengine, mfumo wowote mpya unapoanzishwa huwa unakuja na changamoto mbali mbali,hivyo kuhitajika marekebisho ya hapa na pale, ili kuufanya uweze kufanikisha malengo yaliyokusudiwa tangu mwanzo. Uzuri ni kwamba Zanzibar ina fursa nzuri ya kuweza kujifunza kupitia sehemu nyingine za dunia, ambazozina serikali zenye mfumo wa aina hii.
Vile vile ni jambo la kutia moyo sana, kwetu sisi Wazanzibari, Watanzani na hata jumuiya ya Kimataifa kuona kwamba hapa Zanzibar katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa serikali shirikishi tunashuhudia faida nyingi. Faida kubwa moja wapo ni maelewano makubwa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar. Sote ni mashahidi kwamba, kabla ya kuja kwa utaratibu huu tulikosa kuwa na maelewano, hali iliyokuwa imesababishwa kwa kiasi kikubwa na kutafautiana kwetu katika itikadi za kisiasa na kukosa mashauri ya pamoja katika kuendesha nchi yetu na kujiletea maendeleo.
Katika Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa serikali shirikishi tunashuhudia wananchi wenye itikadi tafauti pamoja na viongozi wao, wakikaa pamoja wakishirikiana katika kila uwanja wa maisha na zaidi katika mambo ya kuwaletea maendeleo yao. Sina budi kukiri kwamba changamoto za hapa na pale zinatokea na hazitaacha kutokea, lakini kutokana na utaratibu tuliojiwekea kuweka maslahi ya wananchi wetu mbele, changamoto zinapojitokeza tunakaa pamoja kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi kwa haraka.
Viongozi na watendaji wa REDET, na takriban wajumbe wengi ninaowaona katika mkutano huu, nyote ni mashahidi juu ya hali ilivyokuwa Zanzibar, ambapo maelewano kama haya tunayo yazungumzia hii leo, ikiwemo watu kutoka vyama tafauti vya kisiasa kupanga mambo yao kwa pamoja na kujadiliana mustakabali wa Zanzibar na baadaye kutoa maamuzi yaliyojikita katika kuendeleza nchi na wananchi wote haikuwa rahisi. Kwa niaba yangu na serikali ya Mapinduzi Zanzibar nakupongezeni kwa dhati kwa namna mlivyoshirikiana na mnavyoendelea kushirikiana nasi na kutupa ushauri katika hatua zote, hadi kufikia hapa tulipo. Nakuombeni msichoke na muendeleze moyo huo huo, na mzidi kushirikiana nasi katika mambo haya yenye maslahi kwa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti na washiriki wa mkutano,
Mada kuu ya mkutano huu ni Hali ya Siasa Zanzibar, hivyo ni vyema nigusie japo kidogo yale yanayohusu mada hiyo.
Siasa ya Zanzibar inajumuisha mlolongo wa mambo mengi na kuweza kuizungumzia kwa kina na ufasaha inahitaji muda mwingi, na sio katika wasaa mdogo kama huu wa ufunguzi wa mkutano. Hata hivyo kwa kugusia japo kidogo nina imani kuwa sote tunakumbuka kwamba, baada ya Uchanguzi Mkuu wa Oktoba 2010, Zanzibar iliunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kuundwa kwa serikali hiyo kulitokana na mabadiliko ya katiba yaliyoruhusu utaratibu huo mpya kutokana na kura ya maoni iliyopigwa tarehe 31 Julai 2010 kuamua iwapo tuwe na serikali ya namna hiyo au laa.
Maamuzi hayo ya busara yalitokana na historia yetu ambayo imekuwa na matukio yasiyopendeza ya kuwa jamii yetu imegawika katika misingi ya kiitikadi na siasa za chuki, ushindani wa kisiasa usiokuwa na tija kwa wananchi wetu, na kutoaminiana baina ya watu wa pande zilizokuwa zinasagana. Hali hiyo ilikuwa ni ya kutisha ukiangalia tulikotoka kama jamii moja na sasa siasa zikaishia kututenganisha na kutufanya mahasimu. Ni dhahiri kuwa wananchi walio wengi walishachoshwa na hali hiyo. Hivyo wananchi walipotakiwa kufanya uamuzi kupitia kura ya maoni juu ya mfumo wa Serikali kuwa shirikishi au tenganishi thuluthi mbili walichagua mfumo shirikishi.
Hali hiyo imesababisha kwa sasa tuwe na maridhiano ambayo yameleta mafanikio kuliko ilivyokuwa kwa Muafaka I na II. Jambo la kupendeza zaidi ni kuwa maridhiano haya yalifanyika baina yetu sisi wenyewe bila shinikizo la nje. Sisi wenyewe Wazanzibari, Watanzania wenzetu wengi na Jumuia ya Kimataifa tumeridhika na utulivu tunaoushuhudia. Kabla ya maamuzi hayo hali ya siasa iliyokuwepo ilifanya shughuli nyingi za kiuchumi kwenda kwa kusuasua, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.
Lakini sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa badala ya kupoteza muda mwingi kushughulikia kutatua migogoro, muda karibu wote unatumiwa kufikiria, kubuni na kupanga mipango ya maendeleo itakayo wanufaisha wananchi. Wawekezaji wa ndani na wa nje wamevutiwa na hali hiyo na wamo katika mazungumzo na taasisi husika kuwekeza nchini Zanzibar.
Mheshimiwa Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano,
Hayo yaliyotokea huko nyuma kabla ya kufikiwa kwa Maridhiano ya Wanzibari yaliendelea kutokea ingawa juhudi kubwa zilishafanywa na zilikuwa zinafanywa zilizolenga kuupatia suluhu ya kudumu mgogoro wa kisiasa Zanzibar. Zipo hatua zilizochukuliwa na serikali zote mbili, ile ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar kwa nia ya kufanikisha azma hiyo. Kwa bahati mbaya, matokeo yake hayakuwa mazuri kama ilivyotarajiwa jambo lililopelekea kujitokeza haja ya kuendeleza kazi hiyo, hadi leo hii ambapo tayari tuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Historia fupi ya Zanzibar inaonesha kuwa wakati wa kupigania uhuru palikuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao uliwatenganisha wananchi katika makundi mawili makuu, kila kundi likiunga mkono chama au muungano wa vyama. Baada ya Mapinduzi ya Januari 1964, tukaingia katika mfumo wa chama kimoja cha siasa ambacho kiliendana na dhana ya chama kushika khatamu, yaani kuwa ndio chombo chenye maamuzi ya mwisho.
Mfumo huo uliendelea kwa takriban miaka ishirini na minane (1964 – 1992). Mwaka 1992 tukaingia katika mfumo wa vyama vingi. Kwa Zanzibar mfumo huu ulipelekea kuwepo kwa vyama viwili vikubwa vya siasa vyenye kulingana kwa kuungwa mkono na wananchi. Misuguano na mikwaruzano iliyokuwepo kabla ya Mapinduzi ikajirudia, siasa ikawa imejengeka juu ya utamaduni wa malumbano, chuki na hasama baina ya wafuasi wa vyama hivyo viwili vya CCM na CUF.
Hali ya mivutano ilikithiri hasa wakati wa uchaguzi hadi kupelekea watu kupoteza maisha, mali kuharibiwa na hata kwa mara ya kwanza Tanzania kuzalisha wakimbizi. Ndio maana juhudi hazikusita kuchukuliwa ili kuiepusha nchi na hasara zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Chaguzi zilizofanyika baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ziligubikwa na kushutumiana kutokana na Tume zilizosimamia chaguzi hizo kutokuwa na uwazi wa kuridhisha. Kulijitokeza kasoro za wazi katika uandikishaji wa wapiga kura, uendeshaji wa mikutano ya kampeni, majukumu katika kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Hivyo basi Serikali ya Mapinduzibaada ya mashauriano na vyama vya CCM na CUF kupitia mazungumzo yaliyozaa miafaka miwili ya 1999 na 2001 ilichukua hatua zilizokusudiwa kusawazisha kasoro hizo.
Miongoni mwa hatua hizo ni ile ya kuanzishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (PVR). Sio kwamba kuwepo kwa Daftari kumemaliza matatizo yote ya wananchi wote kupata haki ya kupiga kura kwani bado malalamiko mengi yapo. Hata hivyo, naamini hii ni hatua muhimu ya kuelekea tunakokusudia na kuhakikisha kila Mzanzibari anapata haki yake ya kuiweka madarakani Serikali anayoiona itaweza kumsaidia kupambana na matatizo yake ya kimaisha.
Uchaguzi wa 2010 ulionesha maendeleo makubwa katika uwanja wa kampeni, vyama vyote vilitumia haki yao ya kufanya kampeni bila ya vizingiti. Kampeni zilikuwa za kiungwana. Pamoja na kuwa na hamasa, lakini kwa kiasi kikubwa hapakuwepo na malumbano, matusi wala kushambuliana. Kila mgombea na chama chake alijikita katika kutetea sera na ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujenga hoja za kuwashawishi wananchi watoe kura zao kwa mgombea na chama chake.
