Thursday, February 2, 2012

JE RAISI WA ZANZIBAR NDIYE AMIRI JESHI MKUU WA JESHI LA ZANZIBAR AU NIKIJIBARAKA TU CHA AMIRI JESHI WA TANGANYIKA...?


WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelieleza Bunge kuwa, Rais wa Zanzibar si Amiri Jeshi Mkuu.
Waziri wa Wizara hiyo, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema leo kuwa,tanganyika ((Tanzania)) ina Amiri Jeshi Mkuu mmoja ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa ((Tanzania.))FEKI
Dk. Mwinyi ametoa msimamo huo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), ambaye aliuliza ni sheria ipi imempa mamlaka Rais wa Zanzibar kuteua vikosi maalum vya ulinzi hivyo kusababisha TANGANYIKA ((Tanzania)) iwe na maamiri jeshi wakuu wawili ndani ya nchi moja.((HAKUNA NCHI MOJA NCHI NI MBILI MUKITAKA MUSITAKE))
Kwa mujibu wa Dk. Mwinyi, Katiba ya Zanzibar ndiyo inayompa Rais wa Zanzibar kuteua idara maalum za ulinzi kikiwemo Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Mafunzo.
Awali wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), Dk. Mwinyi aliwaeleza wabunge kuwa, jukumu la ulinzi majini ni na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) na kwamba, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (NAVY) inalinda Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema, kuna mikakati ya kuiimarisha Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, kivifaa ili pia kuliwezesha kupambana na maharamia wa Kisomali.((uzushi mtupu somalia iko wapi na zanzibar iko wapi kama ni kupambana si kenya wanayo NAVY ila huu ni uzushi tu natusipo angali tutatiwa tena vita kama vita vya uganda na tanganyika kisha dungu zetu wakauliwa na kufanywa viwete mpaka leo hawajalipwa))
Kai alisema, usalama wa Zanzibar unatokana na bahari hivyo alitaka kufahamu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) ina mikakati gani kukisaidia kikosi cha KMKM.
“Si rahisi kuisaidia KMKM kivifaa kwa sababu hata Navy yenyewe haijajitosheleza” amesema Dk Mwinyi.
Wakati anajibu swali la msingi la Mbunge huyo, Dk Mwinyi alisema, Katiba ya TANGANYIKA  inaruhusu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuunda na kuweka TANGANYIKA(( Tanzania)) majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania)) ukiwemo wa maeneo ya bahari na maziwa ya nchi yetu.
“Jukumu la ulinzi wa maji katika maeneo yote ya Jamuhuri ya Muungano wa TANGANYIKA(( Tanzania)) linatekelezwa na JWTZ kupitia Kamandi ya Jeshi la la Wanamaji (NAVY)” amesema Dk. Mwinyi.
Amesema,Serikali ya Jamuhuri ya Muungano imekuwa ikiisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa mafunzo kwa maofisa na askari wa KMKM.
Wakati huohuo, Dk. Mwinyi amesema, amewaeleza wabunge kuwa, hakuna wakati au mazingira yatakayolifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania)) (JWTZ) kufanya kazi za ndani badala ya Jeshi la Polisi.((HII SIO KWELI MAANA KILA CHANGUZI JESHI LIMEUWA WAZANZIBAR NA POLISI PIA KWA HIYO JESHI LANAFANYA KAZI NDANI YA KUTUWA SISI HAPA PEMBA NA UNGUJA WAKATI WA UCHANGUZI))MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU.SEMENI KWELI.
“…bali Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANGANYIKA(( Tanzania ))linaweza kusaidia pale Jeshi la Polisi linapoelemewa na kuoombwa kufanya hivyo” amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Mwinyi, msaada wa JWTZ kwa shughuli za ndani si katika masuala ya usalama wa ndani tu, bali jeshi linaweza kuombwa kusaidia katika shughuli nyingine inapobidi kama vile shughuli za uokoaji, ujenzi hususani nyakati za dharura na majanga((NA HASWA WAKATI WA UCHANGUZI WATUWE NA KUHARIBU DADA ZETU MPAKA TUKAKIMBILIA MOMBASA 20001 AU MUSHASAHAU AU MUNAJISAHAULISHA................?

No comments:

Post a Comment