Hata katika siku ya kupiga kura kama mizengwe ilikuwepo ilikuwa michache. Uhesabuji wa kura ulifanyika vituoni. Pengine shaka ilikuwepo katika sehemu za kujumuisha kura na kutangaza matokeo. Walijitokeza maafisa wa ZEC wachache waliojaribu kuchakachua matokeo. Pale mawakala wa vyama walipokuwa macho na kugundua hila hizo, taarifa zilitolewa kwa Tume ya Uchaguzi Makao Makuu na baadhi ya maafisa wa ZEC waliohusika walichukuliwa hatua papo hapo. Haya ni maendeleo mazuri na ni wajibu wote sote kuyaendeleza na kuyafanya kuwa bora zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Eneo jengine ambalo limepata maendeleo ni uwakilishwaji wa wanawake katika vikao vya kufanya maamuzi na katika ngazi za juu za utendaji serikalini, katika Baraza la Wawakilishi, Bungeni, Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya, uwakilishi wa wanawake umefikia au kupindukia asilimia thelathini (30%).Lengo ni kufikia malengo ya SADC ambapo uwakilishi wa wanawake unatakiwa usipingue asilimia khamsini (50%) katika Mabaraza ya Kutunga Sheria. Leo katika Zanzibar yetu kuna wanawake ambao ni Mawaziri, kuna Makatibu Wakuu wa Wizara, kuna wanawake wanaoongoza taasisi muhimu za serikali kama CAG na kadhalika. Ni nia ya Serikali ya Mapinduzikuwashirikisha wanawake wengi zaidi katika nyadhifa za uongozi wa nchi. Na hili linafanyika sio kwa upendeleo wa jinsia, bali kutokana na uwezo wa wanawake wenyewe.
Eneo jengine, ni kuruhusu vyombo huru vya habari. Hii ni moja ya sifa za nchi ambazo demokrasia inashamiri. Vyombo vya habari vimekuwa vikielezwa kuwa ni mhimili wa nne wa dola kutokana na umuhimu wake katika masuala ya kuwaelimisha wananchi kufahamu haki zao kupata taarifa na kusimamia uwajibikaji wa serikali. Ukweli na uwazi, vyote vikiwa ni vigezo muhimu vya viwango vya maendeleo vyombo vya habari vinawajibika kuvizingatia. Kwa mfano wakati wa chaguzi, vyombo vya habari huviunganisha vyama vya siasa na wagombea wake kwa upande mmoja na wapiga kura wao kwa upande mwingine. Aidha, hutumika pia kama jukwaa la kutangazia sera na ilani za vyama vya siasa, kwa kusaidia waangalizi wa chaguzi kufuatilia hali ya kampeni inavyokwenda pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kuwapima wagombea, sera na ahadi za vyama na hivyo kuwawezesha kufanya maamuzi kwa busara.
La tano, Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu miaka ya 1990, nchi yetu imekuwa ikiondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima katika nyanja ya Asasi za Kiraia. Asasi hizi kwa sasa zinafanya kazi kwa uhuru mkubwa na zimekuwa zikichangia kwa namna moja au nyingine katika maendeleo ya wananchi wetu. Haki ya kuunda na kujiunga na vyama vya kiraia ni kiashiria kuwa mfumo uliopo wa kisiasa unafuata njia sahihi ya kuelekea kwenye demokrasia.
Mheshimiwa Mwenyekiti
Mara nyingi asasi hizi za kiraia katika jamii zinaundwa ili kushughulikia matatizo ya kawaida, vipaumbele vya kikundi, maadili na tamaduni. Juhudi zitokanazo na ushirikiano wao zinaweza kusaidia katika shughuli mbalimbali. Asasi hizi zimefanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu mchakato wa kujenga demokrasia nchini, hasa kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa na katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Tafiti zimeonesha kuwa migogoro mingi baina ya dola na asasi za kiraia, chanzo cheke ni pale asasi zinapoona au kudhani kuwa wadau wao wanatengwa katika michakato ya ufanyaji maamuzi, na hasa maamuzi yale yanayoathiri ustawi wa maisha ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano
Kwa kifupi lengo kuu la juhudi zote hizo ni kuifanya Zanzibar kuwa ni nchi iliyopiga hatua kubwa katika kukuza demokrasia, kuheshimu haki za binaadamu na kujenga misingi ya utawala bora. Kwa maneno mengine kuiwezesha nchi yetu kuwa na,
1. Kiwango cha juu cha Demokrasia.
2. Serikali yenye mihimili mitatu inayofanya kazi zake kwa uhuru na kila mmoja kuhakikisha muhimili mwengine hauvuki mipaka yake (cheks and balances).
3. Wananchi wenye uelewa mkubwa, iliwaweze kushiriki katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya mambo yao kwa maslahi yao na kwa nchi yao.
4. Haki za binaadamu zinaheshimiwa, zinalindwa na kuendelezwa.
5. Vyombo vya habari vinafanya kazi kwa uhuru, lakini kwa kuzingatia weledi na maadili yao.
6. Uhuru, haki na fursa sawa kwa raia wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti na washiriki wa mkutano,
Kwa ujumla hali ya kisiasa ya Zanzibar hivi sasa ni shwari, na kama nilivyogusia hapo awali, wananchi wanafanya shughuli zao za kisiasa, kijamii na kimaendeleo bila ya bughudha yoyote ile. Haya ni maendeleo makubwa tukilinganisha na tulikotoka. Kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika mfumo wa vyama vingi ni hatua kubwa sana, ambayo inaonyesha upevu wa kisiasa ambao utaiwezesha nchi yetu isonge mbele kimaendeleo kwa kasi zaidi. Ile tabia ya kupingana kwa sababu tu za kisiasa imepungua sana na kuelekea kwisha kabisa, jambo ambalo litawezesha serikali kufanya maamuzi kwa haraka na ambayo yatakubalika kwa wananchi wa mirengo yote mikubwa na viongozi wao.
Kukubali kuachana na siasa za ‘mshindi kuchukua kila kitu’ na kuamua kukaa pamoja na kuunda serikali ambayo itapata mchango kutoka kila chama kilichohusishwa katika kuunda serikali hiyo ni suala muhimu, kwa vile linawashirikisha wengi kwa maslahi ya taifa na watu wake. Ile dhana tu ya ‘Umoja wa Kitaifa’ ni kitu cha kutia moyo.
Hivi sasa wawekezaji wanavutiwa na hali ya amani na utulivu ya Zanzibar, ambayo hujenga mazingira bora katika shughuli za uwekezaji na shughuli za kiuchumi kwa jumla. Wawekezaji hao wamekuwa wajijitokeza katika kuonesha nia ya kufungua miradi yao Unguja na Pemba.Hatua hii itachangia kwa kiasi kikubwa wananchi wetu kupata ajira na kuimarisha hali zao za kiuchumi.
Aidha, hivi sasa Wazanzibari wote wanachangia na kushiriki katika harakati za maendeleo ya nchi yao, miongoni mwao ni wale Wazanzibari ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi nje ya Zanzibar yaani ‘Diaspora’. Wazanzibari hao wamekuwa wakielezea kufurahishwa kwao na hali iliyopo ya umoja na maelewano. Baadhi yao wamekuwa wakifuatilia hatua zitakazowawezesha kutumia fursa hiyo kufungua miradi ya kiuchumi itakayowanufaisha wao na jamii nzima ya Wazanzibari. Pia wamekuwa wakijumuika kusaidia wanajamii wenzao hapa Zanzibar, kama vile kwa kuleta kama misaada, vifaa vya elimu, matibabu na fedha taslim kuchangia miradi ya kijamii.
Wako wale walioonesha utayari wao wa kuja kutumia taaluma zao katika kuitumikia nchi yao wakati wanapokuwa katika likizo zao. Hata wale ambao wamestaafu, lakini bado wana nguvu za kimwili na akili wameonesha hamu ya kuja kutumikia Zanzibar na watu wake. Haya yasingeweza hata kufikirika huko nyuma.
Hali hii inanikumbusha swali aliloulizwa mtaalamu mmoja wa nchi ya Liberia, kwa jina akiitwa Mr. Johnson, aliulizwa, ni vipi hali ya amani itakuza uchumi wa nchi hiyo, ambapo jawabu lake rahisi lilikuwa, ‘Nadhani ni pale mioyo ya wananchi wote wa Liberia itakapokuwa imejawa na mapenzi na hamu ya kuwepo amani katika nchi yao, hali hiyo itaepusha machafuko na wafanyabiashara watawekeza miradi itakayosaidia kukuza uchumi wa nchi’.
Majibu ya mtaalamu huyo wa Liberia pia ni darasa tosha kwa Zanzibar,ambayo inahitaji sana kuwa na amani na utulivu, ili iweze kujenga imani kwa wawekezaji na kuondokana na uchumi dhaifu unaosababisha wananchi wetu kukabiliwa na hali ngumu ya umasikini.
Kwa upande wa kijamii hivi sasa tunashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wananchi wetu. Kwa mfano katika tukio la ajali ya kuzama kwa meli ya MV. SPICE ISLANDER, mwezi Septemba mwaka jana hapa Zanzibar, umoja na mshikamano ulioonyeshwa na Wazanzibari ulidhihirisha wazi namna wananchi walivyokuwa wamoja. Wengi wetu tumekuwa tukijiuliza, iwapo tukio lile lingetokea wakati ule ambapo hakuna maelewano miongoni mwetu hali ingekuwaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano,
Huwezi kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kwa ufasaha kabisa bila ya kugusia suala la Muungano wa Tanzania, na ndio maana utaona masuala ya Muungano kwa Zanzibar hupewa uzito na umuhimu wa kipekee na wananchi wetu. Hivi sasa wananchi wana shauku kubwa na hamu ya kutoa maoni yao juu ya Katiba mpya, wakiamini kwamba ndio njia mfuaka kumaliza malalamiko yao ya siku nyingi. Miongoni mwa hayo ni yale yanayogusa uchumi wa Zanzibar na siasa kwa ujumla. Utaona ni kwa jinsi gani Wazanzibari wanavyoguswa na suala hilo, pale walipoletewa rasimu ya awali ya mswada wa sheria ya kuweka utaratibu wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya walivyojitokeza kwa wingi kuujadili na kufikia hatua ya kuukataa kwa sauti moja. Kwa Wazanzibari ambao wao wanayo katiba yao iliyo sawa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, suala kubwa kwao katika kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ni nafasi ya Zanzibar katika Muungano utakaotoa haki sawa kwa washiriki wa Muungano huo, bila ya kuwa na dhana ya mkubwa na mdogo au BIG BROTHER. Mambo gani yawe ya Muungano. Aina ya Muungano: Je uwe kama ulivyo sasa, uwe wa serikali tatu au uwe ni Muungano wa mkataba kwa mambo tutakayokubaliana, badala ya kuwa Muungano wa kufungana Kikatiba.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, mimi mwenyebinafsi na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd pamoja na viongozi wengine serikalini, tumekuwa tukiwahimiza wananchi kufuatilia kwa makini mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano, ili waweze kujipanga vizuri na wakati utakapofika waweze kutoa maoni yao juu ya katiba hiyo mpya wanayoitaka, ambayo wanahisi itakuwa yenye maslahi sawa kwao na Zanzibar na kwa wenza wa Tanganyika. Wananchi wanapaswa kuifanya kazi hiyo wakati utakapofika, bila ya woga, la muhimu watoe maoni yao kwa ustaarabu mkubwa na bila ya kuwatukana watu wengine.
Wakati wa kutoa maoni juu ya katiba mpya utakapofika wananchi kote nchini watapata fursa ya kipekee kuujadili Muungano wao na baadaye kutoa maamuzi yanayofaa, ili kumaliza migogoro, na manung’uko yasiyokwisha baina ya pande mbili zinazounda Muungano huo, malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa wingi na kutishia uimara wake, tangu muungano huo ulipoasisiwa mwaka 1964.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Naona niangalie kwa ufupi changamoto tulizonazo ambazo ni nyingi na zenye uzito wa aina yake. Kama ambavyo mnaelewa serikali za Umoja wa Kitaifa popote pale duniani hukabiliwa na changamoto nyingi na wahusika wasipokuwa makini wanaweza kuhisi kwamba mifumo ya serikali za aina hiyo sio hatua muafaka kufikia pale wanapotarajia. Hata hivyo kwa upande wa Zanzibar hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa bila ya mivutano katika kupata viongozi kutoka kwenye vyama husika au sera na miongozo inayopaswa kutumika katika kuendesha serikali yenyewe.
Mafanikio haya bila shaka yametokana na kufuata Katiba ya Zanzibar ya 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2010. Hata pale zinapojitokeza changamoto za hapa na pale, tumekuwa tukikabiliana nazo kwa majadiliano ya uwazi na kupata maelewano na baadaye kuendelea mbele.Naamini chini ya utaratibu kama huo na kwa mashirikiano na pande nyengine na kwa kuthamini fikra za kitaalamu kama zile tunazotarajia kuzipata kupitia mkutano huu, tutaweza kusonga mbele zaidi na kufikia malengo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano,
Miongoni mwa changamoto tulizonazo ni ukweli kwamba hadi leo wapo baadhi ya viongozi na watu ambao hawafurahishwi na Maridhiano ya Wazanzibari.Watu hao ni wachache.Baadhi yao wamekuwa wakijaribu kutia fitna ili kuvuruga maelewano, kwa bahati mbaya yako magazeti machache yanayotolewa Tanzania Bara ambayo yamepania kuleta chochoko ili kuvuruga kuaminiana kuliko jengeka.Hata hivyo, kwa vile walio wengi wanaona umoja wetu huu unafaida kubwa zaidi, kuliko hasara watu hao hawatafanikiwa. Ni wajibu wetu sote kuendelea kuwaelimisha watu hao, ili nao baadaye waone umuhimu wa umoja wa Wazanzibari na waweke mbele maslahi ya wengi kuliko ya wachache, na kwa hakika watu wa aina hii wanapungua kila kukicha.
Changamoto nyengine tunayokabiliana nayo ni katika kukidhi matarajio makubwa ya wananchi juu ya serikali yao, pengine kuliko hali halisi ilivyo. Wananchi wengi walitarajia serikali yao itaweza kutatua kwa muda mfupi kero kubwa zinazowakabili katika maisha, kama vile mifumko ya bei za bidhaa muhimu na kuwepo hali ngumu ya maisha.
Serikali hii tokea ilipoanza kazi imekuwa ikichukua hatua kubwa kuhakikisha ugumu wa maisha ya Wazanzibari unapungua, na wananchi kote Unguja na Pemba wanapata nafuu katika maisha. Hata hivyo, uhaba wa fedha serikalini pamoja na hali isiyotarajiwa inayojitokeza ulimwenguni, kama vile kupanda kwa bei ya mafuta mara kwa mara, kushuka thamani ya shilingi dhidi ya dola, uharamia katika bahari yetu ya Afrika Mashariki, pamoja na majanga ya ukame na mafuriko katika nchi tunazo zitegemea zaidi kununua bidhaa za vyakula, baadhi ya wakati huchangia kutofikiwa malengo yetu.
Serikali inachukua juhudi kubwa kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi, kama tusemavyo Waswahili, ‘Kata pua uunge wajihi’, baadhi ya wakati tunalazimika kupunguza kodi za bidhaa zote muhimu, kwa kuzingatia hali za maisha ya wananchi wetu.
Tunalazimika kuchukua hatua hizo kwa kuzingatia kuwa, hali ngumu za kimaisha si jambo la mchezo na tayari tumepata fundisho kubwa kwa yale yanayotokea katika baadhi ya nchi, kama huko Mashariki ya Kati, ambapo kwa upande mwengine ugumu wa maisha umechangia hayo yanayotokea.
Kwa upande mwengine uhaba wa fedha unahusishwa pia na baadhi ya kasoro zinazojitokeza, ikiwemo kuchelewa kufanyiwa mapitio daftari la kudumu la wapiga kura Zanzibar, ambalo wananchi waliahidiwa lingefanyiwa mapitio hayo katika mwezi Oktoba wa kula mwaka, lakini hadi sasa kazi hiyo haijafanyika. Bado kuna tatizo la wananchi wasio kuwa haba kupambana na vikwazo katika kupata vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ambavyo ndivyo sharti la lazima la kumuwezesha mwananchi kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Masheha kwa bahati mbaya, wanahusishwa kuwawekea vikwazo wananchi hao kupata vitambulishio hivyo.
Changamoto hizi zinafahamika na Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hatua za kuzimaliza zinajadiliwa.
Ukitulinganisha sisi Wazanzibari na wenzetu wa nchi nyengine zilizokumbwa na mgawanyiko wa raia wake, sisi tumeanza vizuri na tunaendeela vizuri. Ni matumaini yangu kuwa Zanzibar itaendelea kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyengine, ikiwemo Tanzania Bara, katika kuendeleza, amani utulivu, mshikamano na maelewano miongoni mwa wananchi wake.
Baada ya kusema hayo machache naomba kuwashukuru wote kwa uvumilivu wenu wa kunisikiliza kwa makini.
Basi niruhusuni nitamke wazi kuwa Mkutano wa Pili wa Hali ya Siasa Zanzibar nimeufungua Rasmi

KILA SIKU TUNAULIZA NANI ANAYE IUWAA ZANZIBAR......?


KWA JINA LA BABA NA LAMWANA NA LA ROHO MTAKATIFU AMIIN

WASIA WA BABA WA WAKOLONI WAUSI TANGANYIKA KWA KUITAWALA ZANZIBAR KWA MABAVU NA NGUVU ZA JESHI

HAPA NDIO MACHIJIONI WANAPO TUCHINJA SISI WAZENJI

UDOMU UKOLONI MWEUSI UDUMU UNYANYASAJI WA WANANCHI NA KUWAWACHA MASIKINI

LAZIMA ZANZIBAR TUIGEUZE KUWA DANGURO

SWALA YA IJUMAA HAIWAPITI NA MUNAJUWA FIKI MATHUMUNI YA CHAMA HICHI ILA MUMEHADAIKA NA DUNIA NA KUSAHAU M/MUNGU ILA MUJUWA KIFO HAKIKO MBALI NA NYINYI MUTAULIZWA SIKU YA KIAMA MULIKUWA VIONGOZI NINI MULICHOKIFANYA KTK UWONGOZI WENUUUUUUUUU ..? HAPO SASA.

Monday, February 6, 2012

NDIO MAANA SHAMHUNA AKAONA BORA YEYE AUZE BAHARI MAANA NCHI ISHAUZWA ZAMANI HAHAHAHA


JAMBO JAMBO BWANA HABARI GANI MUZIRI SANA VICHOGO MUNAKARIBISHWA ZANZIBAR YETU HAKUNA MATATA JAMBO JAMBO MASAI HABARI GANI MZURI SANA MASAI UNAKARIBISHO ZANZIBAR YETU HAKUNA MATATA ZANZIBAR NCHI NZURI HAKUNA MATAT INAUPEPP WA MARASHI YA KARAFU HAKUNA MATATA

HAYA HII NDIO MATHARI YA DARAJANI ILIVYO SASA HAPA ZANZIBAR LUBEGA,RUNGU,NA JISU KUBWA KIUNONI JE HII NI ZANZIBAR SASA AU UMASAINI..?

KAMA KAWA MZEE NDANI YA NJANCHIBALIIIIIIIIIIIIII

Friday, February 3, 2012

UMASIKINI NCHINI ZANZIBAR UNAZIDI KUONGEZEKA NA MAPINDUZI DAIMA YANAZIDI KUTAJIRIKA WAZENJI MPOO AU MUME LALA FOFOFO....?


kuna tafauti gani kati ya zanzibar 1888 na hii zanzibar ya leo ya 2012..?
huyu ni mzizi na ana watoto hao wanne na wote kawapakia ktk baskili anawapeleka skuli na kila siku kwenye vyombo vya habari utasikia oooh mapinduzi daima ni kuja kuondowa umasiki je umasikini huwo munaouzungumza ni umasikini gani haswa...? wawananchi.. au wamatumbo yenu nyinyi viongozi wa zanzibar..? ikiwa ni wawananchi basi toka 1964 mpaka leo 2012 hakuna moja lililofanyika la maana zaidi ya kuwa na viongozi wengi ndani ya baraza la wawakilishi na maraisi watatu na wabunge kibao.lakini mwananchi maisha yake yako pale pale na kila kukicha ndio yanazidi kuporomoka.lakini ikiwa munazungumza kuhusu umaskini wenu nyinyi viongozi basi sawa hamuna tena umasikini maana hakuna hata mtoto wenu moja anapelekwa skuli na basikili kama hivi au yuko....? je mapinduzi ni ya wananchi au ni ya nyinyi viongozi kuwapinduwa wananchi na kuwawacha katika hali ya umasikini..?nitaweka hapa picha za magari yenu ili tuone kama kweli nyinyi munawajali wananchi au ni matumbo yenu na famili zenu tu.
zanzibar nchi masikini ila kila baada ya miaka mitano ukimalizika uchanguzi tu viongozi wanapata magari kama haya au kuliko haya wananchi wanapata nini wakati wa kampeni taraabu na utenzi na ubale wa kanga na panga au shoka je huo umapinduzi wenu wakuja kuwaondoleya watu umasikini ndio huu...?
HIVI NI MILLIONI NGAPI KUCHONGESHA DESK MOJA..?
NA NI ELFU NGAPI KUNUNUWA MAGARI YENU NYINYI VIONGOZI WA ZANZIBAR..?
MAPINDUZI DAIMA....MAPINDUZI DAIMA....MAPINDUZI DAIMA
ILA KWA VIONGIZI TU RAI KULENI MIHOGO MIKAVU NA MASHELISHELI MPAKA MUZIBE CHOO KWA MIHIGO MINGI

Thursday, February 2, 2012

BANDARI YA NCHI YETU YA ZANZIBAR NI BANDARI AU SOKO,JAA,DANGURO NA MAGENGE YA MAMA NTILIYE KUTOKA NCHI YA JIRANI TANGANYIKA..?


Hali ya mandhar ya bandari ya Zanzibar mnaiona, kw akila msafiri na mpita njia. Hali ya mandhari ya bandari hii, ambalo ni lango kuu la kuingilia wasafiri, na uchumi wa Zanzibar hairidhishi, na inatisha, na ni AIBU kwa nchi.
Eneo la nje ya Bandari kwa sasa limejaa biashara za kipuuzi, kama kuuza kadi za simu – zimetanda mwanzo hadi mwisho, kuuza supu, maziwa, na aina zote za biashara zisizostahiki kufanywa pale eneo la bandarini.
Kuna mmachinga pale (mfalme wetu) anakuwa na gari lake la kukokota (tram/rikwama), huyu anauza mpaka condom ukitaka, anazo pia packet za konyagi (ulevi) na kila laana unayoijua wewe pale inapatikana.
Inasikitisha sana kuona hali kama hii imepata blessing na SMZ-GNU under waziri Hamad Massoud (CUF). Yeye kwa bahati nzuri au mbaya – ofisi yake ipo mbele ya uchafu huu.
Awali, alianza kuuz amaziwa bibi mmoja kutoka Bara (Tanga) – huyu alikaa chini ya mlango wa kuingilia, na mpaka sasa yupo. Then, walifuata wengine, mpaka machangu doa wapo pale.
Hivi kweli Waziri Hamad Massoud haoni, au dr.Shein, au Balozi na Maalim Seif …wanapita pale kila siku.
Ukiangalia sana, hata usalama wa pale eneo la bandari ni mdogo sana.
Inanishangaza sana kusikia na kuona Dr.Shein anawaita watendaji Ikulu (ikiwemo wizara hii) ya mawasiliano na miundo mbinu – na anawasifu kwa utendaji mzuri. Hivi huu ndio utendaji mzuri? Mbaya utakuwa upi?
Imekuwa fashion Dr. Shein kuziita Wizara na kuwasilisha work plan zake, hivi kweli mambo kama haya hayaonekani au kwa sababu wauzaji na wafanya biashara hii ni ‘wafalme wetu’ kutoka Tanganyika. Nina hakika ingalikuwa jamaa zetu kutoka Kengeja, Tundauwa, Matangatuani, Finya n.k Wallah wangalikuwa wameshafukuzwa pale. Lakini hawa wengi wao wanatokea huko ‘baitil muqadas’ wafalme wetu ama wametokea Tanga au Rufiji au Kilwa, Mtwara, Temeke n.k – untouched family.
Zanzibar, kimtazamo, wa identity imekwisha sana, haina tena nasaba au mpaka wa kujua nani ni nani, imekuwa mkorogo tu, na uongozi/viongozi wanachangai hili, na GNU ndio imekuja kumaliza, na kuimaliza Zenj Empire. Viongozi wake ni corrupt sana sana.
Kama kweli SMZ-GNU ina nia ya dhati juu ya kuweka mipnago mizuri ya bandari – basi wafanya biashara hawa, wakiwemo wauza supu, maziwa, na wale wafalme wetu pia waondoshwe pale eneo la bandari ya Zanzibar. Natoa hii challenge kwa Hamad Massoud, SMZ, Dr.Shein na VP1 and VP 2.((VP2 SIO SANA MAANA TUNAMJUWA NI DUNGU YAO JE NYINYI MULIOBAKIA....? ))

JE RAISI WA ZANZIBAR NDIYE AMIRI JESHI MKUU WA JESHI LA ZANZIBAR AU NIKIJIBARAKA TU CHA AMIRI JESHI WA TANGANYIKA...?


WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelieleza Bunge kuwa, Rais wa Zanzibar si Amiri Jeshi Mkuu.
Waziri wa Wizara hiyo, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema leo kuwa,tanganyika ((Tanzania)) ina Amiri Jeshi Mkuu mmoja ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa ((Tanzania.))FEKI
Dk. Mwinyi ametoa msimamo huo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), ambaye aliuliza ni sheria ipi imempa mamlaka Rais wa Zanzibar kuteua vikosi maalum vya ulinzi hivyo kusababisha TANGANYIKA ((Tanzania)) iwe na maamiri jeshi wakuu wawili ndani ya nchi moja.((HAKUNA NCHI MOJA NCHI NI MBILI MUKITAKA MUSITAKE))
Kwa mujibu wa Dk. Mwinyi, Katiba ya Zanzibar ndiyo inayompa Rais wa Zanzibar kuteua idara maalum za ulinzi kikiwemo Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Mafunzo.
Awali wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), Dk. Mwinyi aliwaeleza wabunge kuwa, jukumu la ulinzi majini ni na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) na kwamba, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (NAVY) inalinda Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema, kuna mikakati ya kuiimarisha Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, kivifaa ili pia kuliwezesha kupambana na maharamia wa Kisomali.((uzushi mtupu somalia iko wapi na zanzibar iko wapi kama ni kupambana si kenya wanayo NAVY ila huu ni uzushi tu natusipo angali tutatiwa tena vita kama vita vya uganda na tanganyika kisha dungu zetu wakauliwa na kufanywa viwete mpaka leo hawajalipwa))
Kai alisema, usalama wa Zanzibar unatokana na bahari hivyo alitaka kufahamu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) ina mikakati gani kukisaidia kikosi cha KMKM.
“Si rahisi kuisaidia KMKM kivifaa kwa sababu hata Navy yenyewe haijajitosheleza” amesema Dk Mwinyi.
Wakati anajibu swali la msingi la Mbunge huyo, Dk Mwinyi alisema, Katiba ya TANGANYIKA  inaruhusu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuunda na kuweka TANGANYIKA(( Tanzania)) majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania)) ukiwemo wa maeneo ya bahari na maziwa ya nchi yetu.
“Jukumu la ulinzi wa maji katika maeneo yote ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) linatekelezwa na JWTZ kupitia Kamandi ya Jeshi la la Wanamaji (NAVY)” amesema Dk. Mwinyi.
Amesema,Serikali ya Jamuhuri ya Muungano imekuwa ikiisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa mafunzo kwa maofisa na askari wa KMKM.
Wakati huohuo, Dk. Mwinyi amesema, amewaeleza wabunge kuwa, hakuna wakati au mazingira yatakayolifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania)) (JWTZ) kufanya kazi za ndani badala ya Jeshi la Polisi.((HII SIO KWELI MAANA KILA CHANGUZI JESHI LIMEUWA WAZANZIBAR NA POLISI PIA KWA HIYO JESHI LANAFANYA KAZI NDANI YA KUTUWA SISI HAPA PEMBA NA UNGUJA WAKATI WA UCHANGUZI))MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU.SEMENI KWELI.
“…bali Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania ))linaweza kusaidia pale Jeshi la Polisi linapoelemewa na kuoombwa kufanya hivyo” amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Mwinyi, msaada wa JWTZ kwa shughuli za ndani si katika masuala ya usalama wa ndani tu, bali jeshi linaweza kuombwa kusaidia katika shughuli nyingine inapobidi kama vile shughuli za uokoaji, ujenzi hususani nyakati za dharura na majanga((NA HASWA WAKATI WA UCHANGUZI WATUWE NA KUHARIBU DADA ZETU MPAKA TUKAKIMBILIA MOMBASA 20001 AU MUSHASAHAU AU MUNAJISAHAULISHA................?

Wednesday, February 1, 2012

MKAPA ATAFIKISHWA LINI (( ICC )) THE HAGUE NCHINI UHOLANZI KUELEZEYA NI KWANINI ALIWAULISHA DUNGU ZETU UNGUJA NA PEMBA...?

HUYU NDIYE ALIYE WAULISHA NDUGU ZETU
UNGUJA NA PEMBA JANUARI 27,2001
HIVI karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imewatia hatiani watuhumiwa wanne kati ya sita waliofikishwa katika mahakama hiyo, hivyo watakabiliwa na kesi ya mauaji na vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwaka 2007.
Watuhumiwa hao wamekutwa na hatia mjini The Hague, Uholanzi baada ya jopo la majaji chini ya uongozi wa Jaji, Ekaterina Trendafilova kuwasilisha uamuzi wao kwa watuhumiwa baada ya maelezo ya awali ya pande zote.
Wakati hayo yakitokea Kenya, hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF kimeadhimisha miaka 11 tangu yatokee mauaji na mateso kwa viongozi na wanachama wake baada ya kufanya maandamano makubwa katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba ili kupinga matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2000.
Maandamano hayo yaliyofanyika Januari 27, 2001 yalikabiliwa na polisi na kusababisha vifo na majeruhi. Hadi sasa idadi ya vifo inayotajwa na serikali ni watu 34, lakini kuna madai kuwa waliokufa ni wengi zaidi ya hao. Wengine walipoteza mali zao na mbaya zaidi, Tanzania ilizalisha wakimbizi baada ya baadhi ya wananchi kutoka kisiwani Pemba kukimbilia Mombasa.
Kutokana na tukio hilo wapo baadhi ya Watanzania wanafikiria kuishitaki serikali ya Tanzania ICC kama ilivyofanyika kwa Kenya.
Kwa sasa tunakusanya ushahidi ikiwa ni pamoja na kuwahusisha viongozi waliokuwepo kama vile aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Seif Khatib na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Omar Mahita. Vielelezo vitakapo kamilika tutapeleka kesi mahakamani anasema mmoja wa Watanzania ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini ili kulinda ushahidi wake.
Hata hivyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za binadamu ndani ya CUF Salum Bimani anasema kuwa chama chake kinasubiri maamuzi ya Bunge ili kuhakikisha kuwa madhila yaliyowapata wanachama na viongozi wake yanapatiwa ufumbuzi.
Kwa sasa tunasubiri maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, kwasababu tuliahidiwa kuwa suala hilo litajadiliwa na litapatiwa ufumbuzi anasema Bimani.
Akizungumzia suala la kuishitaki serikali ICC, Bimani anasema kwa sasa chama chake hakina mpango huo, ila kama kuna watu watajitokeza kufanya hivyo chama kitawaunga mkono.
Kwa sasa hatuna mpango huo, lakini kama kuna watu wamejitokeza kushitaki, sisi tutawaunga mkono katika hilo.pia kuna moja wa vijana ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa mdogo wake alipingwa risasi kwenye mlango wao haswa huko pemba.nasama hivi viongozi kama hawa lazima washughulikiwe na kuhukumiwa ndio nchi hii itasonga mbele kimaendeleo la kama hawa wakifanya ni hewala bwana kama fanya na mnyonge akafanya anapandishwa mahakamani basi hatuna nchi sisi hapa.kwa hiyo viongozi wote waliokuwa madarakani wakati ule wajieleze moja baada ya mwengine mpaka tupate joka kubwa tuliuwe ndio tutaendeleya laa sivyo itakuwa kama tunachezo mdako au bao tu asante sana.hapa ndipo alipo malizia kusema na mpaka sasa watu wengi sana wana taka mamba haya yawekwe wazi ili familia na dungu na jamaa walio uliwa dungu zao wao kuwa serekali haichanguwi wala haibaguwi je yatafanywa haya.....? na serekali hii ya viraka....?

WABUNGE NA MAWAZIRI WA SEREKALI YA TANGANYIKA WAULIWA KWA KUTUMIYA SUMU NA AJALI ZA MAGARI JE NI NANI ANAYE WAUWA...?

SittaEAC1
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha kuwa hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.
Amesema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.Waziri Sitta alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu.
“ Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.
Alisema suala hilo la kulishwa sumu ambalo limempata Waziri si la kawaida hivyo Polisi wanatakiwa kufanya uchunguzi ili kupata ukweli.Alisema kuendelea kukaa kimya kwa kisingizio cha ushahidi, kitawatisha Watanzania wengine kuwa wanaweza kufanyiwa chochote na sheria isifuate mkondo wake.
Juzi Waziri Nahodha alimtaka Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu.
Alisema ushahidi wa suala hilo ukiwasilishwa ndipo uchunguzi unaweza kufanyika.
Kauli hiyo ya Nahodha ilikuja baada ya Jumapili iliyopita, Waziri Sitta akiwa na kundi la makada wenzake wanaojipambanua kuwa wapambanaji wa ufisadi alirejea kauli yake ya awali kuwa Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela alilishwa sumu.
Sitta alisema hayo katika uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam.
“ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisema Sitta na kushangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
“ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida,” alisema.Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.
Tangu Dk Mwakyembe arejee nchini Desemba 2011 kutoka katika Hospitali ya Apollo, India alikokuwa akitibiwa maradhi yaliyosababisha ngozi yake iharibike, Jumapili iliyopita ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonekana katika hadhara ya watu.
Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Kahama, James Lembeli, Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Hilda Ngoye, aliyekuwa Mbunge wa Vunjo, Alloyce Kimaro na Mjumbe wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Makonda.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dk Mwakyembe aliapa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi.Alisema, “ Nilifika Hospitali Oktoba 10 (mwaka jana) na tangu wakati huo sikuweza kuvaa viatu lakini leo hii naweza kuvaa viatu, kwa hiyo shetani ameshindwa.na pia tume tambuwa kuwa
Hili sio jambo geni kwa serekali ya tanganyika ((Tanzania)) Mh Sitta kumbuka kuwa Benjamen Mkapa ndani ya Usalama wa Taifa anakundi lake la ujasusi ambalo hulitumilia kwa vitendo vya aina, unakumbuka Kipindi Mkapa yuko Swezaland huku Wazanzibar wanapigwa risasi 26/27 2001?.
Ile ilikuwa ni mipango rasi imepangwa yeye asafiri hujuma zitokee, baada ya kubanwa sana katika mauwaji ya 26/27 Dr Omari ali Juma alisema yeye hahusiki anaye husika ni Amir wa nchi ambaye alikuwa ni Raisi Benjamen Mkapa .
Mkapa kuona hivyo akajuwa huenda Dr Omari ata vobowa mengi kwa vile Dr Omar alikuwa ni mtu wakuropokwa ropokwa Mkapa akatuma vijana wake wa Mshuhulikie na akashuhulikiwa kimya mpaka leo je munakumbuka kifo cha sokoine pia vipi kilikkuwa na wapi mwisho wake mpaka leo kimya na wengine wengi tu, na hata upande wa cuf lilizimwa kwa kuwa Hamad Rashid yeye na Mkewe wote ni Usalama wa Taifa na ndio Nyerere alikuwa anampenda sana na kufika hadi hata kupewa nafasi nyingi nyeti katika serekali.sitta unamjuwa anaye wauwa viongozi mtaje basi apelekwe kwenye koti kuu huko nchini uholanzi kama wenzake wengine ulimwanguni maana kauwa wananchi wengi sana pemba na unguja.ila munanyamaza maana munaogopa atawashuhulikia na nyinyi pia ikiwa mutafunguwa madomo yenu au sio...sitta saba nane.

MADIKTETA BAADA YA MADIKTETA MPAKA LINI MAMBO HAYA WAZANZIBAR AMKENI MUSIWAPIGIE KURA MADIKTETA

HUYU NI IDDI AMIN DADA
NA HUYU NI IDDI AMINI DADA
JE WANANCHI WA ZANZIBAR MUMELEWA....?

“WAWAKILISHI WAKO  SOLIDARITY SIO CCM AU CUF, TUWAGAWE TUWATAWALE”       THAT IS VP2 SEIF IDD
Inasikitisha kwa mara nyengine tena kiongozi aliyechaguliwa kuitetea na kuikomboa Zanzibar kutoka kwa huu Muungano FEKI usiokuwa halali, anafika kusema nirahisishieni kazi kwani Wawakilishi hivi sasa wako Solidarity sio CCM au CUF katika masuala ya Muungano.
Hapa kweli tunakiongozi au KABURU ambaye anadhirisha wazi kwamba lengo  ni kuona Wawakilishi wa CCM na CUF wanatafautiana katika kuitetea Zanzibar kwenye huu Muungano wa Watanganyika waliojivika koti la ((Tanzania)).
Kiongozi wa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar anasema maneno ambayo msingi wake mkubwa ni kuwagawa Wawakilishi hivi kweli tutafika na mtu tapeli kama huyu JI KABURU KUBWA.
Yeye na wengine malengo ni kuhakikisha Raslimali zote za Zanzibar zinakuwa mikononi mwa Watanganyika na ndio maana anawaogopa Wawakilishi kwa kauli yake hii ya tuwagawe na tuwatawale..
Kwa taarifa yako Mzee umekwenda mrama lengo na dhamira yenu imeshajulikana na Wazanzibar kwa kupitia Wawakilishi wao wako kitu kimoja na moto umeshawaka hakuna wa kuuzima.
Huyu VP2 anatakiwa aitwe kwenye Baraza la Wawakilishi na kijueleza kwanini haheshimu maamuzi ya Bazara la wawakilishi, Mafuta na Gesi tayari yameshaondolewa kwenye mjadala, kitu gani kinachoendelea kuzungumzwa na Serikali ya Mapinduzi kwenye hivi vikao vya Watanganyika.
Hii inadhirisha wazi kwamba huyu Balozi Iddy Amini DADA ni miongoni mwa kundi la Shamuhuna kutokuheshimu maamuzi ya Baraza la Wawakilishi.na kama hawaheshimu basi dawa nikulazimishwa kujiuzulu kama alivyo ambiwa shamhuna ajiuzulu maana wao wanaona vyeo walivyo navyo basi zanzibar imekuwa kama nyumba ya marehe baba zao na wao ni kaka wakubwa watafanya watakalo sio hii ni nchi sio nyumba.
Kimtazamo wangu anatakiwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kushindwa kusimamia mamuzi ya vikao vya baraza la wawakilishi kwa hiyo ajiuzulu.
Anafanya mambo kwa matakwa ya Watanganyika na pia huyu Makamo wa Rais Gharib Bilali anatakiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ndio itakuwa mwisho wake na asiruhusiwe tena kukanyanga zanzibar kama ilivyo katazwa JOHN OKELLO kuto kukanyanga tenza zanzibar na huyu afanyiwe hivyo hivyo.Wakati ndio huu, wajumbe tayarisheni hoja ya dharura kuiwasilisha barazani kuwaondoa hawa jamaa sio wenye kuitetea Zanzibar.
Mungu ibariki Zanzibar na watu wake

HAWA NDIO MAZIMWI YANAYO WALA WATU WA ZANZIBAR NA ZANZIBAR YENYEWE

Capture
HAWA NDIO MADALALI NA MAZIMWI WAKU WA KUIFANYA ZANZIBAR IMEZWE NA DOMO LA JINI TANGANYIKA NA HAWAHESHIMU HATA MAMUZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI MBELE YAKUJIPENDEKEZA KWA MABWANA ZAO KUZITOWA RASILIMALI ZA WATU WA ZANZIBAR.
Namnukuu huyu Dalali wa Zanzibar aliokuwa tayari anapingana na mamuzi ya Baraza la Wawakilishi,aliokosekana hapa Giningi ni Spika wa Zanzibar Pandu Ameri Kificho huyu ndie hujifanya Stakafiri Mungu mtu katika Baraza.Lakini asisahau tu kuwa upeyao ndio uvumawo yeye ameshakuwa shaib tayari yuko kati ya dunia na Akhera hivi sasa ana vijukuu na asome sana kuhusu uadilifu na kuhusu makemeo ya M/mungu kuhusu zulma na mali za mayatima.pili akaye akijuwa walikuwepo kama yeye hapo zanzibar na kibri kuliko yeye na kutaka kudidimiza zanzibar kwa kujinufaisha wao na familia zao na sasa wote wamo makaburini wanakula joto ya jiwe.
a). Katika majadiliano hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Dr Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazo husika kutowa maelezo ndani ya kipindi cha miezi mine utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia.
b.) Kuzibiti uharamia wa utekaji meli katika Bahari kuu, hii mana yake katika ufahamu nikuwa Gharibu Bilali anataka kutumia Ujanja wa kigezo hichi ili kuletewa Cost guard Jesh ili liseme linalinda Uharamia wa Wategaji meli kumbe ni kulinda Wachimbaji mafuta ya Zanzibar wasiwe na Bugza.
Hawa ndio eti Wazalendo wa Zanzibar.MAWEEEEEEE
NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.
Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.
Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.Kimsingi, Zanzibar in mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena.
Inashangaza kuwa kwa miaka sasa Zanzibar imekuwa ikipaza sauti kuwa hairidhiki na jinsi Muungano unavyoendeshwa. Lakini, wahusika walichokifanya, na ambacho wamekuwa wakiendelea kusisitiza kukifanya, ni kiini macho walichokipa jina la kutatua kero za Muungano.na hii yote nikuwa wamezoe hawa kuwadanganya wananchi kwa ubale wa kanga na mapanga na jazi za mpira lakini wao wanavimba kama vyura wenye mimba kisha wanasema nchi masikini sasa hatutaki tena sisi ndio rai na sisi ndio tutakao endesha nchi mukitaka musitake au nyote tutawafanya kama gaddafi musitulete upumbavu.na sisi sasa tunawao na munaonekana kuwa ni majuha ni kuwa kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakiendelea na kiini macho hicho cha kutatua kero za Muungano lakini badala ya kwisha, kero zimekuwa zikiongezeka.
Ajabu ni kuwa wanaonekana kuwa hawaoni kuwa kero zinaongezeka badala ya kupungua licha ya juhudi zao za kushughulikia kero za Muungano.Kwangu mimi, ilichokifanya Zanzibar mpaka hivi sasa ni njia za kuonyesha kistaarabu kuwa hairidhishwi na Muungano kwa sababu Wazanzibari wanaamini kuwa hauzingatii masilahi ya Zanzibar. Na walichokifanya wahusika ni kutumia nguvu kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kujiamulia mambo yao.Walianza kudai kwa maneno tu, wakaonekana hawana hoja, wakakataliwa. Kwa kuwa walidhamiria kuendelea kudai kile wanachoamini kuwa ni haki yao, wakaanza kufanya baadhi ya vitu kwa vitendo.Wakabadilisha sheria kadhaa ambazo kimsingi zinakiuka kabisa makubaliano ya Muungano kama ilivyopo sasa. Walipoona upande wa pili haujashtuka, wakaamua kubadili na Katiba kabisa. Lakini, inaonekana bado wahusika hawaelewi hawa jamaa wanataka nini.Kitakachotokea sasa, sidhani kama ni kosa la Wazanzibari kwa sababu kama ni onyo walishalitoa na wakadharauliwa.Upo msemo kuwa paka akibanwa kwenye kona, anaweza kugeuka kuwa chui. Hilo ndilo litakalotokea kwa Zanzibar. Kwa sababu imebanwa sana katika azima yake ya kutaka Muungano ambao una masilahi kwake, sasa itageuka kuwa mbogo kweli kweli. Na dalalili zimeanza kuonekana.Zipo chockochoko za chini kwa chini ambazo zinawahusisha watu wa kawaida tu hivi sasa. Wapo watu wenye asili ya Tanganyika huko Zanzibar ambao wameanza kunyanyaswa na watu wa kawaida tu wa Zanzibar.Kwa maelezo yanayotolewa, inaonyesha kuwa hilo ni suala la uhalifu wa kawaida tu ambao hata Tanzania bara upo, ingawa haulekezwi kwa Wazanzibari.
Lakini kwa wanaotaka kukiita kitu kwa jina lake halisi wanaelewa fika kuwa chokochoko hizi zina uhusiano ya kutoridhishwa kwa Zanzibari katika masuala ya Muungano. Wahusika hawataki kulikubali hilo lakini hiyo haibadilishi ukweli wa suala hilo.Kwa kuwa tumeamua kuficha maradhi, tusubiri kifo kituumbue. Naamini kuwa Zanzibar haitachoka wala kuacha kudai haki zake ndani ya Muungano. Na kwa jinsi mambo yalivyo,viongozi wezi,majambazi,walafi,watapia mloo miroho ya mali isiyo tosheka kwa walivyo iba tayari wataendelea kukataa kutekeleza matakwa hayo.Kwa kuwa suala hili limeshafika kwenye ngazi ya wananchi, ambao wameamka baada ya kuona kuna viongozi wao wengi tu ambao wana mawazo kama yao, tusitarajie kuwa litakwisha hivi hivi.Nadhani viongozi walafii wana hofu ya kuvunjika kwa muungano. Lakini wafahamu kuwa kuvunjika huko kwa Muungano kunaweza kuwa ndio suluhisho la kujenga Muungano mwingine utakaokuwa imara kwa sababu uta jengwa chini ya maridhiano ya pande mbili zikikubaliana kuungana.Lakini, ni kweli kuwa  Zanzibar inabanwa sana kiuchumi ndani ya muungano na hivyo kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuisaidia ikajitanua. Itaisaidia pia Tanganyika iwapo itakuwa na jirani tajiri.na ikiwa mutaileta zanzibar kuwa huru bila ya kusababisha machafuko kwanza kisha ndio muilete kuwa huru wazanzibar hawatakuwa na imani na nyinyi tena kwa hiyo hata wakiwa matajiri vipi hawata watiza nyinyi tena na Kuendelea kulazimisha Muungano huu kutatuletea maafa hapo baadaye. Imeshajidhihirisha kuwa Wazanzibari hawataacha kudai haki zao mpaka wazipate.Na itafika wakati Watanganyika nao watakapochoka na chokochoko hizo na wao kuamua kuanza kudai haki zao kwa hila na kwa nguvu. Sijui kama viongozi walafii miroho isiyotosheka kuwa walivyo iba tayari kama watakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na Watanganyika na Wazanzibari watakapoamua kudai haki zao kila mmoja kivyake.
Kuna nafasi adhimu ambayo viongozi wetu wanataka kutukosesha bila sababu za msingi. Kwa mtu anayepima upepo, atagundua kuwa watu wengi hawaridhishwi na aina ya Muungano uliopo. Na kwa hakika kabisa, miongoni mwa watu hao ni viongozi wetu wengi tu.Tatizo ni kuwa waliopo madarakani hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kuwa ndio walioshiriki kuua Muungano. Wana hofu kuwa Zanzibar ikiruhusiwa kutoka basi Muungano utakuwa umekufa. Ile fursa kuwa kuondoka kwa Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuunda Muungano imara wala hawajaiona.Wamejawa hofu ya kihistoria iliyopatia upofu wa masuala dhahiri kuwa kwa kulazimisha Muungano, eti tu kwa sababu ulianzishwa na waasisi wa taifa nao sio wa asisi wa taifa maana sio walio zitowa nchi ktk mikono ya wakolo ni wengine kisha wao wakawau viongozi wengine na kujiweka wao kuwa ndio wasisi kisha wakaunganisha ili wasipinduliwe kwa hiyo ilikuwa sio muungano wa nchi mbili bali ni kujihami kwa nchi mbili na hawa viongozi wa sasa majizi malafii wanaungangania na kudhani watakuwa wanadumisha utaifa. Lakini kama wakiamua kufungua macho, watabaini kuwa wanachokifanya kinaua utaifa.Kama nilivyoeleza awali, Zanzibar haiwezi kuendelea kuvumilia kulazimishwa kuwepo ndani ya Muungano. Itafika mahali itageuka mbogo na kulazimisha kile inachokitaka. Itakuwa vigumu sana kuzuia na kudhibiti hali ya mambo wakati huo.na mifano tushaiyona ktk nchi tafauti duniani.Kama tunataka salama, ni heri tukaiacha Zanzibar iondoke kwenye Muungano sasa hivi kwa amani na utulivu, nasi tutabaki salama huku tukiwa na uwezekano wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu zaidi.Lakini iwapo tutasubiri mpaka Zanzibar, au hata Tanganyika, ikaamua kujiondoa kwa nguvu, hatutabaki salama na wala hakutakuwa na uaminifu uliobakia wa kuwa msingi wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu.